Wakuu naona kama town (Dar) kumekuwa na matumizi mabaya ya ving'ora

Wakuu naona kama town (Dar) kumekuwa na matumizi mabaya ya ving'ora

Hata jana usiku wakati wa tamasha la miaka thelathini ya bongo flavor walikuwa wanapiga sana ving'ora
 
Tunapoelekea tutafunga hadi kwenye scania
Mbona vipo vile vya taa na mpaka kwenye mabasi hasa haya ya mikoani. Kimulimuli ni fungu moja na king'ola na hivi ndio vimeshamili.
Nasikia machawa wote wameruhusiwa kufunga ving'ola (ili wawahi kuchawika) nashangaa mleta mada haujui huu ulimwengu wa machawa ukoje.
 
Mbona vipo vile vya taa na kwenye mabasi. Kimulimuli ni fungu moja na king'ola na hivi ndio vimeshamili.
Nasikia machawa wote wameruhusiwa kufunga ving'ola (ili wawahi kuchawika) nashangaa mleta mada haujui huu ulimwengu wa machawa ukoje.
Uchawa ni wa kujipendekeza i mean sio chawa wa faida
 
Wazee inakuwaje siku hizi unaweza kuwa unapita zako labda Maandazi Road mara ghafla V8 inawasha king'ora ili mumpishe.. yaani imekuwa kero kubwa. Wakazi wa Dar wanakutana na ving'ora vingi kwa siku. Ifikie sehemu mamlaka zinazohusika zidhibiti hii hali.

Kwani idadi ya viongozi au watendaji wa serikali wenye haraka imeongezeka? Kama vipi ving'ora viwekwe kwenye magari yanayokidhi vigezo vya kusheria. Au kama vipi sheria ifanyiwe marekebisho kupunguza idadi ya wanaostahili kupita na kung'ora.
Dodoma ndo hovyo kabisa, hata afisa mtendaji wa kata anawasha kinora kisa tu ana ki OPA chake
 
muongozo wa ving;ora na vimulimuli umetolewa wiki kama mbili tatu hivi hapa nyuma, sijabahatika kukariri jina la muongozo ila umeangazia mambo hayo


thecitizentz
Edited•5w
Following widespread complaints from road users nationwide, the Tanzanian government has enacted regulations prohibiting the unauthorised installation of sirens and beacon lights on private vehicles, introducing fines of up to Sh300,000 for offenders.

The regulations, titled the Road Traffic (Siren, Sound Signals, Whistles and Warning Flashing Lights) Regulations, 2026, were published in the Government Gazette on June 19, 2026, under the Road Traffic Act, Cap 168, and gained public attention after circulating on social media on Thursday, August 13, 2026.

Issued by the Minister for Home Affairs, Mr Patrobas Katambi, the law restricts the use of sirens and specific beacon light colour combinations to emergency vehicles and seven distinct categories of top government officials.

Installing these devices without a formal permit from the minister is now a criminal offence.

The law targets a growing trend of drivers, particularly those operating luxury SUVs, long-distance passenger buses, commercial trucks, autorickshaws, and motorcycles, arbitrarily fitting VIP lights and sirens to bypass traffic congestion or evade police checks.

Security officials noted that unauthorised beacon lights have also been used as cover to smuggle illicit cargo, such as khat, through checkpoints under the pretense of carrying high-profile dignitaries.

Read more on The Citizen website



KANUNI MPYA ZA UDHIBITI WA VING’ORA VISIVYO RASMI, TAA ZA VIMULIMULI KUANZA KUNG’ATA
Ndugu Msomaji
Serikali imechapisha katika Gazeti la Serikali, Kanuni mpya za Udhibiti wa Ving’ora na taa za vimulimuli, kwenye magari barabarani. Kanuni hizo zinajulikana kama Sheria ya Usalama Barabarani (Kanuni za Ving’ora, Ishara Zinazosikika, Filimbi na Vimulimuli) za 2026, Tangazo la Serikali Na. 151 la tarehe 19/6/2026, yaani THE ROAD TRAFFIC (SIRENS, AUDIBLE SIGNALS, WHISTLES AND FLASHING BEACONS) REGULATIONS, 2026, Government Notice No. 151 Published On 19/6/2026. Katika mfululizo wa Makala hizi, tutakuletea sehemu ya Kwanza ya Makala itakayoangazia matumizi ya Kanuni na misafara inayoruhusiwa kuwa na ving’ora na Vimulimuli.
Matumizi ya Kanuni
Kanuni hizo zitatumika kwa magari rasmi ya Viongozi na magari ya dharura yaliyoidhinishwa.
Use of Siren,Audible signal,Whistle, and Flashing Beacons
Kwa mujibu wa Kanuni, ving’ora na taa za vimulimuli zitatumika kwenye magari ya Viongozi yafuatayo:
(a) Kwa upande wa Msafara wa Rais, Msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za rangi Nyekundu na Nyeupe pamoja na king’ora cha sauti;
(b) Kwa upande wa Msafara wa Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar, msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za rangi Nyekundu na nyeupe na king’ora cha sauti;
(c) Kwa upande wa Msafara wa Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za njano (amber) na nyeupe na king’ora cha sauti;
(d) Kwa upande wa msafara wa Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Naibu Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi, Msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zenye mwanga wa Bluu na Mweupe pamoja na King’ora cha Sauti;
(e) Kwa upande wa msafara wa Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, msafara utakuwa magari yenye kimulimuli/bikoni zenye mwanga wa Bluu pamoja na King’ora cha sauti, wakiwa katika kazi zao za kiofisi.
(f) Kwa misafara ya ma-Rais wastaafu. Msafara utakuwa na magari yenye ving’ora vya sauti na taa za ukungu (fog lights) bila kimulimuli.
Haya ndiyo Makundi sita yanayostahili kuwa na vimulimuli na ving’ora. Sasa wewe mwenzangu na mimi, mtumishi wa serikali sijui mkuu wa nini, unaweka kimulimuli kwenye Kirikuu yako, IST au hata kama ni hilo benzi lako kwa sheria ipi? Sheria ndio imeshatoka sasa. Hata DC tu hayumo kwenye orodha, wewe je?
Kwa mujibu wa Kanuni ya 7, mtu yeyote haruhusiwi kufunga king’ora, ishara ya sauti, filimbi au kimulimuli kwenye gari isipokuwa tu kama amepata idhini ya Waziri mwenye dhamana itakayotolewa chini ya Kanuni hizi.
Kwa mujibu wa kanuni ya 9, yeyote atakayekiuka au kukaidi Kanuni hizi atakuwa anatenda kosa na adhabu yake ni kati ya shilingi 50,000 na 300,000 au kifungo kisichopungua miezi 6 na kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja.
Kuchapishwa kwa kanuni hizi kwenye Gazeti la serikali, kuna maana kwamba muda wowote kuanzia zilipochapishwa askari sasa wanaweza kusimamisha gari lolote na kukagua iwapo lina King’ora na kama king’ora hicho kimeruhusiwa au wanaweza kusimamisha gari lolote na kujiridhisha iwapo lina ruksa ya kuwa na king’ora au kimulimuli, kama hakuna ruksa hiyo ni adhabu. Ndugu zangu neno “gari” hapa ni pamoja na boda boda na bajaji, kwa hiyo usijitoe ufahamu.
Tii Sheria Bila Shuruti
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
 
Wazee inakuwaje siku hizi unaweza kuwa unapita zako labda Maandazi Road mara ghafla V8 inawasha king'ora ili mumpishe.. yaani imekuwa kero kubwa. Wakazi wa Dar wanakutana na ving'ora vingi kwa siku. Ifikie sehemu mamlaka zinazohusika zidhibiti hii hali.

Kwani idadi ya viongozi au watendaji wa serikali wenye haraka imeongezeka? Kama vipi ving'ora viwekwe kwenye magari yanayokidhi vigezo vya kusheria. Au kama vipi sheria ifanyiwe marekebisho kupunguza idadi ya wanaostahili kupita na kung'ora.
Vingorq wamepewa hadi mashekh mwaipopo wakitaka kujamba wanavipiga.
 
Back
Top Bottom