Hizi design za choo cha master bedroom ukiwa na wife, mmoja wenu tu kiingia chooni kushusha mzigo akishatoka tu kama upo room harufu yote lazima uusikie yani.
Mkuu ni makosa sana kukariri jambo bila kulifanyia utafiti wa kuridhisha.
Nukuu za kukariri mambo namna hii zinaweza kukufanya ukaishi maisha ya dhiki bila kujali una ukwasi kiasi gani.
Choo cha chumba cha 'self' kinatakiwa kijengwe kwa utaalamu wa hali ya juu sana kwa kufuata kanuni zinazotakiwa:
bomba la kutoa taka kwenda kwenye sept tank lilazwe kwa kutumia vipimo sahihi, lisiegeme kwa mlalo wa slop kali ili takataka zinaposukumwa na maji zisiweze kubakia.
Kukiwa na slop kali, maji hukimbia kasi na kuacha takataka na vinyesi nyuma, hivyo kuzalisha harufu na baadaye bomba kuziba.
Tumia pima maji ili mlalo wa bomba usiwe mkali, liegeme angalau 0.5-1cm, ukiliangalia kwa macho makavu waweza kudhani lina ulalo wa kulingana.
Chemba ya nje kwenye ukuta wa chumba cha choo ni lazima ili kujenga Exsozy ya kutolea hewa chafu itakayoelekezwa juu kwa urefu usiopungua 5-6 mtrs.
Katika kuunganisha sink la choo na bomba la maji taka lazima pawe na kitovu(siweki majina ya kitaalamu kurahisisha uelewa) kinachounganisha sink na bomba, ili unapo flash pabakiwe na maji yanayozuia harufu kurudi nyuma.
Sink zuri kwa choo cha self ni lile la kukaa(siielezi faida yake na raha yake), lisiwe la kuchuchumaa, chagua quality nzuri ili flash tank yake isikusumbue.
Kama umekijenga kwa vipimo sahihi, hakuna harufu itakayosalia baada ya kujissidia na kuflash.
Pia pasikose sabuni ya maji na brush ya kuclear kama ikitokea kuna masalia ya harufu ama mabaki ya kinyesi kwenye sink baada ya kuflash.
Halafu, weka urinal sink(sink la kukojolea wanaume).
Mwanaume kukojolea kwenye sink la choo kunaweza kusababisha kero itokanayo na harufu ya mkojo usipozingatia kusafisha kwa umakini na mkojo usiposafishwa kwa maji, uelewe kuwa una harufu kali sana kuzidi hata ya kinyesi.
Kama utakuwa umejenga bila sink la mkojo, hakikisha toilet paper haikosi, kila unapokojoa mwanaume, lazima ukaushe mabaki ya mkojo yanayokuwa yamedondokea kwenye seat, maana wanaume tuna tabia ya kukung'unta, sijui nani hutufundisha huu mtindo!
Choo kikijengwa kienyeji kwa kuruka ama kukosea vipengele vya ujenzi, hauwezi kuvumilia kukaa katika master room yako kwa raha kutokana na harufu ya kukera itakayozalishwa chumbani mwako.
Maana harufu pamoja na gas inayozalishwa kwenye septic tank ina tabia ya kutafuta upenyo wa kutoka, hivyo hufuata mabomba kurudi nyuma.
Choo chako cha ndani ukikipatia kukiset vizuri waweza kuwa unasomea magazeti ama kuchatia humo, bila usumbufu wa harufu yoyote.
Mkuu umejenga kwa gharama halafu tena uanze kukimbia kimbia kwenda msalani na mama watoto kama vile bado upo kwenye nyumba za kupanga!