Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Ah..jf bhana unaweza umiza kichwa kumshauri mtu kumbe hata akaunti yenyewe hana kalala kwa mama yake mdogo hapo abiola hata pakwenda hana asubuhi hii
Kinachokufanya usiamini kuwa amewekewa hiyo pesa kwenye account ni nini ilhali humjui?
 
Wewe kweli ng'ombe wa masikini.
Ningekuwa Mimi ningetoa hata milioni 100.
Maana sijaiba Hilo sio kosa langu.
Kama account NI yangu hizo hela zimefikaje kwenye account yangu?.
Yaani Hilo ni kosa Lao.wewe halikuhusu
Kwenye account kulikuwa na hela zangu, kwa hiyo nilivyotoa ile 1M ule mzigo wao ulikuwapo intact... nilitoa ili nijue je account bado ipo accessible? je balance yangu ya zamani ipo sawa? je mzigo wao utaonekana kwenye balance yangu mpya? kweli ulionekana wote.
 
Yaani kosa lao wao alafu nipasuke Mimi?.
Daah haya mazali yanawakuta watu sio.
Jamaa walisakwa na mitutu ya bunduki kila kona. Yeye alipewa milioni kadhaa na Serikali Kwa kutojihusisha na kuitoa. Kwa ujumla fedha kama hizo zipo kwenye mfumo ambao ni vigumu kutokukamatwa. Labda walioiweka wawe wamefanya hivyo kwa kujiokoa halafu washindwe namna ya kuzifuatilia tena. Ndiyo maana nikatoa pia maoni kwamba anaweza akajipa muda mrefu wa kukaa kimya kama hakuna kilichotokea. Asiseme na asizitoe. Akizitoa na kuzitumia kuna uwezekano mkubwa zikamtokea puani. Pia itapasuka na atakosa furaha.
 
kweli tumeumbwa tofauti.....mpaka muda huu hujajua cha kufanya.....mangi usivute bange tena....
 
King Kong III huwezi kumtunzia huyu mtu pesa?

Analeta Usanii ndani ya Jumba la Sanaa! Sisi wasanii tunamshangaa tu.

Mtu aliyekuta 300m kwenye account yake asingepata hata muda wa kuja kuandika humu JF angenyofoa mdogo mdogo kwenye ATM mpaka Bank wenye wastukie abnormal transactions ndio wangepiga PIN na yeye angeambulia hata kidogo.
 
Kinachokufanya usiamini kuwa amewekewa hiyo pesa kwenye account ni nini ilhali humjui?

Bushmamy hela ina wenge ,ukikuta hiyo 300m hauwezi kupata hata muda wa kuingia JF achilia mbali kufungua thread ,hao watu humu tunawaita Game Changer ,Spin Doctor ,wanaanzisha mada kututoa kwenye jambo linalojadiliwa.
 
Analeta Usanii ndani ya Jumba la Sanaa! Sisi wasanii tunamshangaa tu.

Mtu aliyekuta 300m kwenye account yake asingepata hata muda wa kuja kuandika humu JF angenyofoa mdogo mdogo kwenye ATM mpaka Bank wenye wastukie abnormal transactions ndio wangepiga PIN na yeye angeambulia hata kidogo.
Mmh. Labda huyu mtu huwa anachezaga na milioni 200 kwa 250 kwenye akaunti yake kwa hiyo kuja kuomba ushauri huku kukosea wap?
 
Kuna ndugu yangu nataka kumtumia muda huu kwa PayPal - yupo nje ya nchi - Sasa naogopa endapo Transaction hii kama inaweza kushtukiwa na BOT ama lah - nina muda mchache sana kuamua hili... then nichimbe!!
King Kong III si unaona kabisa hapa maelezo yake halafu unasema ni uongo jamani
 
Mmh. Labda huyu mtu huwa anachezaga na milioni 200 kwa 250 kwenye akaunti yake kwa hiyo kuja kuomba ushauri huku kukosea wap?

Bushmamy mtu anayecheza na 200m-250m hana muda kabisa wa kuingia JF na kuanza kuleta ngonjera maana ana emails zaidi ya 100 za kufanyiwa kazi,ana vikao karibu 10 per day huo muda atautoa wapi? Matajiri wengi kama yupo addicted na mitandao basi ana ajiri watu wa social media kumsaidia maana yeye hana muda.
 
Hapana. Umekosea bana watu huku wapo na pesa, kuna mmoja huku ana kampuni zake kibao na ni diaspora lakini pia huwa anaperuzi peruzi huku sana tu
 
So hii jf ni ya makapuku kama sisi sio?
 
King Kong III si unaona kabisa hapa maelezo yake halafu unasema ni uongo jamani

Bank wana kitengo cha Risk Management ,wana mifumo ya kisasa ya kumonitor transactions zote ,kwanza mtoa mada anashangaa kukuta mil 300 ina maana acc yake haijazoea kuwa na mipunga kiasi hiko ,kwa system za bank kama account ina cheza na digits chache ikija ingiziwa digits nyingi lazima itawapa alert watu wa Risk Management na kuweza ku act immediately.

Hayo maelezo ni moja ya sanaa za mtoa mada...wewe amini tu jamaa anauza chai tu....kuna watu wana vibaji vya uandishi ,akiandika unaona ukweli mtupu.
 
Hapana. Umekosea bana watu huku wapo na pesa, kuna mmoja huku ana kampuni zake kibao na ni diaspora lakini pia huwa anaperuzi peruzi huku sana tu

Sijakataa wapo watu wana pesa humu JF lakini hauwezi kuwakuta wanauza chai(wanapiga porojo),wewe ebu angalia huyo mtu unayemsema kama utaona kama yupo active kwenye comments au kwenye mijadala.
 
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu:

1. Niripoti bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?

Wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
Nilitegemea kukuta picha ya risiti ya ATM.
Tunapoteza Muda Tu hapa, hakuna rijali yeyote atakayekuta hiyo hela akajakuomba ushauri jinsi ya kuitumia.
 
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu:

1. Niripoti bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?

Wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
Jiuzulu!
 
Kuhamishia nje utashtukiwa na kukamatwa haraka sana,kama unaona ni pesa ya kawaida iache katika akaunti,sikilizia kwa muda.Nasema hivyo kwa sababu pesa hiyo si nyingi ya kukufanya uhame nchi,ukienda huko utaishiwa tu.Isikilizie ukiona kimya ni kwako mzee,huna biashara yoyote?
Hii ndiyo ID ya kina Bakhressa au Mo??
Eti $130,000 ni hela ndogo mil300.

JF jamani 😅 😅 sihami ng'oooo milele

Everyday is Saturday................................😎
 
Back
Top Bottom