Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Inawezekana Afrika tuna wanafalsafa wengi sana, lakini hatuandiki tu mambo.Nyerere had a ton of common sense.
Sasa ukichanganya common sense nzuri aliyonayo mtu, uwezo mkubwa wa kupokea taarifa na kuzichakata, uwezo mzuri wa kuwasilisha taarifa na mawazo yake kwa watu kwa lugha inayoeleweka kirahisi, ndo unapata mtu kama Nyerere.
Ambaye hawezi kumwelewa Nyerere kwenye hiyo hotuba, huyo atakuwa ana tatizo tu la kuelewa.
Mimi kabla hata ya kuujua msimamo wa Nyerere kuhusu mahari, kimsingi akili yangu ilikuwa inawaza hivyo hivyo kama yeye.
Toka nikiwa mdogo kabisa nilikuwa naona kuna kitu hakiko sawa katika suala zima la kutoa mahari, ambayo wakati mwingine ilikuwa inatolewa kama pesa. Huko Usukumani suala la mahari ni kubwa sana.
Sasa hiyo ilikuwa ni common sense yangu tu ya utotoni mimi bila kuhusisha akili yangu na ile ya kuchanganya na za wengine.
Baada ya kukua, kusoma soma, kutembea huku na kule duniani, kubadilishana mawazo na watu, ndo mtu unajikuta unakubaliana sasa na hoja za watu kama akina Nyerere ambazo walizitoa kabla hata mtu hujazaliwa.
Naamini hata yeye Nyerere kabla ya kupata fursa ya kusoma na kusafiri duniani, alikuwa na hayo mawazo ya usawa na baada ya kusafiri na kusoma, ndo akayanoa vizuri hayo mawazi yake.
Hotuba nyingi sana za Nyerere ukizisikiliza, hotupata vitu vingi ambavyo hutokubaliana naye.
Hiyo haimaanishi kwamba alikuwa sahihi kwenye mambo yote.
Ila kwa ujumla, ukimfuatilia vizuri utaona kwamba alikuwa ni mtu anayefikiria kimantiki sana.
Yani tuna mifumo mingi sana batili, na watu wengi sana wanaona ubatili huo, lakini, watu wengi hao, kwa kipindi kirefu, wamekuwa wagumu kufunguka na kuiondoa hii mifumo batili. Kwa sababu nyingi tu, mojawapo ikiwa ni social penalty ya kuondoa mifumo hii batili.
Ikiwa mwanamke anaangaliwa kama mali na familia zinanufaika kwa kumuuza kwenye ndoa, kuondoa mfumo huo ni kuondoa mfumo unaoizalishia familia kipato, wengi hawatapenda hilo.
Ila, wenzetu wamejikubalia kwamba, kuwe na uwazi, watu waandike sana mapungufu, halafu mabadiliko yakubalike.
Ndiyo maana unaweza kukuta mpaka leo tunamnukuu John Stuart Mill kwenye mambo ya uhuru, wakati kwetu tunao kina Nyani Ngabu kibao waliofikiria hivyo hivyo kwa miaka mingi sana.