Wakuu wa vita kuua watu kuanzia 300

Wakuu wa vita kuua watu kuanzia 300

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,352
Miongoni mwa wafalme waliokuwa na nguvu sana kipindi hicho alikuwa mfalme Daudi. Nguvu kubwa na alikuwa mzee wa totozi sana lakini pamoja na hayo mungu alimpenda sana, kwa sababu gani? Ni kwa sababu alikuwa mnyenyekevu mbele zake.

Ndiyo! Mungu hupenda watu wa aina hii, yaani unapokosea, ulijue kosa lako, uende mbele zake na kumuomba msamaha, sio unajifanya much know kwa sana.

Sasa pale Israel kipindi hicho akiwa mfalme, alikuwa anapambana vita vingi na kushinda, wakati mwingine najaribu kumfananisha na Alexander The Great kwa namna alivyokuwa mkali wa vita.

Sasa wakati Daudi ameanza utawala wake hapo Israel, akakusanya wanajeshi wa vita, ambao watapambana kwa ajili yake na taifa, na jeshi lake hilo lilikuwa na viongozi watatu, mmojawapo alikuwa Adino.

Huyu alikuja kuwa mkuu wa majeshi kutokana na uwezo wake mkubwa. Kwenye vita moja, jamaa aliua maadui 800 peke yake, hapo unaweza kuona jamaa alikuwa na nguvu kiasi gani.

Ukiachana na huyo pia kulikuwa na mwingine aliyeitwa Abishai. Huyu jamaa yeye aliwahi kuua watu 300 kwenye vita moja.

Na wa tatu aliitwa Eleazer. Huyu jamaa naye alikuwa mkali sana vitani. Kuna kipindi alikuwa akipigana vita kwa kutumia panga lake mpaka mkono ukawa unakataa kutoka kwenye panga.

Kwa nini?

Inawezekana alilishikilia panga sana kiasi cha kushindwa kutoka mikononi mwake ama damu zilisababisha kuufanya mkono wake ushikilie vilivyo kutokana na kuwa tayari imekuwa kama gundi kwenye panga lile. Hii inaitwa Cougulation.

Hawa majamaa walikuwa loyal sana kwa mfalme wao, walikuwa tayari kufanya lolote lile ilimradi mfalme apate alichokuwa anakihitaji.

Kuna kipindi Daudi alihitaji maji kutoka kwenye kisima huko Bethlehem, akawatuma wapiganaji hawa kwenda huko kwani mji ulikuwa umezingirwa na maadui.

Majamaa wakaenda, wakaingia, wakachoka maji na kumpelekea mfalme.

Daudi alishinda vita vingi kwa sababu alikuwa na watu hatari, waliompigania kupita kawaida. Kama alikusanya watu wenye uwezo wa kuua watu kuanzia 300 kwenda juu, unadhani kuna vita gani ungempiga huyu mwamba?
 

Attachments

  • FB_IMG_1723149876494.jpg
    FB_IMG_1723149876494.jpg
    36.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom