Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Juzi hapa kulifanyika tamasha la Landrover. Mkuu wa mkoa wa Arusha akapigia debe kwelikweli jambo hilo. Akatumia resources za ofisi ya umma ikiwemo wakati kupigia promo jambo hilo. Lakini hayo yakifanyika, bila shaka anatambua wazi kuwa anapigia debe kampuni ya magari ya Landrover. Hasa ukizingatia huo ni mkoa wenye vyanzo vingi vya utalii na magari hayo huingia mbugani kupeleka watalii, basi ameitangazia biashara kampuni hiyo kwa kiwango kikubwa. Sijui kama kalipwa lakini vitu rahisirahisi kama hivyo siyo kazi ya mkuu wa mkoa.
The same imetokea hapa Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam naye anautangazia umma kuwa kutakuwa na Tamasha kubwa la kula na kunywa lilioandaliwa na kampuni ya pombe ya HEINEKEN. Yaani matangzao ambayo zamani yangefanywa na redio zetu, ama watu binafsi leo ofisi ya mkuu wa mkoa ndiyo inaenda kutangazia kampuni ya pombe tamasha lao. Sasa Sijui kazi waliotumwa hawa wakuu wa mikoa ni kugeuka na kuwa madalali wa makampuni makubwa au kufanya shughuli kwa miongozo ya taratibu za kazi zao.
Zamani enzi za mwalimu wakuu wa wilaya na mikoa walikuwa wanashindana kubuni vitu kama uanzishwaji wa kilimo fulani katika maeneo yao ili kukabiliana na njaa, kuhimiza elimu ya watu wazima na watoto, kusaidia kuzunguuka na kuangalia wapi kuna matatizo kama maji na kusaidiana na wananchi kuchimba visima, kujenga madaraja etc. Ila wakuu wa mikoa wa Rais Samia wao wanatangaza bash, landrover festivals na mambo mengine madogomadogo yasiyo na tija pana kwenye equation nzima ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi.
Labda huenda kwa sababu bosi wao juzi wakati akihojiwa kasema Tanzania siyo masikini (kwa kuwa hata watu tunaodhani ni masikini kama vile Wahadzabe wana matunda mengi kama 30 hivi ya kula na nyama tele wakati ulaya hayo ni ghali, basi hiyo ni proof kuwa sisis siyo masikni!!!) , basi huenda wateule wake nao wananadhani kuwa kwa kuwa Tanzania siyo masikini basi kazi yao kubwa siyo kuchagiza jitihada za kupambana na umasikini. Wao changamoto yao ni namna kali zaidi ya kula bata, kuenjoy, kustarehe!. Hiyo ndiyo kazi kubwa wanaoyadhani wanayo!.