Wakuu nifanyeje nilijue draft?

Wakuu nifanyeje nilijue draft?

Hicho kipengele cha tatu upo sahihi hayo mengine nayaacha kama yalivyo
Nilijua draft kipindi nina miaka 12 nadhani draft ni kipaji.
Kwanza draft haitakiwi ufikirie sana.
pili kabla hujasukuma kete mtazame usoni mpinzani wako.
Tatu kabla ya zamu yako kucheza usiangalie sana wenzako wanavyo cheza.
nne usicheze na watu wasio na viwango utadumaza kiwango chako.
 
mkuu hesabu za darasani na za draft tofauti kabisa ,Nikiendaga vile vijiwe vya draft nawakutaga jamaa vilaza tu kwenye hesabu alafu sisi tunaojua,log,matrix na ndugu zake kina probability tunafungwa tu binafs naupenda sana huu mchezo mpaka nimedowload game kwenye kitekno bt kila siku nafungwa tu.

Kuna kujua hesabu hlf kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria..

Yeyote anayejua draft sana basi ujue ht km darasani ni kilaza vip,huyo hajui uwezo wake halisi au aliaminishwa yeye ni kilaza ila kimsingi ana uwezo mkubwa tu hata darasani
 
Kujua hesabu hakuna mahusiano yoyote na draft, Drafti ni mchezo wa mitego kuanzia kete ya Kwanza mbaka ya mwisho. Usikariri magazijuto ukafikiri utakua mwamba wa draft.
 
Najipa big up maana huwa naweka level ya 100 kwa Dalmax checkers namkalisha mi binafasi kwa sasa nipo level ya juu sana,
Nilianza kucheza draft nna miaka 10.
dalmax habadiliki, mchezo uliomfunga kama unaukumbuka ukipita miguu ile ile naye anakuja vile vile kama ulivyomfunga mwanzo

njoo street huku ukutane na watu wanaoweka mbungi
 
Kuna ushindi unaitwa Super,mchezo mmoja unapigwa 12.
Wataalam wengi wapo uswahilini.mtu anashinda kijiweni kutwa nzima kwa mwaka ancheza draft.
Na wengi uwa ni madalali,mishen town muda mwingi wanakaa kucheza draft.
 
Kaka mimi nimeshawahi kuiwakilisha Tz kwenye michezo ya jumuia ya Madola kwa mchezo wa draft, usinichukulie poa
haya maneno hutumiwa na beginners
 
Hahahaahahaaa kwanza darasani somo la hesabu ulikuwa unapataje???

Amini nakuambia mabingwa wote wa draft wanajua hesabu hata km hawakwenda shule.Draft ni mchezo wa Akili na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri ndo wanashinda otherwise utakuwa mchezaji wa Copy flani na ikipanguliwa kdg unafungwa vby sana
Kwa kutumia nadharia za draft nahitimisha kwa kusema katika draft wewe ni kilaza. (hujui draft), nadhani hata kwenye Math unaweza kujua kukokotoa tu, ila hujui kuitumia.
 
Unatakiwa ucheze mechi nyingi sana...na ujue michezo yote kwa maana ya kwamba BRITISH na FRENCH ,CHINESE sio saana...kwa mfano ukiwa kanda ya ziwa inayochezwa sana ni FRENCH (Mbele na Nyuma)...ukienda Pwani na Nyanda za juu kusini ni BRITISH (Mbele tu)...na unapocheza draft unacheza madraft mawili (la kwako na la mwenzio) ...
 
😂😅😂😂😃....wewe wakujua drafti wewe,kwa kichwa kipi??

Bhange si ya kila mtu...acha bange mkuu.

Naona unashindana na ulivyoviumba??😂
 
Wasalaam wakuu.

Nimejaribu njia nyingi, kuangalia tutorials,Kucheza online, kudownload checkers, kucheza na watu lakini mara nyingi naishia kula za uso tu.

Hivi hakuna app ya kunifunza strategies step by step?

Kila siku nachekwa kijiweni hadi naona aibu kuomba mechi.
Jifunze golf mkuu!
 
Uhusiano upo tena mkubwa

Kuna watu wana akili sema wameaminishwa ni wajinga hivyo wameishi maisha yao yote wanaamini ni wazito darasani...

Namjua mtu ambaye alikuwa kati ya mwisho darasa la kwanza mpk la 5 halafu la sita na darasa 7 ndo anakuja kuwa kinara mnagombania nafasi za mwanzoni.Ni wasababu wamechelewa kujua uwezo wao


Kuna watu wana uwezo ila wanaamini hawana hao ndo wanakujaga kuwa wazuri kwenye draft wakati darasani ni wabovu.Kama unalijua draft vzr utakubaliana na mimi mwenye uwezo mdg wa kufikiria hawezi kuwa bingwa wa draft...
Mzee naona umekomaa na hiki kipimo cha draft.Narudia tena hakuna uhusiano wowote wa hicho unachosema. Kujua draft ni kipaji tu kama vipaji vingine kama kupiga danana, kuruka sarakasi, kuchekesha nk.
 
Heeee....., Sio kwa mashushu hayo loooh, shushu la Xmas , nimeshushukaje mie Mchina wa Nzovwe?
Halafu nyie wanyakyusa mna-inferior za kishamba sana

Wakati hapo kabwe madanali yanachezwa hadi asubuhi na kombe linawekwa. Mshindi watatu anachukua parachichi
 
Wasalaam wakuu.

Nimejaribu njia nyingi, kuangalia tutorials,Kucheza online, kudownload checkers, kucheza na watu lakini mara nyingi naishia kula za uso tu.

Hivi hakuna app ya kunifunza strategies step by step?

Kila siku nachekwa kijiweni hadi naona aibu kuomba mechi.
Huu nao uzi!!!!???? JF inaelekea wapi!?
 
Back
Top Bottom