Wakuu muongozo wa kununua bidhaa AliExpress na Amazon

Mbalizi feedstuff

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2025
Posts
238
Reaction score
269
Ninaomba mchakato wa kununua bidhaa hasa Amazon. Nahitaji mwongozo kutoka kwa ambaye amewahi kununua bidhaa kupitia jukwaa tajwa.

Ninachotaka kufahamu ni details gani zinajazwa, hela ya supplier inakatwaje, mzigo naupokeaje na kodi nakatwaje, je, mambo gani ya muhimu ya kuzingatia kuhusu usalama wa kufanya transaction? Na mwisho, nataka kujua mambo ya shipping fee ita-apply kwa kila item niliyonunua? Natanguliza shukrani za awali.
 
Ninaomba mchakato wa kununua bidhaa hasa Amazon.
Kuna njia mbili
1. Jihudumie kwa kufuata mwongozo hapa:
=
2. Tumia mtu mwenye uzoefu wa zaidi ya Miaka kumi hapa Jukwaani:
- Hapa tuweke kumbu kumbua sawa: Thread nilianzisha (Start date Aug 19, 2016) ikiwa na maana kwamba Mwaka huu (Aug 19, 2026) Huduma ina zaidi ya Miaka kumi.
==
Huduma bado Active, Angalia Picha.
 
Mkuu, nimewahi kufuatilia utaratibu wa manunuzi ya online. Cha msingi ni kuangalia bei ya bidhaa pamoja na gharama zote za kuifikisha Tanzania. Kodi, shipping na clearing vinaweza kufanya bidhaa ionekane nafuu mtandaoni lakini ikafika kwa gharama kubwa.

Ushauri wangu:

1. Tumia malipo rasmi ndani ya platform husika na epuka kutuma pesa nje ya mfumo kwa mtu usiyemjua.

2. Hakikisha seller ana reviews nzuri na bidhaa ina maelezo sahihi.

3. Angalia kama shipping inafika Tanzania na kama kuna tracking number.

4. Kabla ya kulipia, hakikisha unaelewa gharama za shipping, ushuru wa forodha na gharama za kampuni ya usafirishaji.

5. Shipping inaweza kutozwa kwa kila bidhaa au kuunganishwa kulingana na seller, aina ya usafirishaji na kama bidhaa zinasafirishwa pamoja.

Pia, Amazon na AliExpress zina taratibu tofauti. Kwa anayeanza, ni vizuri kuagiza bidhaa moja yenye thamani ndogo kwanza ili kujifunza mchakato kabla ya kuagiza mzigo mkubwa. Muhimu zaidi ni kujua gharama ya mwisho mpaka bidhaa ifike mikononi mwako, si bei iliyoonyeshwa kwenye tovuti pekee.
 
Pia, Amazon na AliExpress zina taratibu tofauti.
Na akienda kichwa kichwa, Mzigo ataukimbia pindi ukifika hapa nchini, kutokana na Tozo/kodi/ushuru/tbs/agency fee

Uzuri wa JF Refence(Rejea) zipo, Ingia hapa post namba 25:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…