Wakuu njiani nzuri ya kutumia ili kuondoa kitambi

Wakuu njiani gani nzuri ya kutumia ili kuondoa kitambi.

Kwa kweli naibika , Tumbo kubwa nakosa Confedence.

Nimekimbiwa hadi na shemeji yenu 😎😎😎.


View attachment 3623637
Njia pekee iliyo ya kweli ni kupunguza misosi, basi. Mtu asikudanganye eti fanya mazoezi. Katika kupunguza misosi, hakikisha huli vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi kama nyama za mafuta, chips, vyakula vingine vya kukaanga. Acha kula ugali au wali mwingi. Acha kunywa soda zenye sukari na bia. Wine kunywa.

Punguza kula kwa wingi na mara kwa mara. Mlo mmoja wa kadiri kwa siku unatosha. Jaza tumbo na mbogamboga zaidi.

Huku ukifanya hayo, nunua unga mwingi wa ubuyu na utumie kijiko 1-2 kila siku kwenye uji, chai au supu. Halafu uje hapa utupe mrejesho baada ya mwezi 1-2..
 
Acha kula kitimoto au nyama ya mafuta mengi, acha kunywa pombe na soda punguza kula vitu vyenye sukari na ngano, acha kunywa supu kula milo miwili kwa siku. Baada ya hapo njoo utoe mrejesho, njia nyingine zitakupa mafaniko kidogo sana
 
1. Punguza ratio ya msosi unaokula.

2. Achana na vyakula vya ngano hasa chapati.

3. Achana junkies kama soda na chips.

4. Kula milo 2 kwa siku, breakfast btn saa 3 hadi saa 5, kisha kula menu nzito btn saa 9 hadi saa 12 jioni. Baada ya hapo usile tena mpaka next breakfast.

5.Fanya shughuli za mikono zinazotoa jasho. Kama hauishi nyumba ya pavings hakikisha usafi wa nyumba unafanya mwenyewe. Kutembea iwe ndo maisha yako.

Ukifanya hayo hapo juu utakuwa umeshapata ufumbuzi wa tatizo kwa 80%. Baada ya miezi 6 utapataajibu chanya.
 
Shukran Mkuu
 
Acha kula kitimoto au nyama ya mafuta mengi, acha kunywa pombe na soda punguza kula vitu vyenye sukari na ngano, acha kunywa supu kula milo miwili kwa siku. Baada ya hapo njoo utoe mrejesho, njia nyingine zitakupa mafaniko kidogo sana
Safi Mkuu nishaanza kufanya ivyo
 
Safi Mkuu nitafanya ivyo
 
kitambi is fat, to remove it, you "burn" it, while you burn it, make sure you don't consume other fat that will make the process pointless. burn more that you consume.
Niombe ufungue inbox
 
Chukua mkopo taasisi za pesa kausha damu halafu weka nyumba rehani au kadi ya gari yako uipendayo kama unayo halafu ponda raha. Kitambi kisipo kwisha umelogwa! 🀣
 
Piga mashine kwa siku mara3 kitaisha chenyewe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…