comesucces
Senior Member
- Feb 21, 2017
- 160
- 105
Jamani Mimi nataka kujua tu kwa wazoefu ukinunua hisa kama hio je makadilio ya faida inaweza kuwa ngapi msaada tafadhari kwa wazoefu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa je mwananchi wa kawaida anayajua hayo.1. Kujiunga
*150*36# ni mfumo uliobuniwa na Maxcom Africa (MaxMalipo) kwa kushirikiana na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwawezesha washiriki kununua na kuuza hisa. Mfumo huu hurahisisha biashara kwa kuwa muuzaji au mnunuzi halazimiki kuwatafuta mawakala wa soko la hisa ambao karibu wote wapo DSM. Ninachojua ni kwamba mfumo huu hauitaji kuwa na salio kwenye simu (credit), labda kama mitandao ina kanuni zake ila kwa tiGO ni bure. Ukifanikiwa kuingia itakubidi kununua hisa 100 na zaidi, na hapo utapata namba ya kumbukumbu ambayo utalipia kwa njia ya M-Pesa, au MaxMalipo. Kama unatumia mfumo huu kwa mara ya kwanza inakubidi ujisajili kwa kufuata maelekezo. Au la, unaweza kuwatembelea madalali walioainishwa na soko, au tawi lolote la beki ya NBC ambayo imeteuliwa na Vodacom.
2. Faida na Hasara za kununua Hisa
Kama umesikia tangazo vizuri, wanasema "biashara ya hisa ina changamoto nyingi, tafadhali wasiliana na mshauri wako wa masuala ya fedha". Na ndivyo ilivyo, unapotaka kununua hisa zozote kuna mambo lazima uyaangalie. Kama una utaalam wa kung'amua ni vizuri, ila kama huna basi yakupasa kutafuta washauri wa masuala ya fedha.
3. Muda wa Uhai wa Hisa
Ukinunua hisa unakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni husika na unaweza kuwa nazo maisha yako yote. Malipo ya hisa yanajulikana kama gawio. Masuala kama hayo yanaainishwa kabla ya kuanza kuuzwa kwa hisa. Tafadhali soma waraka wa matarajio uliotolewa na Vodacom na kuthibitishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji, CMSA, kupata taarifa zaidi.
4. Kujitoa
'Kujitoa' ni hiyari yako. Yaani unaamua kuuza hisa zako kama hutaki tena kuendelea kuwa mmiliki. Unapotaka kuuza hisa unaweza kutumia njia ya simu au kuwasiliana na madalali waliosajiliwa na DSE ka ajili ya taratibu husika.
lakini mwisho wa siku mtu hapati hata shilingi moja kwa ufatiliaji huo.Watu wako kwa GWIJIMA
hapa hupati comment ata tano bora uanzishe ya GWAJUMA HAPO UTAPATA POINT ZA ZIADA
Asante mkuu kwa muongozo wako sijaziuza bado nasubiri mpaka bei itakapo kaa sawaHapo hapo kuna wenzio walikua mamilionea kupitia hiyo hiyo Crdb trust me... Kweny hisa inabid uwe sharp and information is a very powerful tool..Kama ambavyo watu watapiga hela kweny Voda wengine wakibaki wanatoa macho..but I would tell you..bado hujapoteza kitu kweny crdb..kitu cha msingi kampuni iwe ina make consistent profit afu iwe inatoa gawio..bei itakuja panda tu no need to worry.. Kilichotokea Crdb walifanya Rights issue in 2015..hii huchangia kupunguza bei kwasab idadi ya issued shares iliongezeka sokoni..kingine Crdb Ina wanahisa wadogowadogo wengi ambao hupenda kuuza hisa Mara kwa Mara as compared to big investors who buy and hold..hii hupeleka demand kushuka hence Price.. Kingine ni current liquidity problem tangia jpm ashike hatamu..watu hawana loose money as in the past
Ninachifahamu kidogo kuhusu hisa ni kwamba Mwenye asilimia kubwa ya hisa ndio Mwenye nguvu na maamuzi.kuna mahali nilisikia kwamba kama kampuni inapata hasara ,wanaokua wa kwanza kupata hasara au hata kupoteza hisa zao ni wale wenye hisa ndogo katika kampuni husika.naomba kufafanuliwa hapa
Salaam, huyo alikudanganya kama hadi leo huja nunua jitahidi ununue. Ni biashara nzuri mimi ndio biashara ninayo fanya. Ukihitaji Fomu naweza kukutumia ukijaza una scan kitambulisho tunatuma kwa wakala wa Serikali TIB INVESTIMENT kisha una weka fedha Benki inayogawanyika kwa 850 (nyingi kwa kadri unavyo weza ) kisha mwezi wa tano tarehe 16 zinaingia sokoni. HutajutaKuna mtu aliniambia hisa wananunua wazee wenyewe hela benk et kwa kijana mdogo ni bora uzungushe hizo senti zako cuz return ya share ni ndogo sana
CDS ni akaunti ambayo kwa kirefu ni "Central Depository System"CDS kwa kirefu ni nini?
Ni account ya nini?
Naifungua wapi, kwa garama ya sh ngapi?
Broker pia nampata wapi
Sorry kwa maswali mengi
hata mie ni mwananchi wa kawaida tu. jambo la muhimu ni kuwa mfuatiliaji wa mambo. mtu hataweza kujua haya mambo kwa kuoteshwa. hata na hivyo ni mambo yenye changamoto nyingi!sasa je mwananchi wa kawaida anayajua hayo.
Mpesa inasumbua sana sijajua tatizo ni nini?Lazima ufungue CDS akaunti kabla hujaanza kununua hisa. Waombaji ambao hawajawa na akaunti ya hisa (CDS wengine wanaita CSD) watatakiwa kujisajili ili kupata akaunti waweze kununua hisa. Usajili huo unaweza kufanyika kupitia orodha (menu) ya M-Pesa au Maximalipo.
Inakwambia vipi mkuu. PoleMpesa inasumbua sana sijajua tatizo ni nini?
Inakata katikatiInakwambia vipi mkuu. Pole
Wamesema wanategemea 100% nfsn ya mwaka inamaana ela yako ina doubleJamani Mimi nataka kujua tu kwa wazoefu ukinunua hisa kama hio je makadilio ya faida inaweza kuwa ngapi msaada tafadhari kwa wazoefu