Wakuu mwanamke huyu kwenye mzunguko wa hedhi, siku zake za hatari ni zipi?

Wakuu mwanamke huyu kwenye mzunguko wa hedhi, siku zake za hatari ni zipi?

issac77

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
4,128
Reaction score
7,899
Hedhi anakaa siku 3 hadi 4,

Mara nyingi kwenye siku anaingia kati ya tarehe 26, 27 na 28 kila mwezi.

Je, kwenye mzunguko huu hapana tatizo?,

je mzunguko huu ni wa siku ngapi?

Je, kwenye mzunguko huu siku zake za hatari ni zipi?
 
Mkuu kwa siku hizo za hedhi kukaa ni kawaida, kwa ajili ya suala la siku za hatari adownload app inaitwa “Flo” apo atajua mzunguko wake hua ni siku ngapi na siku za hatari kila kitu
 
Mkuu kwa siku hizo za hedhi kukaa ni kawaida, kwa ajili ya suala la siku za hatari adownload app inaitwa “Flo” apo atajua mzunguko wake hua ni siku ngapi na siku za hatari kila kitu
Kwa sasa anaetaka kujua ni mimi, mkuu, inamaana hapo siku za hatari haziwezi kung'amuliwa mpaka hiyo app?
 
Hedhi anakaa siku 3 hadi 4,

Mara nyingi kwenye siku anaingia kati ya tarehe 26, 27 na 28 kila mwezi...
Kutokana na knowledge niliyonayo 28 days circle maana yake anaanza siku ya 11 hadi 17 katika hiyo circle ni za hatari, kwakuwa fertilization inaanza siku ya 14 ambayo yai linaingia kwenye mirija ya uzazi kutoka kwenye ovary hivyo ukisex nae siku ya 11 sperm zinakaa masaa 72 ndipo zinakufa Kwahiyo 11 yai itazikuta sperm siku ya 14 zikiwa zinasubiri, naomba kuishia hapo maana hii kitu imenisababishia kupata watoto wa kiume tuu
 
Period ya 28 days siyo sahihi. Kuingia hedhi kila tarehe 26, 27, au 28 haina maana kwamba period (muda tangu one menstrual flow hadi nyingine) nayo ni 28. Wrong mathematics.
 
1. Lini aliingia period mara ya mwisho? 28th possibly
2. Menstrual flow inakaa siku ngapi? 4
3. Menstrual cycle in siku ngapi? (30 days?)

Siku za rutuba (fertile days) ni tarehe 8 hadi tarehe 17
Ovulation inapaswa kuwa tarehe 12
 
Mzunguko inahesabika tangu tarehe anayoingia hedhi hadi tarehe nyingine anayoingia, fafanua kuhusu hesabu zako navyofahamu mwanamke siku ya 14 hata kama anaenda siku 30 ndiyo huwa best target ya kupata mimba ambayo sperm zinakuwa na afya ya kutosha na siku za hatari ni kuanzia ya 11-17 katika mzunguko wake wa hedhi hakuna cha kutoa siku za kutoka damu
 
Hedhi anakaa siku 3 hadi 4,

Mara nyingi kwenye siku anaingia kati ya tarehe 26, 27 na 28 kila mwezi.

Je, kwenye mzunguko huu hapana tatizo?,

je mzunguko huu ni wa siku ngapi?

Je, kwenye mzunguko huu siku zake za hatari ni zipi?

Mambi ya msingi na kuzingatia:
1: Mzunguko wa mwanamke (urefu wake), huesabiwa toka siku anapoona tone la damu/siku ya kwanza mpaka siku kabla ya tone la damu la mzunguko unaofuata/siku ya mwisho. Hii huleta idadi kamili ya mzunguko wa kawaida, ambayo ni kati ya siku 21 -35 kwa mzunguko wa kawaida/regular.

2: Kutoka kwenye hizo jumla ya siku/urefu ndo huweza kufanyika hesabu kujua siku ambazo kuna uwezo wa yai kupevuka/ovulation/siku ya hatari/siku njema/fertile period kulingana na lengo.

3: Siku hiyo namba mbili hapo juu hubadilika kulingana na urefu wa mzunguko ambao ni namba moja juu.

4: Hivyo bila kutoa siku ambazo alianza kupata damu na kukamilika kwa mzunguko, angalau kwa miezi/mizunguko mitatu mfululizo si rahisi kupata jibu mwafaka hapo juu.

5: Pia kuna wale ambao mizunguko yao ni irregular, urefu unabadilika kila mzunguko pia wao huangaliwa kwa mtizamo tofauti kidogo.

Hivyo, ili kupata jibu mwafaka ni mpaka upate jibu la namba nne (4) hapo juu.
 
1. Lini aliingia period mara ya mwisho? 28th possibly
2. Menstrual flow inakaa siku ngapi? 4
3. Menstrual cycle in siku ngapi? (30 days?)

Siku za rutuba (fertile days) ni tarehe 8 hadi tarehe 17
Ovulation inapaswa kuwa tarehe 12
26-18=8
28-11=17
Hebu fafanua hii kanuni
 
Back
Top Bottom