Wakuu tulipe madeni ya mikopo, ukizembea utaumia zaidi...

Wakuu tulipe madeni ya mikopo, ukizembea utaumia zaidi...

koba lee

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Posts
981
Reaction score
1,606
Hbari za muda huu wakuu,

Niende kwenye mada, kuna office moja ya kukopesha nilichukua hela kiasi cha Tsh. laki 2 kwa mwezi mmoja na ikatakiwa nilipe laki mbili na sitini,kama ikishindikana niwe natoa riba. Sasa bana nimeenda nao vizuri na ilikuwa mwaka jana mwanzoni, nimewalipa vizuri tu riba zao, sasa kafika mahali mambo yakawa magumu riba haionekani wakipiga simu wanakula sound,wakipiga tena sipatikani.

Kumbe walikuwa wananilia timing imepita miezi minne sijafanya rejesho lolote na mimi nikawa najipa moyo kua labda wamepotezea maana laki mbili kitu gani.

Leo sasa niko kazini mara simu ya mezani inaita nikapokea upande wa pili anaongea HR akanambia "come to my office as soon as possible"., chale zikanicheza nikasema potelea pote naenda maana hapakuwa na jingine la kufanya, kufka mule ofisini namkuta mshkaji mmoja na binti wa kike, nikajua ndo walewale nikajisemea kumekucha

Yakaanza maneno mengi pale mi mdogo kama sh mia hapo, nashukuru HR kidogo alikuwa upande wangu lakini mwisho wa siku inabidi niwalipe hela yote ndani ya miezi miwili ambayo malimbikizo yake ni kama mara tatu ya hela niliyochukua,haya mambo haya.Sasa hapa nawaza naanzia wapi maana hata salary yenyewe ina viraka kila mahali.

Inawezekana mliokuja leo ofisini mpo humu na mnausoma huu uzi, hela yenu nitawalipa.

Wakuu tulipe madeni ikiwezekana tukishalipa tuachane na haya mambo ya mikopo japo upande mwingine ni ngumu maana vyuma vikiumana unaanza kuhaha kila microfinance kupata mkopo.

Ni hayo tu wakuu.
 
Mimi mtaani Sina madeni mengi labda 30000 iv ...ila mm nazowadai raia Ni Zaid ya laki moja...siku zinavyoenda nazidi kuwasamehe,,sitaki stress
 
Unaogopaje deni mtoto wa kiume....
mimi jamaa wananidai mia moja na kumi na tatu milioni.
na sijalipa....
Big up kamanda,kingine mi siogopi ila kusumbuliwa ndo sitaki,maana mda mwingine mpaka usingizi unakata
 
Back
Top Bottom