Pre GE2025 Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka

Pre GE2025 Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanamlipa fadhila sababu sasa amewaachia wafanye watakavyo.

Hizo shule za sekondari zimekuwa pango la wanyonyaji.
Sasa wakuu wa shule wamebuni miradi yao ya kukamua wazazi michango kibao mara ya mitihani jumamosi, mara michango wa chakula, mara nini.....

Sasa hivi waalimu hawafundishi wanapiga miradi yao binafsi, shuleni Wana ripoti na kuendeleza na mambo yao.
Hutaki kumchangia mwanao Chakula shuleni?
 
Tatizo lipo kwa uongozi wa TAHOSSA sidhani kama walimu wakuu wote wameridhia.Hawa walimu wakuu wa shule zote za msingi na sekondari za Serikali na Private . Uongozi wa TAHOSSA unajua gharama ya fomu ya urais itauzwa bei gani au wanataka Maokoto yatakayobaki wajinufaishe
Naamini tatizo limeanzia kwa Boss wao Mchengerwa, huyu ndo engineer wa huu mpango. Hata sijui kwanini imani yangu inanituma hivi[emoji3]
 
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.

Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?

Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?

Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?

Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?

Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu? View attachment 2847719

Hao nao wajinga. Wako 3000 halafu wanataka kuleta kapu kwa raia ili iweje?. Si wajichange hao watatu.
 
Wewe hujuhi kuwa Tanzania walimu ni wale waliofeli fomu 4 au fomu six??unakuta 4 ya 35 ndo walimu au fomu six 4 ya 20 ndo walimu wetu.
 
Back
Top Bottom