Wakuu njiani nzuri ya kutumia ili kuondoa kitambi

Wakuu njiani nzuri ya kutumia ili kuondoa kitambi

Njia pekee iliyo ya kweli ni kupunguza misosi, basi. Mtu asikudanganye eti fanya mazoezi. Katika kupunguza misosi, hakikisha huli vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi kama nyama za mafuta, chips, vyakula vingine vya kukaanga. Acha kula ugali au wali mwingi. Acha kunywa soda zenye sukari na bia. Wine kunywa.

Punguza kula kwa wingi na mara kwa mara. Mlo mmoja wa kadiri kwa siku unatosha. Jaza tumbo na mbogamboga zaidi.

Huku ukifanya hayo, nunua unga mwingi wa ubuyu na utumie kijiko 1-2 kila siku kwenye uji, chai au supu. Halafu uje hapa utupe mrejesho baada ya mwezi 1-2..
Tofauti ya wine na bia katika kuongeza au kupunguza unene ipo kwenye nini mtaalamu?
 
ili uondoe kitambi unatakiwa uache kunywa soda energy drinks na beer pia unatakiwa unywe maji mengi sana ukiweza tuu hivo basi kitambi kitapungua
 

Attachments

  • 13801F2D-F1ED-4625-84B0-907FF5645FDF.jpeg
    13801F2D-F1ED-4625-84B0-907FF5645FDF.jpeg
    488.1 KB · Views: 15
Daah! Hivi inakuwaje hadi mtu unafutuka namna hiyo?

Ni kula tu au?

Nawaza tu namna utakavyoteseka na kupata tabu mpaka kupata mwili wenye afadhali.

Pole sana Mkuu. Siku ukipungua usirudie tena kufutuka namna hiyo.
 
Kitambi kukiondoa mazima sio jambo dogo. Inabidi u-sacrifice msosi kwa kiasi kikubwa... usile hovyo halafu fanya mazoezi ya kukimbia angalau mara 3 kwa wiki. Kula mara moja kwa siku chakula chochote ila pia usifakamie sana kama watu wa dini ya mnyaaz wanaofakamia msosi saa 10 alfajiri na kujidanganya kuwa kesho wamefunga.
 
Afadhali umemsaidia hivyo hapo ni mchanganyiko wa nini na nini?
Nimeweka nyama ya ngombe, yeye anaweza weka ya kuku, kabichi nimekata big size, na veggies! Kwahiyo chakula ni hichocho kazi yake kupasha tu mpaka amalize siku 2-3
 
Kumbuka kitu kimoja, huwezi kuondoa kitambi peke yake, ni lazima mwili wote upungue.

Kama upo radhi kwa hivyo basi namna pekee ya haraka ya kuondoa kitambi ni ku control chakula. Mazoezi ni extra tu

1. Acha tungi
2. Acha kula wali, ngano, ugali, tambi na carbohydrates kwa muda
3. Acha matumizi excessive ya sukari. Jibane sana kwenye masukari ya aina zote

Mwili ukishakaa Level unayotaka na kitambi kuondoka utaanza kidogo kidogo mawanga huku unakomaa na mazoezi

Ushauri wa "ACHA" kitu fulani is impractical and unsustainable. Ushauri wa hovyo.
 
Wakuu njiani gani nzuri ya kutumia ili kuondoa kitambi.

Kwa kweli naibika , Tumbo kubwa nakosa Confedence.

Nimekimbiwa hadi na shemeji yenu 😎😎😎.


Mimi nakupa mbinu ambayo ni practical na inaweza kudumu kwa muda mrefu.

Kwanza, usisikilize ushauri wa "acha wanga" au "acha chakula fulani." Mara nyingi huo si ushauri endelevu, na watu wengi huishia kurudi kwenye tabia zao za zamani.

Cha msingi ni kula kwa kiasi, kunywa maji ya kutosha, na kutembea angalau 10k steps everyday. Usikimbie kama lengo lako ni kupunguza mafuta. Walking burns more fat than running. Pia hakikisha unalala vizuri ili mwili upate muda wa kurecover vizuri.

Ukianza kuwa fiti, ongeza mazoezi kama push-ups, pull-ups na bodyweight exercises nyingine.

Haya ni mabadiliko ya maisha (lifestyle changes) ambayo unaweza kufanya mahala popote ulipo, bila kuhitaji gym au vifaa vya gharama.
 
Ushauri wa "ACHA" kitu fulani is impractical and unsustainable. Ushauri wa hovyo.
Oooh sorry blaza, samahani sana. Asiache chochote aendelee kula vyote kabisa! Anywe pombe za kutosha mabia mangurue na vyote
 
Back
Top Bottom