Wakuu Msaada: Biashara haiendi ghafla, nifanyeje?

Wakuu Msaada: Biashara haiendi ghafla, nifanyeje?

Ni Duka langu la Nguo , Sasa Wiki ilopita Niliingiza Mzigo Mpya , katika hali isiokawaida Mara nyingi Nikishaleta Mzigo Mpya , nikiwapigia wateja wangu, Huwa Ndani ya Siku Mauzo nikaribuu 150K

Kijana ananiambia Alikuja Jiran ( Jiran naye ana frame pemben ya Huduma yake) akamuomba elfu Kumi, na alipompa tu Toka hapo Hajauza .

Mara ananiambia, Kuna Mwanamke Alikuja kama mteja, akaishia kushika shika Nguo weee akasepa, tokea hapo Biashara imesimama.

Wakuuu ,hamna Mauzo toka Ijumaa mpaka Leo Jumanne, hamna hata Mia, Mzigo Mpya, Kila mtu akija anausifiaaa Sanaa, lkn anaishia kusema nitarudi ila harudiii.

Wakuuu hata Mia, hata Miaaa!!

Au niamin tu ni hali,,,, ndio Kuna Siku Mauzo yanakua kiduchu ila huwez kosa Hata 30K.

Naondoaje Hili Jinamizi ?? ... Ni Duka ambalo niliamua kulifungua Kwa ajili ya Mwanamke ( Singo mama, nilizaa naye ) hivo nikalifungua ila Kila kitu anakisimamia yeye maana mtoto wetu alipata shida fulan ivi ivo sikutaka zile simu za mara Kwa mara za Hela .

( Huyo jamaa alomuomba Kijana elfu Kumi, ni rafiki wa aliyekua Mume wa Singo mama huyu nlozaa naye, na huyu alokua Mume amekua akimtangaza na kumuombea mabaya sana huku akisema Biashara yenyewe itafungwa tuu, Jamaa ana cheo Kwa tawi Moja la vya Dola, amekua anamchomea sana utambi Hadi mpaka TRA inafikia wakati wanataka kutuongezea Kodi bila sababu za msingi. ).
Chai
 
Matunda huonekana baada ya mti fulani kukua vizuri. Na mti mzuri ni matokeo ya uimara wa mizizi yake. Hata mtumie mafuta ya kila aina, chumvi za kila namna...kama tatizo halijashughulikiwa in the roots mtakua mnatwanga maji kwenye kinu.

Kuna the root of this problem..na naamini ndani yako ama yenu mnaijua...its either muamue kukata mizizi kabisa ama just keep on playing these to and fro games..thou miaka inazidi kwenda..Mr G!
If this is offensive to you just ignore it Sir.
 
Mbona wakati unauza sana dukani kwako hukutushirikisha???ni hali ya kawaida hasa katika maisha mf:kuna wakati utafurahi na kucheka sana,,,lakini kuna wakati pia utakuja wa kulia na huzuni ,,,,Endelea na biashara!!
 
Option nyepesi ni kuchoma moto hilo duka la jirani yako ambaye ndiye mshindani wako wa karibu. Na duka lolote ambalo lina bidhaa kama zako karibu na wewe.

Now kuchoma moto mali za watu utakamatwa kwa arson hivyo fikiria ni tukio gani linaloweza fanania na kuchoma moto katika mazingira ambayo ni halali kisheria.

  • Ongeza awareness kwa wateja ya bei.
  • Ongeza bidhaa zinazosaidiana kwa hizo zilizopo mfano unauza nguo ongeza accessories.
  • Tangaza umeshusha bei kwa 5%
  • Kisha go back to basics. Kwa sasa fanya biashara kama kplindi cha mara ya kwanza unaifungua.

Ukiona hayo yote magumu go with the first option. Choma moto maduka yote ya karibu
 
Hapo ndipo tatizo linapoanzia, naomba kifungu kinachoonyesha inabidi kuwapa fungu la kumi viongozi wa dini?
Wewe huenda una matatizo ya akili, naomba unionyeshe sehemu nilipoandika kwamba uwape fungu la kumi viongozi wa dini? Kinachofata nakuweka ignore list, sasa unaniambia kuwapa tithing viongozi wa dini kitu ambacho sijakisema. Embu ACHA KUKAA ndani jichanganye na watu huenda unapitia msongo wa mawazo. Siyo kila kitu lazima ucomment
 
Ungelikua unamtegemea Yesu huyu tunayemjua wala usingekuja hapa ungemwambia huko sirini. Hakika hutauza kwelikweli mpaka umtegemee ipasavyo
Mkuu namwamini sana maana amenipigania katika mengi.

Ila siunajua mtu mzima akipatwa jambo?.
 
Sijamaliza kusoma. Ila wewe unajifunza biashara. Utahanvaika sana, nami nafanya biashara kama yako. Bodo una safari ndefu hadi uijui hii biashara
weka mbili tatu , sio mgeni sana kivile , ila hii hali haikuwah kuwepo
 
Matunda huonekana baada ya mti fulani kukua vizuri. Na mti mzuri ni matokeo ya uimara wa mizizi yake. Hata mtumie mafuta ya kila aina, chumvi za kila namna...kama tatizo halijashughulikiwa in the roots mtakua mnatwanga maji kwenye kinu.

Kuna the root of this problem..na naamini ndani yako ama yenu mnaijua...its either muamue kukata mizizi kabisa ama just keep on playing these to and fro games..thou miaka inazidi kwenda..Mr G!
If this is offensive to you just ignore it Sir.
Nitalipitia Hii Mkuu wangu!!.
 
Kwa Sasa niliamua Kumtegemea Yesu, masuala ya waganga niliachana nayo Toka kile kipindi Cha Jaji na Kesi yetu ya Shamba.

Ila nahitaji Mbinu mnazotumiaga kuondoa mabalaa kama haya Kwenye Biashara zenu
Tayari umeshjiroga Kiongozi...ila Kwa Sasa sisi wateja wako mahitaji yetu ya Msingi ni afya ,afya,afya...ie chakula nadawa!
Ila uchawi upo!😊
 
Biashara ya nguo

1.Biashara ina muda gani?

2.Wateja wako wengi ni wa aina gani? Wapita njia au online waangalia status?

3.Unavufaham vipindi/majira tofauti ya mwaka kwa biashara yako?
Mwaka mmoja na miezi Kadhaa Kwa hili .

Wapita Barabara kutoka na eneo, wa mtandao ni wale ambao nawafaham ambao Huwa ni wkaudumu.

Tarehe za kuanzia 23---10 Huwa Kuna Mauzo sana, na Mizigo yangu Huwa napeleka kutokana na majira
 
Tayari umeshjiroga Kiongozi...ila Kwa Sasa sisi wateja wako mahitaji yetu ya Msingi ni afya ,afya,afya...ie chakula nadawa!
Ila uchawi upo!😊
🤣🤣🤣 Nahapa namaliza kunywa chai niwahi Kikao Cha Asubuhi Cha Hosp.
 
Wewe huenda una matatizo ya akili, naomba unionyeshe sehemu nilipoandika kwamba uwape fungu la kumi viongozi wa dini? Kinachofata nakuweka ignore list, sasa unaniambia kuwapa tithing viongozi wa dini kitu ambacho sijakisema. Embu ACHA KUKAA ndani jichanganye na watu huenda unapitia msongo wa mawazo. Siyo kila kitu lazima ucomment
Ngoja nicheke kwanza, Kwa nini mtu kama hakijui kitu, na akiwa amekalilishwa anakuwaga mkali bila sababu,Kwanza mimi sikai huko Tanzania mnakoongoza kwa kuwa na msongo wa mawazo,

Huku ninakoishi lazima nitoke nikatafute,sababu inabidi nilipie parmity au kibali cha kuishi kila mwaka, zaidi ya milion 2 kwa mwaka
 
Uchawi upo kwenye ubongo wako tayari, ni ngumu kuutoa.
Unavitiko eti kwenye ubongo wako,labda nini kinakufanya useme hivyo kama ni imani basi kwenye vitabu vya dini vinabainisha wazi.

Uchawi upo toka Dunia ilivyoumbwa maana nguvu inayotumika katika uchawi imetoka kwa huyo huyo Mungu maana yeye ndio chanzo cha kila kitu hapa Duniani.
 
Biashara Zina mambo mengi, Kuna siku nimefungua tu nakuta ndani funza balaaaa, na siuzi bidhaaa kusema zimeoza!! Nauza tu vitu vya Ujenzi!!
Nilisafisha na kendelea na kazi hata hivyo sikuwa na Imani na lile tukio!!....... Mwisho wa siku nikapata ufumbuzi
 
Back
Top Bottom