Wakuu, mnapambana vipi na changamoto za ununuzi wa bidhaa nje ya nchi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Wakuu, katika harakati zangu za biashara, nikakutana na kampuni B mtandaoni.

Kutokana na bidhaa zao walizozichapisha kwenye ukurasa wao, ziliweza kunivutia sana na kunishawishi kufanya nao biashara.

Nikapiga mahesabu, mpaka nizilete hapa bongo, naweza kupata faida mara mbili.

Nikawasiliana nao, na wakawa wananitumia picha mbalimbali za bidhaa zao.

Nikawa nimeridhika, ikafuata utaratibu wa malipo na usafirishaji.

Ili mzigo uweze kusafirishwa, nilitakiwa niulipie pamoja na gharama za usafiri, ndipo mzigo utatoka ofisini kwao na kuanza kusafirishwa.

Kutokana na huo utaratibu, na kwa kuwa hatuaminiani, nikaamua kulipia mzigo kidogo wenye thamani ya mil. 1.3 kuliko kuwekeza sana kisha nipate hasara kubwa.

Baada ya kulipia, waliupaki kwenye mabox wakiwa wameuandika jina la mpokeaji na kunitumia picha na kuniahidi baada ya siku 7 mzigo utakuwa umefika.

Kutokana na walivyokuwa wameupaki nikawa na uhakika mzigo utafika.

Lakini cha ajabu, mpaka leo mzigo haujafika, simu zangu hawapokei wala kujibu, na siku zimepita zaidi ya wiki 3.

Kimoyomoyo imenibidi nikubali, nimepigwa tayari.

Ingawa nimepoteza, nachukulia kama funzo la kutokumuamini mtu yeyote katika biashara.

Je, kwa upande wako hizi changamoto unapambana nazo vipi?​
 
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: shipping from our factory to your local warehouse : USD 3460
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: total USD 5710
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: including import taxes, process ,all ...
 
Vipi kampuni ya Usafirishaji ulitumia ipi!?
Si vizuri kutaja jina la kampuni husika, ila kampuni ya usafirisha iliyopo nje walinipigia kwa w/app, ile namba ikajisoma kwenye simu yangu 'automatically' jina la hiyo kampuni ya usafirishaji, na kuniakikishia mzigo wameupokea, ndipo nikawamini.

Kumbe ni mchezo wa IT

Kutembelea ofisi yao hapa bongo, wakasema hawana taarifa zozote na huo usafirishaji, bali hao ni matapeli.​
 
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: shipping from our factory to your local warehouse : USD 3460
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: total USD 5710
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: including import taxes, process ,all ...
Ni kuwa nazo makini tu; hela niliyopoteza imenibidi niifanye kuwa ada ya kuhitimu kujua huu utapeli.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa mwagizaji wa bidhaa hasa china....OGOPA supplier yeyote unayekutana naye facebook, instgram au tiktok etc..USITHUBUTU WENGI NI MATAPELI ..Sehemu salama sijawahi pata matatizo more than Five years ni Alibaba..ingawa sometimes mara chache unaweza pata bidhaa chini ya ubora...
NJIA YA PILI ..Ukijipanga nenda hizo nchi kama ni china au turkey au india etc ukatengeneze masupplier wako then uwe unafanya nao kazi ukiwa tz ila sio kwa kiwango kikubwa cha pesa kuwatumia...mimi supplier mmoja na nayemwamini maximum kumtumia haizidi 2 mill..
So , mambo ya kupigwa hapo utayaepuk sana
 
Wakuu, katika harakati zangu za biashara, nikakutana na kampuni B mtandaoni.

Kutokana na bidhaa zao walizozichapisha kwenye ukurasa wao, ziliweza kunivutia sana na kunishawishi kufanya nao biashara.

Nikapiga mahesabu, mpaka nizilete hapa bongo, naweza kupata faida mara mbili.

Nikawasiliana nao, na wakawa wananitumia picha mbalimbali za bidhaa zao.

Nikawa nimeridhika, ikafuata utaratibu wa malipo na usafirishaji.

Ili mzigo uweze kusafirishwa, nilitakiwa niulipie pamoja na gharama za usafiri, ndipo mzigo utatoka ofisini kwao na kuanza kusafirishwa.

Kutokana na huo utaratibu, na kwa kuwa hatuaminiani, nikaamua kulipia mzigo kidogo wenye thamani ya mil. 1.3 kuliko kuwekeza sana kisha nipate hasara kubwa.

Baada ya kulipia, waliupaki kwenye mabox wakiwa wameuandika jina la mpokeaji na kunitumia picha na kuniahidi baada ya siku 7 mzigo utakuwa umefika.

Kutokana na walivyokuwa wameupaki nikawa na uhakika mzigo utafika.

Lakini cha ajabu, mpaka leo mzigo haujafika, simu zangu hawapokei wala kujibu, na siku zimepita zaidi ya wiki 3.

Kimoyomoyo imenibidi nikubali, nimepigwa tayari.

Ingawa nimepoteza, nachukulia kama funzo la kutokumuamini mtu yeyote katika biashara.

Je, kwa upande wako hizi changamoto unapambana nazo vipi?​
Epuka kabisa suppliers unaokutana nao FB Insta Ticktock na pop up adv online…….. Huko kumejaa Matapeli wa kinaijeria

Hakikisha una deal na suppliers wa uhakika kama Alibaba
 
Si vizuri kutaja jina la kampuni husika, ila kampuni ya usafirisha iliyopo nje walinipigia kwa w/app, ile namba ikajisoma kwenye simu yangu 'automatically' jina la hiyo kampuni ya usafirishaji, na kuniakikishia mzigo wameupokea, ndipo nikawamini.

Kumbe ni mchezo wa IT

Kutembelea ofisi yao hapa bongo, wakasema hawana taarifa zozote na huo usafirishaji, bali hao ni matapeli.​
Next time Wacheki ofisini kwanza. Itasaidia
 
Back
Top Bottom