Unayosema yawezekana ni kweli lakini aliyewateua ndio kasema mrudushe, na tatizo la hawa wateule sijui kama wewe ni miongoni mwao kama sio samahani, huwa ni waoga kusema ukweli au kumwambia mkuu kuwa hivyo sivyo, sasa haisaidii kulalama mitandaoni, mmetumia au lah, kasma imepitishwa na bunge au lah mkubwa kasema rudisheni, La sivyo msirudishe atengue uteuzi iwe aibu kwenu au mrudishe na mjiuzulu ili mkuu atambue kuwa mmechukia na mtaonekana mashujaa. Kwani matumizi yakigeuzwa kutoka posho kwenda maendeleo kuna kosa gani almradi ijulikane imeenda kufanya shughuli gani ya maendeleo.
Poleni kama mlifikiri mlipoteuliwa mnaenda kutunisha matumbo mtaambulia magonjwa ya moyo na stress kibao kwa kutojua kesho kutaamkaje.