Tetesi: Wakuu wa mikoa, wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa serikali wahoji kurudisha posho za Mwenge

Tetesi: Wakuu wa mikoa, wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa serikali wahoji kurudisha posho za Mwenge

Mimi nakubali 100% nia ya Rais, kinachoshindwa kuelewa na labda wengine watanisaidia na hilo, ni kwasababu gani agizo la kutodhuria sherehe ya mwenge limetangazwa baada ya watu kujipanga na kupokea posho? Kupanga si dalili ya utawala bora? Je kwa stahili hii kweli tutaweza?
 
Bandiko lina nembo ya TETESI, na tetesi haina tofauti kubwa na neno UDAKU,hakuna sababu ya kuendekeza udaku jukwaani kwani unashusha hadhi ya jukwaa,ila kama ni kweli wanalalamika na wako serious ni vyema wangedocument malalamiko yako kwenye right platform kwani kwa kanuni za kiofisi "if not documented then it is not done".
 
Unayosema yawezekana ni kweli lakini aliyewateua ndio kasema mrudushe, na tatizo la hawa wateule sijui kama wewe ni miongoni mwao kama sio samahani, huwa ni waoga kusema ukweli au kumwambia mkuu kuwa hivyo sivyo, sasa haisaidii kulalama mitandaoni, mmetumia au lah, kasma imepitishwa na bunge au lah mkubwa kasema rudisheni, La sivyo msirudishe atengue uteuzi iwe aibu kwenu au mrudishe na mjiuzulu ili mkuu atambue kuwa mmechukia na mtaonekana mashujaa. Kwani matumizi yakigeuzwa kutoka posho kwenda maendeleo kuna kosa gani almradi ijulikane imeenda kufanya shughuli gani ya maendeleo.
Poleni kama mlifikiri mlipoteuliwa mnaenda kutunisha matumbo mtaambulia magonjwa ya moyo na stress kibao kwa kutojua kesho kutaamkaje.
Wanajuuuuuuuta.....
 
hapo ndipo mtaamini kwamba kuna chama cha ndiooooooo!!!!!!!!!!!!!!!! ili mradi aliyesema ni mkubwa wao hata likiwa ni jambo la kuuzunisha
 
Wanajuuuuuuuta.....
Haswa ukute wameacha kazi zao(ajira)nzuri kwa kukimbilia uteuzi kwa kudhani wameula kuwa kujipatia posho ndefu na virushwa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Nani, lini, wapi, na chanzo cha hbari (source) ni maswali muhimu unapoleta taarifa, vinginevyo taarifa yako inakuwa udaku.

Tena huyu mleta mada ni mtu hatari sana, anataka kuwachonganisha watu hawa na mkuu!
 
Kufatana na agizo la mheshimiwa rais la kurudisha pesa za posho walizolipwa wakurungezi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wa serikali wamehoji kwanini warudishe pesa hizo wakati wametumia kwenye maandalizi mbalimbali.

Hii imetokea leo kuanza kulalamika wakuu hao na kusema wao hawapaswi kulaumiwa maana walipokea maagizo na pesa hizo juu walidai kuwa tayari watumishi hao walikuwa wameanza safari na wengine kufanya maandalizi ya kwenda kuhudhuria mwaliko huo watendaji hao wameonyesha kutolidhishwa na hali hii ya utendaji ambayo ipo sasa.

Chanzo: Viongozi waliofika eneo la tukio na wale walioko ofisini kulalamika mbele za watumishi wenzake.
wewe utakuwa wa ujabu sana
 
Mwenge una ratiba na inajulikana ilitakiwa hawa viongozi waambiwe mapema kabla hata ya maandalizi.kuna wengine walikua simiyu tayari na pesa ilishatumika kwa maandalizi.Hasara imeshapatikana tayari japo raisi hajafanya vibaya kwa maamuzi yake ila yamechelewa.
 
Back
Top Bottom