Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nilikuwa na mahusiano na pisi kali balaa (mchepuko), kutokana na uzuri wake akawa ananipiga mizinga mara kwa mara, mpaka ikafikia nikawa navaa suruali moja kauka nikuvae.
Kutokana na uzuri wake, pamoja na mizinga aliyokuwa ananipiga; nikaamua kumuwekea mazingira abebe ujauzito wangu.
Kweli haikupita muda, kitu kikajaa; mbaya zaidi akawa bado ananibana kwenye shoo; ila siku akinipatia lazima awajibike ipasavyo.
Sasa kutokana na uzuri wake, tukawa tunavutana sana hapa na pale; mpaka ikafikia hakuna kuwasiliana. Mpaka sasa hivi nina kama miezi mitatu sina mawasiliano naye.
Sasa leo nimepumzika zangu mchana, naona simu yangu inaita; kuangalia ni namba ngeni, ikabidi nipokee.
Kuna dada akajitambulisha, mimi ni W dada yake V (mchepuko), nilikuwa nakupa taarifa V yupo hospitali, (akawa anongea huku analia), ikabidi nimbembeleze, akanyamaza.
Nikamuuliza tatizo ni nini? Akasema V anatakiwa afanyiwe 'operation' mtoto ni mkubwa ana 4kg; kwa hiyo tunahitaji sapoti kidogo.
Nikajaribu kufikiria mbwembwe za muhusika, ila nikasema kwenye kupambania uhai, huwa tunasahau yote; ingawa sikuwa na bajeti yake, ikanibidi nijibane ninavyoweza niweze kuwafanikishia.
Baada ya kama lisaa limoja na nusu hivi, akanipigia simu; amejifungua salama na mtoto ni mzuri kweli kweli, dume kama dume equation x na mama yake yuko salama.
Basi nikamshukuru mungu, na kuahidi tutakuwa bega kwa bega pale patakapotokea changamoto.
Kwa hiyo wakuu, nimeshaongeza mpiga kura mwigine; pia nashauri masista duu wapunguze mizengwe mizengwe kwenye mahusiano; panapokuwa na changamoto huwezi kujua nani atakuwa karibu.