Wakuu Msaada: Biashara haiendi ghafla, nifanyeje?

Unajua kuwa mambo ya Mungu ni imani kama ulivyo uchawi, na imani ili ifanye kazi kwako lazima uiamini vinginevyo haitokuwa na athari kwako.

Mleta mada tayari kashaanza ngonjera sijui nani aliomba elfu kumi wateja wakakoma, sijui Ex alisemaje... Tayari kwenye akili yake ameshajenga picha ya uchawi, jambo ambalo ni ngumu kumwaminisha kuwa hakuna anaye mloga.
 
Pole sana mkuu
 
weka mbili tatu , sio mgeni sana kivile , ila hii hali haikuwah kuwepo
Mm ni mvivu kuandika. Kwa ufupi sana. Kwenye biashara mchawi ni wewe mwenyewe na mentality yako. Pili unatakiwa uhue kuwa mishahara ya watu ndio chanzo kikuu cha mzunguko wa fedha kitaa. Mishahara ikitoka kila biashara inauza, chips, nguo, vyakula na huduma zingine. Muuza chips akiuza akapata pesa anakuja kununua nguo. Hivyo tarehe za mshahara zikipita hali huwa tete.

Mishahara mingi hutoka kwenye tarehe 20-30 kutegemea na taasisi na watu hufanya mtumizi ya hio pes kwenye tarehe 20 hadi tar za 5+ za mweizi unaofuata kisha pesa hupungua. Hivyo ukishusha mzigo kwenye tare za 7-18 hivi tegemea mauzo ya chini haijalishi mzigo ni mzyri kiasi gani. Zingatia uzuri wa mali haumfanyi mtu kununua ila uhitaji na uwepo wa pesa+uzuri wa ali ndivyo humfanya mtu nunue.

Mm huwa nashusha mzigo mara mbili kwa mwezi. Tarehe za 16+ nikivizia mishahara watu wakianza kupata tu mzigo mzuri uwepo na tarehe za 2+ hapo mishahara ndio huwa imepamba moto na mzigo huu hunipeleka hadi zile tarehe kudunduliza.

Lingenze kwenye bishara zangatia sana bidhaa iliyokutambulisha sokoni, hio ndio ishikirie. Tengeneza identity yako kwamba kwa flan kuna bidhaa flan uhakika, usiwe mtu wa kurukaruka na kujaribu kila bidhaa kisha unaacha.

Kuna jirani zangu wawili wanauza mitumba. Kila siku wanatuhumiana uchawi mm nipo neutral tu hivyo huwa wananiletea tuhuma. Shida ya haya mamo ukiyaamini tu, hata nguvu na akili ya ubunifu inashuka unaanza kutafuta mchawi. Bei ya bidhaa ni mchawi wa kwanza. Weka bei nzuri ili kila mtu aje kununua, wapo wale vibopa ambao wao pesa yao sio ya kuchungulia hao wakiingia huwa tunawalipua tu ila hawa wengine wauzie bei ndogo kumbuka siku hizi kila mtu anauza nguo kama sio duka basi mtandaoni.

Mm kuna jirani yangu anauza nguo bei ghari sana watu wakiingia kwangu wanakuta bei kitonga tu wanaanza kumsema. Mm naweza nikauza nguo kwa faida ya buku mbili tu. Ila watu wengi sana wanaelekezana dukani kwangu. Utaskia mteja anakuja anakuambia "unamjua flan, kanielekeza nije kwenye duka flan kuna nguo mzuri kwa bei nzuri" hicho ndio muhimu kwenye biashara yetu. Tengeneza msingi wa biashara yako kwanza kwa faida ndogo, baadae utapata faida kubwa sana baada ya kuaminika.

Mwisho kuto kuuza kwa mida wa siku 3 ni kawaida kutegemea na location uliyopo. Mm mwanzoni ilikua inanipa shida sana akilini ila baada ya kuilewa trend sina shida kabisa. Muhimu usipouza unaenda kwenye kioo unajiuliza nini shida. Hapa na namaanisha pengine umebadili bdhaa, mfano mwanzo ulikua na nguo official sasa una za disco. Ila kama mali ni ileile basi utauza. Pia kuna issue ya upepo wa pesa kitaa. Kuna muda pesa huadimika kabisa. Inaweza kupita hata wiki hivi kila mtu aanalia pesa hakuna hada boda hawapati abilia, hapo jua shida sio ww, ni lesa imeadimika. Wachumi wanajua kua BOT ndio inayo control haya mambo. Kuna muda huwa wanaamua pesa zirudi serikalini kwa sababu flaniflani, hili huna maamuzi nalo.

Biashara ni mentality yako pia, utakachokiamini kinaweza kukufanikishia. Humu kuna watu watakuambia fanya hivi fanya vile zote imani tu. Mm kuna jamaa huwa anatambeza viatu. Huwa ahaendi kuiza hadi apite dukani kwangu ili nimbariki, hio ni kila siku. Na kweli huwa nikimbariki anaenda anauza. Kuna siku hadi aliwahi niletea hela eti baraka zangu zinamsaidia, niliikataa. Jana alikuja nikambariki baada ya lisaa akatuma text hii nimeimbatanisha. Mm naamini kwenye biashara kuna watu wanahitaji watu wa kuwapa maneno ya kuwatia moyo ili wasonge. Ndio maana kuna mtu yeye na wachungaji. Wachungaji wanachompa ni maneno tu ya kumtia moyo kitoka hapo amejaa anaenda kutekeleza na anatoboa kweli kumbe angeweza kufanya kwa juhudi ileile na akafanikiqa bila mchungaji.

Nimechoka kuandika, Goodluck
View attachment 2616551
 
Bwana Yesu asifiwe.



Leo alioshea Chumvi na magadi.

Na Mungu kasaidia, Mauzo yamekuwepo Si haba.
 
Shukran Mkuu !!
 
Kuna watu wengi wamebarikiwa kwenye biblia bila kutoa fungu la kumi
Hayo mafundisho hapo juu ndiyo yanayowageuza wakristo watumwa.

Mchungaji mchawi mchawi ndio anaweza kukuchezea mapichapicha kama haya ya huyo Mzee aliyesafiri.

Muhimu mwenye duka ashike Imani kuwa ni MUNGU aliyeruhusu mauzo kukauka ..aombe Toba na rehema MUNGU huyo huyo ataruhusu mauzo kurejea.Kuna kitu MUNGU anataka ujifunze kwa hili
 
Wale mademu uliojitapa umewala kimasihara ndo wamekupa nuksi
 
Nenda kwa Nabii Clear Malisa!
 
Lakini watu wengi wamebarikiwa KWA kutoa fungu la kumi pia ni swala la imani ndiyo maana mwisho nikasema kama unaamini hilo, asante mkuu KWA mchango wako.
 
Daah, hii aya mwisho imechanganywa mpaka imenichanganya na mimi sasa😩
 
Kama unaushaidi anachoma mpaka TRA nenda kaonane na meneja wa TRA eneo husika elezea story ilivo kama Kuna vitisho vya tra ulisikia akivitoa x wa bidada kuhusu tra na kwel baada ya sku kadhaa wakaja mweleze hawatorudia tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…