Wale ambao kwenu mpo zaidi ya watoto 6 baba na mama moja, maisha ya ukubwani yapo vipi kindugu ?

Wale ambao kwenu mpo zaidi ya watoto 6 baba na mama moja, maisha ya ukubwani yapo vipi kindugu ?

Sisi kwetu watoto tupo 10 baba na mama mmoja.
Ila kuna wengne tumeshea baba wamama tofaut nao wapo 8 na mama wanne(hapo mzee alibalance kila mama alimpa watoto wawili ili wasiwe wapweke.)
Sie 10 wa baba na mama mmoja tunamshkamano, ila wale wa nje kunabaadh hatupatan kutokana na mama zao na wengne tunapatana hata kwao tunaenda na kujihis tupo kwa mama kabxa
 
Wa Baba mmoja na Mama mmoja wa undugu sana tatizo linakuja pale wanapooa na kuolewa kuna kuwa na kamtikisiko kiasi hasa kwenye malezi ya watoto wao ndipo panapoibuka vita vya mabinamu na matabaka
haswa pale muolewaj au muoaji nae anakuja na tabia zake na kuua umoja
 
Mimi nawashangaa wale wanaozaa watoto 2 au 3 siku hizi!

Huo uzungu tulikuwa bado hatujaufikia!
Tatizo afya ya mama wazazi siku hizi duni.
Wanawake wengi kama wanaume wa siku hizi hawana afya njema. Mwanamke akifikisha watoto watatu au wanne uzazi unakuwa wa hatari na shida sana.
Nadhani mfumo wa maisha hasa upande wa lishe ndiyo chanzo cha tatizo.
Ukiachana na lishe suala la kufanya mazoezi au kazi za nguvu muhimu. Mama zetu walifanya mazoezi kupitia kazi ngumu.
 
Matabaka huwa yapo, wenye kipato kuwa ndio watoa mawazo.....wale wenzangu na mimi huwa wanapewa maelekezo tu nini cha kufanya.....wanasadiana kwenye matatizo yakitokea.....naona wanapendana pia
 
Ndugu wa damu huwa tunazinguana tu ila ule uadui wenyewe kabisa hakuna. Hata kama tumezinguana mmoja akipata tatizo tunasaidiana kwanza. Damu nzito wakuu. Kusema kuwa mtu baki atakuwa na uchungu kuliko ndugu yako wa damu ni kujifariji upumbavu. Kama mna mifarakano kaeni chini mtatue. Sisi tuko 6 kwa mama mmoja ila ninawajua wengine watatu kwa mama tofauti... imagine nina mdogo wangu niliyemzidi miaka 35... wazee wa kiafrika wazinguzi sana
 
Duuhh 🤣
Unamaanisha baba mmoja mama mmoja? Sisi tuko 13.

Ukiweka baba mmoja na mama tofauti na Baba tofauti tuko 22 .

Sijui wewe umekulia wapi.
Ila sisi tuko vizuri tu tunasongabele.
 
Watoto wa baba moja mama tofauti huwa na uadui na sababu kubwa huwa ni pale baba anapoonyesha upendeleo kwa mke flani na watoto wake.

Chuki au Upendo hua zinajengwa na hao wanawake, So itategemea wataamua ku co exist vipi
 
Ndugu wa damu huwa tunazinguana tu ila ule uadui wenyewe kabisa hakuna. Hata kama tumezinguana mmoja akipata tatizo tunasaidiana kwanza. Damu nzito wakuu. Kusema kuwa mtu baki atakuwa na uchungu kuliko ndugu yako wa damu ni kujifariji upumbavu. Kama mna mifarakano kaeni chini mtatue. Sisi tuko 6 kwa mama mmoja ila ninawajua wengine watatu kwa mama tofauti... imagine nina mdogo wangu niliyemzidi miaka 35... wazee wa kiafrika wazinguzi sana
Hahahaha angalia nawe usizae hivyo
 
Baba na mama mmoja sio shida sana, shida baba mmoja mama tofauti. Hapa ndio visa vingi tunasikia vya mirathi hutokea...
 
NI kweli, reference Elon Musk anao wengi kama timu ya mpira na sub juu
Huyo ni mmoja katika mabilioni. Maskini wengi wana watoto wengi. Tukisema tutumie mfano wa Elon Musk basi itabidi tukubaliane na wale mataahira wanaosemaga darasa la 7 wengi ni matajiri kuliko waliosoma.
 
Hahahaha angalia nawe usizae hivyo
Mimi ninauchukia sana umaskini kwa sababu nimeuishi. Bora nisiwe hata na mtoto kuliko kuwa naye halafu akaishi kwenye umaskini uliokithiri kama nilioishi mimi hadi naingia chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom