Wakuu naombeni msaada wa ramani Kali ya kisasa chumba sebule jiko choo

Wageni wanini tena maisha haya yaani nianze kupiga hesabu za wageni tena mimi mbona siendi kulala kwao Kila mtu afe na chake
Mkuu ongeza bajeti ya bati 6 na saruji mifuko minne, ili uongezee chumba kimoja hapo, viwe vyumba viwili kama walivyokushauri wadau wengi hapo juu.

Mimi ni mzoefu sana na ni mtaalamu wa ramani.

Neema ya leo hauna 'mandate' ya kuimiliki kesho isipokuwa kwa kudra za M/Mungu pekee.

Leo unapobarikiwa kufanya jambo jema kama hili usilifanye kimzaha, lifanye kwa ukamilifu unaoweza kuumudu kwa kuongezea bajeti kidogo.

Kukushauri kuongeza chumba kimoja kunamaanisha kwamba bajeti kidogo iliyoongezeka hapo haiwezi kukushinda, pia ikitokea ukakwama huko mbele za safari baada ya kujenga nyumba hii, yaweza kukusaidia kukidhi maisha yako yote yaliyosalia bila ya kuwa umebanana sana.

Kama utanielewa nitakuchorea ramani ya vyumba viwili, sebule, jiko na mfumo wa vyoo kwa namna utakavyopenda self au viwe kwa mtindo wa public.

Nb: material ya kuongezea chumba kimoja kwenye ramani ya chumba kimoja ni machache tofauti na kujenga chumba kimoja kinachojitegemea, kwa hiyo usihofie ukubwa wa gharama.
 
Kumbuka hapo lazima niingie bajeti ya tiles alminium na grill mzee hapo tayari inakua imenicost pesa nyingi jumlisha na mlango hapa Mimi nataka nijenge nyumba ndogo ila Kali ninavyoweza kuimudu sio kujenga pagale
 
Huyu hapana, atanisumbua ๐Ÿ˜‚
Atasema hata sitting room tuweke kochi moja la 2 by 2.. kisa tuko wawili
Mim sitokusumbua hakika tutajenge Casri๐Ÿ˜Ž na sitocheka na wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ