Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Tusubirie ushuhuda mbalimbaliNi vyema ukaitaja hiyo kampuni uokoe na wengine mkuu
Ulishawahi kukutana na hii changamoto?Inasikitisha sana!
Ilishapoa ingawa inaumaPole sana
Vipi kampuni ya Usafirishaji ulitumia ipi!?
Nje ya nchiOfisi zao unajua zilipo?
Ni kuwa nazo makini tu; hela niliyopoteza imenibidi niifanye kuwa ada ya kuhitimu kujua huu utapeli.[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: shipping from our factory to your local warehouse : USD 3460
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: total USD 5710
[7/20, 09:23] Lisa_chicken cage,gabion: including import taxes, process ,all ...
Umetumia eBay!Ni kuwa nazo makini tu; hela niliyopoteza imenibidi niifanye kuwa ada ya kuhitimu kujua huu utapeli.
Epuka kabisa suppliers unaokutana nao FB Insta Ticktock na pop up adv online…….. Huko kumejaa Matapeli wa kinaijeriaWakuu, katika harakati zangu za biashara, nikakutana na kampuni B mtandaoni.
Kutokana na bidhaa zao walizozichapisha kwenye ukurasa wao, ziliweza kunivutia sana na kunishawishi kufanya nao biashara.
Nikapiga mahesabu, mpaka nizilete hapa bongo, naweza kupata faida mara mbili.
Nikawasiliana nao, na wakawa wananitumia picha mbalimbali za bidhaa zao.
Nikawa nimeridhika, ikafuata utaratibu wa malipo na usafirishaji.
Ili mzigo uweze kusafirishwa, nilitakiwa niulipie pamoja na gharama za usafiri, ndipo mzigo utatoka ofisini kwao na kuanza kusafirishwa.
Kutokana na huo utaratibu, na kwa kuwa hatuaminiani, nikaamua kulipia mzigo kidogo wenye thamani ya mil. 1.3 kuliko kuwekeza sana kisha nipate hasara kubwa.
Baada ya kulipia, waliupaki kwenye mabox wakiwa wameuandika jina la mpokeaji na kunitumia picha na kuniahidi baada ya siku 7 mzigo utakuwa umefika.
Kutokana na walivyokuwa wameupaki nikawa na uhakika mzigo utafika.
Lakini cha ajabu, mpaka leo mzigo haujafika, simu zangu hawapokei wala kujibu, na siku zimepita zaidi ya wiki 3.
Kimoyomoyo imenibidi nikubali, nimepigwa tayari.
Ingawa nimepoteza, nachukulia kama funzo la kutokumuamini mtu yeyote katika biashara.
Je, kwa upande wako hizi changamoto unapambana nazo vipi?
Next time Wacheki ofisini kwanza. ItasaidiaSi vizuri kutaja jina la kampuni husika, ila kampuni ya usafirisha iliyopo nje walinipigia kwa w/app, ile namba ikajisoma kwenye simu yangu 'automatically' jina la hiyo kampuni ya usafirishaji, na kuniakikishia mzigo wameupokea, ndipo nikawamini.
Kumbe ni mchezo wa IT
Kutembelea ofisi yao hapa bongo, wakasema hawana taarifa zozote na huo usafirishaji, bali hao ni matapeli.