Biashara na wazawa pia wanufaike siyo wageni tu. Mnakuwa na vilabu viwili au vitatu ambavyo first 11 ni karibu wageni watupu au wageni watupu. Timu zilizobaki kwenye ligi ambazo uwezo wake wa kusajili wachezaji wageni ni mdogo sana hivyo ubingwa miaka yote ni timu hizo hizo tatu. Tukija kuchagua timu ya Taifa ni midebwedo mwanzo mwisho. Algeria wana timu nzuri sana ya Taifa ambayo wamewahi kushiriki World Cup.
Kwa huu upuuzi wa kuruhusu foreign players wengi itafika wakati kutakuwa hakuna Mtanzania atayekuwa na kiwango cha kuchezea timu ya Taifa kwani wengi ama wanaishia bench hivyo kutoongeza viwango vyao au hawasajiliwi.
Michezo inatakiwa itiliwe mkazo mkubwa sana mashuleni ambako miaka ya nyuma shule nyingi za ziliweza kutoa wachezaji wenye viwango vikubwa tu.
Tukiendekeza huu upuuzi wa kuongeza idadi ya wageni soka Tanzania itaanguka kabisa. Kama biashara hata China soka ni biashara kubwa sana kuliko hata Tanzania lakini bado wameweka idadi ndogo ya wageni ili kukuza viwango vya wachezaji wazawa.
Hapo umekuja sasa mkuu tufungue mjadala,,
Kwanza uelewe mkishahama kutoka armature mnataka kuelekea proffesional na mnauangalia mpira in a bussness aspect hakuna kuoneana huruma.
Watu wanaweka pesa zao nyingi wanatarajia kupata faida kubwa as well,,
Sasa kama wewe hujutumi tukubebe t kwa sbbu ni mtanzania hakuna icho kitu mkuu,,..
Ligi yetu sasa ishakua biashara kubwa hakuna muda tena wakumsubiri na kum bembeleza ibrahim ajibu ajitambue,waziri afunge magoli..
Mifumo mizuri ya soka tupate vipaji maridhawa vya kulisaidia taifa hizo ni.kazi za tff za kimkakati.
Ligi ile ni biashara na vilabu vyetu alhamdulillah vkmefunguka vinaingia sasa kwenye biashara ya mpira ambayo haina mipaka.
Ndo maana unaona leo al_ahly wanamtaka miquissone kwa b2,
Hii hela inaingia simba,kama huna bidhaa bora hujawekeza pesa kupata vipaji maridhawa kama hivo unaingizaje pesa kama hiyo.
Cha msingi tujitazame sie tumekosea wapi,,
Kumzuia chama asicheze si kumfanya ajibu awe chama.