Wakuu Msaada: Biashara haiendi ghafla, nifanyeje?

Wakuu Msaada: Biashara haiendi ghafla, nifanyeje?

Lazima kuna kitu kimabadilika ghafla ambacho mwanzo hakikuwako katika biashara na sasa kimekuwako.

Hizo superstitious beliefs zako weka kando kwanza anza kutafiti kisayansi ni mambo gani yamefanyika ndipo utapata jawabu.
 
Nimeuchukua ushauri wako ,Mimi Huwa naendapo Mara Moja Moja sana, na huyu Bidada ni mbishii mnoo.

Nitakwenda Mwenyewe Mkuu.
 
Mnaomjibu huyu jamaa sijui anawaonaje? Mwanzo kabisa namkariri kasema “Ni Duka langu la Nguo , Sasa Wiki ilopita Niliingiza Mzigo Mpya , katika hali isiokawaida Mara nyingi Nikishaleta Mzigo Mpya , nikiwapigia wateja wangu, Huwa Ndani ya Siku Mauzo nikaribuu 150K” ukiendelea katikati anasema “ Ni Duka ambalo niliamua kulifungua Kwa ajili ya Mwanamke ( Singo mama, nilizaa naye ) hivo nikalifungua ila Kila kitu anakisimamia yeye…”
Kiufupi mleta mada hajielewi au anataka kuwatangazia biashara masingo maza wa humu waingie mkenge kwake kuwa atawafungulia biashara
Acha mawazo yasokuwepo Mkuu.

Ni Duka nilolifungua mwenyewe Kwa Pesa yangu Kwa ajili ya Mwanamke niliyezaa naye mtoto kuepusha usumbufu wa Mizinga ya Mara Kwa mara Kwa kigezocha mtoto

Kwahivo Ni Duka langu,hapohapo ni Duka la Bidada wangu.
 
Mnaomjibu huyu jamaa sijui anawaonaje? Mwanzo kabisa namkariri kasema “Ni Duka langu la Nguo , Sasa Wiki ilopita Niliingiza Mzigo Mpya , katika hali isiokawaida Mara nyingi Nikishaleta Mzigo Mpya , nikiwapigia wateja wangu, Huwa Ndani ya Siku Mauzo nikaribuu 150K” ukiendelea katikati anasema “ Ni Duka ambalo niliamua kulifungua Kwa ajili ya Mwanamke ( Singo mama, nilizaa naye ) hivo nikalifungua ila Kila kitu anakisimamia yeye…”
Kiufupi mleta mada hajielewi au anataka kuwatangazia biashara masingo maza wa humu waingie mkenge kwake kuwa atawafungulia biashara
Kwa kifupi tumepigwa bakora , kamba na chai kwa wakati m'moja. Lo lo lo lo lo lo lo jamani.
 
Mkuuu umelogwa ww kaa chonjo aseeeeeeeeeee.

Hiyo ishawahi mtokea ndugu yangu hiyo elf 10 uliyotoa ni chuma ulete nakupa week 3 hesabu hiyo ni hasara tupu
Ndo namm nmehisi, Sasa Ananipigia analia kwelikweli, nmemuambia wachanitafute mbinu mitandaoni
 
Hivi kuna uhusiano gani ya chumvi ya mawe na mambo ya giza?!

Anayejua anijuze maana kuna shangazi yangu ukienda kuzoa chumvi aliyomwaga kwenye nyumba yake unaweza kupata gunia tatu za kilo 100.
Ina ondoa negative energy
 
Bidada wangu anawaamin hao akina Mwaposa, na kipindi kaja Mkoan kwetu, alinunua Katoni la maji na mafuta chupa Tano.

Kwamwaga wee wapi !!.
😀😀😀😀😀kama ni mkatoliki kachukue yale ya kanisani
 
Kiukweli mkuu kama kweli umesema unamtegemea yesu embu soma hapa
Malaki 3:8_9
Malaki 3:10
Mimi nina ushuhuda wa mtu ninayemfahamu alikuwa ni boss wa duka la nguo za kiume kama biashara YAKO, akawa amesafiri kaachia mfanyakazi jamaa alikuwa ni lazima atoe fungu la kumi yule mfanyakazi akapewa maagizo mauzo yote kwanzia j3 mpaka jmosi piga hesabu ya faida nipe nitoe fungu la kumi baada ya kusafiri yule mfanyakazi akawa hafanyi hivyoo wee alikaa wiki 3 mfululizo ajauza na watu wanaingia KWA nadra sana dukani na boss hana habari yyte maana anajua fungu la kumi jumapili lazima ipelekwe na mfanyakazi kumbe hafanyi hivyo alirudi akamsimamisha KAZI alivyoanza tu kutoa fungu la kumi mambo yakawa safi, nimekujibu kutokana na umesema kwamba unamtegemea yesu japo kuna wengine hawaamini haya mambo jaribu kumtolea MUNGU
Shukrani Mkuu, Ahsante Kwa kunikumbusha hili, ninachompendea zaidi huyu Mwanamke ,ni mwenye huruma sana, anasaidia wahitaji, nahisi Kwa Hilo ndio linafanya anaumizwa.

Siunajua Binadam.
 
Back
Top Bottom