Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Jamani Mimi nataka kujua tu kwa wazoefu ukinunua hisa kama hio je makadilio ya faida inaweza kuwa ngapi msaada tafadhari kwa wazoefu
 
form ni lazima zipatikane NBC tu? maana sehemu zingine hazina huduma za NBC ila NMB.
 
Habari zenu wanajamvi leo naomba nitumie fursa hii kupata ufafanuzi kuhusu hawa jamaa zetu wa voda .kuna tangazo kuwa wanauza hisa kwa wananchi yaani mwananchi anakuwa miongoni mwa wamiliki wa kampuni sasa nataka kujua yafuatayo na ni kwa faida ya wengi ikizingatia sasa hivi maisha ni ya kutumia akiri zaidi ili uweze kupata pesa.

1:kujiunga

kwasababu wana sema bonyeza *150*36 alama ya reli .ila ukifuata formula hii inakuambia hauna pesa ambayo ina kuwezesha kupata huduma hii.yaani haitoi ufafanuzi unatakiwa kuwa na pesa kiasi gani ili uweze kujiunga.

2:Kuna faida gani au hasara ya kununua hisa.
hakuna maelezo ya kutosha kwamba nikitaka kununua hisa napata faida au hasara kwa fomula ipi.

3:muda wa uhai wa hisa na muda wa kupata faida

bado hakuna maelezo kuwa je nikinunua hisa nitapata faida baada ya muda gani

4:kujitoa
kwa forumula mlio iweka ina maana labda kama mtu ana pesa ya kutosha kwenye simu moja kwa moja atakua amejiunga na hii huduma sasa je anawezaje kutoka kama akibadilisha mawzo au ndiyo imekula kwake? au baada ya muda mteja akitaka kujitoa inakuwaje naomba watu wa voda mnijibu maswali haya kwa faida ya watu wengine pia

hitimisho naomba samahani kwa kutoweka bandiko hili kwenye sticky thread yenu hapo juu kwababu siyo watu wote wanatembelea hiyo thread. Asanteni.
 
Watu wako kwa GWIJIMA

hapa hupati comment ata tano bora uanzishe ya GWAJUMA HAPO UTAPATA POINT ZA ZIADA
 
1. Kujiunga
*150*36# ni mfumo uliobuniwa na Maxcom Africa (MaxMalipo) kwa kushirikiana na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwawezesha washiriki kununua na kuuza hisa. Mfumo huu hurahisisha biashara kwa kuwa muuzaji au mnunuzi halazimiki kuwatafuta mawakala wa soko la hisa ambao karibu wote wapo DSM. Ninachojua ni kwamba mfumo huu hauitaji kuwa na salio kwenye simu (credit), labda kama mitandao ina kanuni zake ila kwa tiGO ni bure. Ukifanikiwa kuingia itakubidi kununua hisa 100 na zaidi, na hapo utapata namba ya kumbukumbu ambayo utalipia kwa njia ya M-Pesa, au MaxMalipo. Kama unatumia mfumo huu kwa mara ya kwanza inakubidi ujisajili kwa kufuata maelekezo. Au la, unaweza kuwatembelea madalali walioainishwa na soko, au tawi lolote la beki ya NBC ambayo imeteuliwa na Vodacom.

2. Faida na Hasara za kununua Hisa
Kama umesikia tangazo vizuri, wanasema "biashara ya hisa ina changamoto nyingi, tafadhali wasiliana na mshauri wako wa masuala ya fedha". Na ndivyo ilivyo, unapotaka kununua hisa zozote kuna mambo lazima uyaangalie. Kama una utaalam wa kung'amua ni vizuri, ila kama huna basi yakupasa kutafuta washauri wa masuala ya fedha.

3. Muda wa Uhai wa Hisa

Ukinunua hisa unakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni husika na unaweza kuwa nazo maisha yako yote. Malipo ya hisa yanajulikana kama gawio. Masuala kama hayo yanaainishwa kabla ya kuanza kuuzwa kwa hisa. Tafadhali soma waraka wa matarajio uliotolewa na Vodacom na kuthibitishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji, CMSA, kupata taarifa zaidi.

4. Kujitoa
'Kujitoa' ni hiyari yako. Yaani unaamua kuuza hisa zako kama hutaki tena kuendelea kuwa mmiliki. Unapotaka kuuza hisa unaweza kutumia njia ya simu au kuwasiliana na madalali waliosajiliwa na DSE ka ajili ya taratibu husika.
 
sasa je mwananchi wa kawaida anayajua hayo.
 
Watu wako kwa GWIJIMA

hapa hupati comment ata tano bora uanzishe ya GWAJUMA HAPO UTAPATA POINT ZA ZIADA
lakini mwisho wa siku mtu hapati hata shilingi moja kwa ufatiliaji huo.
 
Hapo hapo kuna wenzio walikua mamilionea kupitia hiyo hiyo Crdb trust me... Kweny hisa inabid uwe sharp and information is a very powerful tool..Kama ambavyo watu watapiga hela kweny Voda wengine wakibaki wanatoa macho..but I would tell you..bado hujapoteza kitu kweny crdb..kitu cha msingi kampuni iwe ina make consistent profit afu iwe inatoa gawio..bei itakuja panda tu no need to worry.. Kilichotokea Crdb walifanya Rights issue in 2015..hii huchangia kupunguza bei kwasab idadi ya issued shares iliongezeka sokoni..kingine Crdb Ina wanahisa wadogowadogo wengi ambao hupenda kuuza hisa Mara kwa Mara as compared to big investors who buy and hold..hii hupeleka demand kushuka hence Price.. Kingine ni current liquidity problem tangia jpm ashike hatamu..watu hawana loose money as in the past
Asante mkuu kwa muongozo wako sijaziuza bado nasubiri mpaka bei itakapo kaa sawa
 
Kuhusu faidia ya kampuni kwa mtu wakawaida atawezatambuaje kama hapa kuna faida au hasara maana, naona hapa kwentu kama uwazi au uthibiti bado ni wamashaka.
Kama makampuni ya uchimbaji madini wengi wanalalama kupata hasara...je sisi tutathibitisha vipi kama ugunjwa huyo pia ukihamia huku kwa hizi kampuni mfano Voda.
 
kuna mahali nilisikia kwamba kama kampuni inapata hasara ,wanaokua wa kwanza kupata hasara au hata kupoteza hisa zao ni wale wenye hisa ndogo katika kampuni husika.naomba kufafanuliwa hapa
Ninachifahamu kidogo kuhusu hisa ni kwamba Mwenye asilimia kubwa ya hisa ndio Mwenye nguvu na maamuzi.
Mfano vodacom wanauza 25% tu ya hizo zao hivyo kuna 75% inamilikuwa na wengine so hapo hata kama ninyi ambalo mmenunua hisa ndani ya 25% niwamiliki sawa wa Voda Ila kwenye swala la maamuzi ya kampuni Hamna nguvu hata kama ni wengi kushinda wamiliki kwenye 75% ya hisa.
Nikimaanisha kama 75% ya hisa za Voda anamiliki Rostam pekee basi anaweza Fanya maamuzi ya kuthiri ninyi nyooote kwenye umiliki/hisa 25%.

Elimu zaidi yahitajika kuhusu hisa kwa tuliowengi.
 
Kuna mtu aliniambia hisa wananunua wazee wenyewe hela benk et kwa kijana mdogo ni bora uzungushe hizo senti zako cuz return ya share ni ndogo sana
Salaam, huyo alikudanganya kama hadi leo huja nunua jitahidi ununue. Ni biashara nzuri mimi ndio biashara ninayo fanya. Ukihitaji Fomu naweza kukutumia ukijaza una scan kitambulisho tunatuma kwa wakala wa Serikali TIB INVESTIMENT kisha una weka fedha Benki inayogawanyika kwa 850 (nyingi kwa kadri unavyo weza ) kisha mwezi wa tano tarehe 16 zinaingia sokoni. Hutajuta
 
CDS kwa kirefu ni nini?
Ni account ya nini?
Naifungua wapi, kwa garama ya sh ngapi?
Broker pia nampata wapi
Sorry kwa maswali mengi
CDS ni akaunti ambayo kwa kirefu ni "Central Depository System"
Ni akaunti ya Usajili ili utambulike kama Mnunuzi
Unaifungua kwenye mtandao na hakuna gharama kuifungua
Breaker wapo zaidi ya kumi wengi wapo. Mtaa wa Samora Dar Es Salaam ila yupo wa Serikali anaitwa TIB Investiment kampuni dada ya TIB Bank. Ukihitaji Fomu naweza kukutumia.
 
sasa je mwananchi wa kawaida anayajua hayo.
hata mie ni mwananchi wa kawaida tu. jambo la muhimu ni kuwa mfuatiliaji wa mambo. mtu hataweza kujua haya mambo kwa kuoteshwa. hata na hivyo ni mambo yenye changamoto nyingi!
 
Lazima ufungue CDS akaunti kabla hujaanza kununua hisa. Waombaji ambao hawajawa na akaunti ya hisa (CDS wengine wanaita CSD) watatakiwa kujisajili ili kupata akaunti waweze kununua hisa. Usajili huo unaweza kufanyika kupitia orodha (menu) ya M-Pesa au Maximalipo.
Mpesa inasumbua sana sijajua tatizo ni nini?
 
Nikitakiwa kununua hisa ni mpaka nijisajali na bank???nahitaji kujuzwa zaidi
 
Jamani Mimi nataka kujua tu kwa wazoefu ukinunua hisa kama hio je makadilio ya faida inaweza kuwa ngapi msaada tafadhari kwa wazoefu
Wamesema wanategemea 100% nfsn ya mwaka inamaana ela yako ina double
 
Back
Top Bottom