Kuna design unaweza fanya choo na bafu vikawa chumba kimoja kisha nje ya choo na bafu kunakuwa na open space nyingine ambayo ukiamua unaweza ifanya kama sehemu ya kupigia mswaki/kunyolea au kubadilishia nguo pia yaan ikawa kama walk in closet. Hivyo kunakua na milango miwili yaani mpaka uingie chooni itakubid ufungue milango miwili, wapili ukiwa huo wa chooni na unakua usawa/mstari tofauti na mlango wa kwanza.
Au ukaamua tu chumba chako kikawa kama master ila choo inakua kwa nje pembeni ya chumba.
Hapo hata ushushe mzigo unatoa harufu kama yai viza aliyepo chumbani hawezi sikia harufu.
Kuna vipimo pia vya kuzingatia hapo.