Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Fahari ya kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2022
Posts
545
Reaction score
1,908
Wakuu mama mjamzito amefariki wakati namzalisha baada ya kumwaga damu nyingi hali iliyopelekea kufariki hii tukio linastress sana na kunipa posttraumatic syndrome nalijitahidi kadri ya uwezo wangu kiukweli nilipaniki sana je maternal death ( kifo cha mjamzito) inaweza kufungiwa leseni yangu na kufukuzwa kaZi?

Halmashauri( CHMT) wasimamizi wa afya ngazi ya halmashauri wameniambia nisimuhumudumie mgonjwa, mjamzito au mteja yoyote yule)
 
Pole sana mkuu, hilo ni tukio zito sana. Kifo cha mama mjamzito hakimaanishi moja kwa moja kwamba utapoteza leseni au kazi; inategemea uchunguzi kubaini kama kulikuwa na uzembe, ukiukwaji wa taratibu au kosa la kitaalamu.

Kwa kuwa CHMT imekuelekeza usimhudumie mgonjwa kwa sasa, fuata maelekezo hayo kwa maandishi ikiwezekana, lakini omba ufafanuzi wa sababu, muda wa zuio na hatua zinazofuata. Usisaini maelezo yoyote ya kukiri kosa bila kupata ushauri wa kisheria. Pia hifadhi kumbukumbu zote za mgonjwa na tukio kwa usalama na kwa mujibu wa taratibu za kituo.

Kisheria, unaweza kuomba wakili au mwakilishi wa chama/chombo chako cha kitaaluma akusaidie wakati wa uchunguzi. Na kwa kuwa umesema tukio limekuacha na dalili za trauma, tafuta pia msaada wa kitaalamu wa afya ya akili.
 
Ndiyo shida ya kuanzisha watoto shule wakiwa na miaka 4, anamaliza diploma akiwa na miaka 20.

Ona sasa mambo madogodogo kama haya hata bado haujui.

Na unapataje PTSD kwa changamoto ya kazi yako, kitu ambacho ni unajua kabisa in one way or another litatokea tu.

Sasa kama unapata PTSD kirahisi hivi, si confidence yote ya kuhudumia watanzania itaisha?
 
Huu sio muda wa kumtia lawama ni hali ambayo inaweza kumtokea daktari yyte
 
Pole sana mkuu..

Unaweza usipoteze kazi ila ni muda wa kukaa chini na kufanya tathmini kama uendelee na hio kazi??,; kupanic na kupata PTSD litajirudia mara ngapi in the future?! Sababu nature ya kazi yako ni utakutana na same scenario tena na tena......
 
Pole dokta,kifo cha mjamzito sio mchezo na mbaya zaidi lawama wanapewa wahudumu hata kama yeye hahusiki. Usipaniki,cha muhimu tunza kumbukumbu zote muhimu ambazo zitakuokoa huko mbele. Haya mambo ni magumu hapa Bongo,picha linaanza wajawazito hawahudhurii kliniki ipasavyo,dawa muhimu hawatumii,yaani anakuja kujifungua tayari anachungulia kaburi. Hapo bado unakuta hospital haina vifaa vya kutosha,mara damu hamna, lakini kifo kikitokea lawama kwa daktari.
Naamini utashinda hili mkuu.
 
Bila sheria ya kuwashtaki madaktari kwa mamilioni na kupoteza license zao za udaktari hawataacha uzembe, najua watu wawili walipoteza maisha kwa ujinga kabisa, wote baada ya operation walipata infections kwa vitu vilivyoachwa ndani yao na procedure hazikufuatwa, mimi mwenyewe niliwahi kupewa wrong diagnosis & prescription za uwongo kabisa
 
Wakuu mama mjamzito amefariki wakati namzalisha baada ya kumwaga damu nyingi hali iliyopelekea kufariki hii tukio linastress sana na kunipa posttraumatic syndrome nalijitahidi kadri ya uwezo wangu kiukweli nilipaniki sana je maternal death ( kifo cha mjamzito) inaweza kufungiwa leseni yangu na kufukuzwa kaZi?

Halmashauri( CHMT) wasimamizi wa afya ngazi ya halmashauri wameniambia nisimuhumudumie mgonjwa, mjamzito au mteja yoyote yule)

Pole sana; hiyo changamoto inatokea kwa baadhi ya kinamama na ikitokea unatakiwa uwe very proactive; Omba msaada chap kwa dactari wa zamu au Dactari yoyote akusaidie au Senior nurse kama hakuna Dactari.
Muhimu zaidi ni kumchoma sindano ya kupunguza damu kutoka; lakini pia kuongezewa damu chap kwa
haraka ili hata kama inaendelea kutoka kidogo kidogo; isimuishie.

Kumbuka Dactari anauwezo wa kutoa maelekezo chap, mgonjwa akahamishiwa hospitali kubwa au akaomba damu kutoka kituo cha jirani au hata ikitokea changamoto ndiye ataandika report.
Sasa sijui kama ulikuwa kwenye hospitali ya ngazi gani hivyo siwezi kuongea zaidi.
Kukuambia usitoe huduma; wanataka tu kujiridhirisha kuwa ulifuata taratibu zote za dharura ili kuokoa maisha
 
Back
Top Bottom