Wakuu naomba niwaage humu Jf nimepashindwa kwa kweli

Du ndg yangu Abbasfarudume , imenibidi nicheke na kumkumbuka yule mwanamziki Husen Machozi aliyeimba nitoke vipi... Zilipendwa sasa. Lakini nadhani utakuwa umeghairi kuaga kwa leo na hutokaa ufanye hivyo. JF ni sehemu ambayo huwezi kuwa bored hata kidogo, always kuna vitu vipya na kuna almost kila kitu. Unaweza kumpuzika tu kama uko busy lakini ukipata nafasi unarudi tena na tena.

Mwisho kabisa ushauri katika uandishi wako mkuu, jitahidi kuandika vizuri, weka nukta/kituo pale ambapo inatakiwa kiwekwe, weka koma pale ambapo inatakiwa iwekwe, anza paragraph mpya nk. Ukiandika habari ndefu haina hivyo vitu na pia ina makosa ya kiuandishi ni rahisi sana watu kuipotezea na mwisho wa siku utaishia kuona kama jamii hii haikupendi ama ina ubaguzi. Hapa JF tulio wengi hatufahamiani kwa sura wala majina halisi, hivyo siyo rahisi sana kuwa na hizo element za ubaguzi nk.

Ahsante wana Jf nadhani mmemuonesha upendo wa hali ya juu sana ndugu yetu Abbasfarudume na nina imani ameghairi kusudio lake la kuondoka.
 
Ahsanteee mkuu wangu kwa mawazo, na ushauri wako nzuri, na pia ahsante sana kwa Comments Ubarikiwe sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji12] [emoji12] Nimesema nimehairisha sitoki tena Jf.
 
Kwaheri mkuu ila naona hata kule huonekani au nako uliaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…