Wakuu wa Mikoa wanapogeuka madalali wa kutangaza biashara za makampuni

Mkuu ni kama nakuelewa; basi tusaidie kwa takwimu, Ajira za Moja kwa Moja za kudumu na za muda mfupi ambazo tukizipeleka NBS Wizara husika inaweza kuliambia bunge kwamba kazi Ile imechagia kuleta Ajira nvhini na kwahiyo viongzi kama hao tuwatambue kama ni wanunifu na njia ya matamasha iigwe hata na serikali kuu katika kupanua wigo wa Ajira! Na kutatua changamoto kubwa ya Ajira inayotukbali kama taifa! Ahsante
 
Balozi wa Tz uingereza aandaa tamasha, Serengeti Festival, jijini London kwa ajili ya kutangaza utalii na fursa nyingine za uwekezaji Tz vs RC wa Arusha aandaa Landrover Festival kwa ajili ya… Africans are bearly out of the bush
 
Mtoa mada jifunze kitu kwenye ishu za promotion, ili kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri wewe umetengeneza hisia zaidi badala ya uelewa
 
If it works it's not stupid.

Mapato yaliongezeka siku hiyo na miezi ya nyuma yake wauzaji wa spare parts na mafundi walipata kazi nyingi kwahiyo ilikua ni fursa
 
Hahaha hawa wtu hawana kazi kabisa, yani Ukuu wa mkoa hata mtoto aliyemaliza darasa la saba ana umudu. Angalia wanavyoteuliwa, hakuna special skill au knowledge au ability inayohitajika. Unakuata mkuu wa wilaya ana PHD, Mkuu wa mkoa ana Degree moja. Majukumu yao hayaeleweki ni yapi hivyo wanajikuta wanayatafuta kila kukicha, yani ukienda na kesi ya ardhi, yake, ukienda na tamasha la wauza mboga lake, daladala wakilalamika lake, sijui walimu wakilala mika yeye.

Kwa kifupi, Hawana kazi ni kama Antena wao hunasa kila kinachopita mbele yao bila kujali ni majukumu yao au la, utasikia mimi ndiye mkuu wa mkoa.

Mi ningetamani tungekuwa tunachapishiwa kwenye gazeti la serikali, majukumu ya hawa wanaoteuliwa na Rais ili tuwe tuna wapima kwa wanayotakiwa kuyafanya, kuliko hivi sasa ilivyo holela holela.
 
Kamaliza Land Rover Festival aje na Land Cruiser Festival tuuze magari kirahisi kwa wahitaji...
 
Hauna Exposure una mawazo mgando.

Kama exposure inahusu petty issues basi ni exposure feki. Wakuu wa mikoa wanatakiwa kuwa front kwenye mambo makubwa siyo kuwa agents wa biashara za watu. Unaumiza biashara za walipa kodi wengine kwa kuwa promoter wa washindani wao wengi.

Hayo mambo ya festivals wawaachie watu binafsi kama redios na makampuni ya starehe yafanye promo. Mbona kuna Fiesta za Clouds FM toka zamani na walikuwa wakifanya promo wenyewe?
 
Rushwa haitakuja kuisha
 
Mambo makubwa Tanzania ni yepi kama sio hayo yanayohusu watu moja kwa moja hizo redio hawakukatazwa kugundua wakifikiri wafanye huyu jamaa mimi simkubali ila kwenye hili nipo nae moja kwa moja Nchi masikini pamoja na watu wake mtu anakuja na vitu vya kujikwamua mnapinga mnataka nini sasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…