Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Nyerere had a ton of common sense.

Sasa ukichanganya common sense nzuri aliyonayo mtu, uwezo mkubwa wa kupokea taarifa na kuzichakata, uwezo mzuri wa kuwasilisha taarifa na mawazo yake kwa watu kwa lugha inayoeleweka kirahisi, ndo unapata mtu kama Nyerere.

Ambaye hawezi kumwelewa Nyerere kwenye hiyo hotuba, huyo atakuwa ana tatizo tu la kuelewa.

Mimi kabla hata ya kuujua msimamo wa Nyerere kuhusu mahari, kimsingi akili yangu ilikuwa inawaza hivyo hivyo kama yeye.

Toka nikiwa mdogo kabisa nilikuwa naona kuna kitu hakiko sawa katika suala zima la kutoa mahari, ambayo wakati mwingine ilikuwa inatolewa kama pesa. Huko Usukumani suala la mahari ni kubwa sana.

Sasa hiyo ilikuwa ni common sense yangu tu ya utotoni mimi bila kuhusisha akili yangu na ile ya kuchanganya na za wengine.

Baada ya kukua, kusoma soma, kutembea huku na kule duniani, kubadilishana mawazo na watu, ndo mtu unajikuta unakubaliana sasa na hoja za watu kama akina Nyerere ambazo walizitoa kabla hata mtu hujazaliwa.

Naamini hata yeye Nyerere kabla ya kupata fursa ya kusoma na kusafiri duniani, alikuwa na hayo mawazo ya usawa na baada ya kusafiri na kusoma, ndo akayanoa vizuri hayo mawazi yake.

Hotuba nyingi sana za Nyerere ukizisikiliza, hotupata vitu vingi ambavyo hutokubaliana naye.

Hiyo haimaanishi kwamba alikuwa sahihi kwenye mambo yote.

Ila kwa ujumla, ukimfuatilia vizuri utaona kwamba alikuwa ni mtu anayefikiria kimantiki sana.
Inawezekana Afrika tuna wanafalsafa wengi sana, lakini hatuandiki tu mambo.

Yani tuna mifumo mingi sana batili, na watu wengi sana wanaona ubatili huo, lakini, watu wengi hao, kwa kipindi kirefu, wamekuwa wagumu kufunguka na kuiondoa hii mifumo batili. Kwa sababu nyingi tu, mojawapo ikiwa ni social penalty ya kuondoa mifumo hii batili.

Ikiwa mwanamke anaangaliwa kama mali na familia zinanufaika kwa kumuuza kwenye ndoa, kuondoa mfumo huo ni kuondoa mfumo unaoizalishia familia kipato, wengi hawatapenda hilo.

Ila, wenzetu wamejikubalia kwamba, kuwe na uwazi, watu waandike sana mapungufu, halafu mabadiliko yakubalike.

Ndiyo maana unaweza kukuta mpaka leo tunamnukuu John Stuart Mill kwenye mambo ya uhuru, wakati kwetu tunao kina Nyani Ngabu kibao waliofikiria hivyo hivyo kwa miaka mingi sana.
 
Dah.

Nyerere alikuwa mbali sana wenye hili. Shukurani kwa kuweka hii audio hapa.

Nilisoma kitabu cha Profesa Thomas Molony wa University of Edinburgh "Nyerere: The Early Years" kilichojikita na kuangazia miaka 30 ya mwanzo ya maisha ya Nyerere.

Actually kabla ya kuandika kitabu nilipata kuzungumza naye, alikuwa anataka kujua maisha na mahusiano ya wafanyakazi wa Ikulu ya Nyerere na Nyerere mwenyewe, akataka kujua zaidi kuhusu mama yangu na wakati wake akifanya kazi Ikulu ya Nyerere.

Profesa Molony kwa sababu alikuwa anafundisha Edinburgh, aliposoma Nyerere, alifanya utafiti mkubwa sana uliotumia documents za Edinburgh, mpaka insha alizoandika Nyerere akiwa chuoni. Profesa Molony anasema Nyerere aliandika sana kuhusu hili suala tangu alivyokuwa Makerere, akipenda sana kutoa mifano kwenye jamii za kiafrika kama kwao, na kuelezea sana falsafa za John Stuart Mill.

Hii tarehe ya siku ya wanawake mwaka 1975 kwa kweli hapo alikuwa anafundisha kama Mwalimu, earning his title, maana habari hizi kwa Watanzania wengi zilikuwa jambo jipya, na kwa wengine mpaka sasa ni jambo jipya.

Halafu kama mwanafalsafa mzuri, ameepuka logical fallacy ya "argument from authority", amekataa kukubali kitu kwa sababu kipo katika misahafu tu ( jambo ambalo huwa nalisema sana hapa) na kwa upande mwingine amekataa hata kuwataja wanafalsafa kama John Stuart Mill.

He just argued from principles.

Shukurani kwa hii audio.
Mkuu Kiranga ,vipi kitabu chako kiliishakamilika?
 
Mahari ni Utamaduni ,ina maanisha usione vyaelea vilitunzwa mpaka unakutana nae ,alizaliwa akalelewa alisomeshwa aliuguzwa alipoumwa akakua akasaidiwa aanze maisha Sasa wewe unakutana nae yupo ready na maisha labda kaanza kujitegemea na wewe tayari umeanza kujitegemea ni rahisi kusema mmepandana muanze maisha pamoja kwa tamaduni za Africa mtahesabika nyie wahuni tu mmechukuana mnafanya uzinzi tu hamtapata baraka za wazazi ne je mtoto wa watu akikufia utamzika mwenyewe ,akikuambia wazazi wake wanaumwa utaenda kuwaona wazazi wake wewe kama nani .Jamii za watu wa Ulaya na America nyingi ndio hazina hizo mambo ya mahari sababu kubwa zimekomaa na maisha ya kibepari na Serikali zao zina pesa kusaidiana mahitaji binafsi ya watu sio lazima ndugu wahusike kwa Africa tamaduni na Serikali hazijimudu kihivyo ,tamaduni za kiafrica zinaishi kindugu ,zinauguzana ,zinasaidiana zinafurahi na kuhuzunika pamoja ,harusi kwa Africa ni jambo la kindugu na kijamii ,mahari ni sehemu ya tamaduni za Africa hata kama mmeona ulaya peke yenu itawabidi mje Africa kutimiza matakwa ya kitamaduni ,hata makanisani mkitaka mjifungishe ndoa mtaulizwa kama mmemalizana na mambo ya tamaduni zenu kama mahari na wakati mwingine mahari sio lazima.pesa inaweza ambiwa lete blanket ,lete mashuka let ng'ombe ,mbuzi au kuku unajua maana yake? Vijana wengi wa siku hizi wakitajiwa hivyo husema wapigiwe hesabu hivyo vitu shs ngapi ,wazee wanaojua mila hukataa pesa hutaka kama blanket ulete blanket kwao blanket ni kumbukumbu ya kumuaga mtoto wait kuliko pesa ambayo watatumia itaisha na haitakuwa kumbukumbu nzuri ya kuagana na binti yao
Kwani wewe haujalelewa na kuhudumiwa? Kwanini naye asitoe zawadi kwenu?
 
Kwani mwanaume naye huwa hatunzwi na wazazi wake hadi mnasema mtoto umemkuta katunzwa??? Biashara ni biashara tu... Sijawahi ona zawadi inapangwa na comand juu labda biashara tena sio barter trade ya akina vasco da gama bali za karl peters. Kama mahari ni zawadi subiri watakuletea sio uwapangie ng'ombe watatu ilihali hata hujawah fuga kuku shefuuu
 
Kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye.

Basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote, na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari.
Hakuna kitu cha kijinga kama kile ni aheri awe hawala tu na siyo kumchukua na kuanza kuishi naye bila kwenda kutambulika hata kutoa kidogo

Imagine siku ya siku ki kaukita unafikiri nani atakuelewa eeeeeeh

Mavi debe
 
Wazazi hawana haki ya kutaja mahali. Ongea na binti akutajie kiasi cha mahali unachoweza kulipa..

Haifai kukaa na mwanamke ukiwa bado hujamuoa wala kumtolea mahari. Hio sio ndoa bali ni uzinzi.
 
Kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye.

Basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote, na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari.
Kila la kher
 
Mimi nina mawazo haya kulingana na mtazamo wa mahari

Mwanamke ni kiumbe ambacho wanaume tunanunua either direct au indirect katika maisha ya kila siku

Suala la mahari ni biashara ambayo hata wanawake wenyewe hawana shida nayo;
Ukitaka kujua ni biashara kuna kigezo cha quality na price yake
Kuna jamii za kiafrica walipokutana kujadili mahari ya binti mweusi ilikuwa tofauti na ya binti mweupe
Lakini pia kuna specification mfano
Ubikra
Kutokuwa na mtoto
Elimu aliyonayo

Yote haya huathiri bei ya binti.

Wanawake wanajua hii ni biashara na hawana shida na hilo kiasili,

Wengine ukiwafatilia kauli zao zikitoka midomoni mwao wakisema

Nina shepu.
Nina rangi
Nina kimo
Nina elimu

Yote haya huyatumia kuamua bei zao

Wengine hujikuta wakienda nchi za mbali kubadilisha maumbile ili kukutana na sifa za wanaume sokoni.

Kimsingi nifupishe kuwa kiasili mwanamke uwe umemuoa yuko ndani ama hujamuoa utafanya biashara.

Mwanamme legelelege kwenye utafutaji atanyinwa haki yake ya ndoa tena kwa mwanamke aliyemtolea mahari.

Waafrika tumeamua kuwa wakweli tu,tumeamua kufanya biashara ili kieleweke.

Wenzetu wazungu wana namna wasiyoiita mahari lakini wanafanya biashara tu.

Hata hawa wahindi mnaosema wanawake ndo hulipa mahari, hiyo mahali haiendi kwa mwanaume hohehahe.

Tuendelee kulipa mahali, kufanya biashara.
 
Watanzania wengi hawana uwezo wa kufikiri kidhahania.

Wanafikiri ukipinga mahari, wewe ni masikini, huna pesa, ndiyo maana unapinga mahari.

Hawaelewi kwamba kuna watu wanapinga mahari kifalsafa, na wanasaidia kipesa kuliko hata hiyo hela ya mahari.

Kwa watu hawa, ukiwaambia kwamba unapinga ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi, mara moja wana assume wewe ni mweusi.

Hawaelewi kwamba hata mzungu anaweza kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya weusi, kwa sababu za kifalsafa.
Wanawake hawana shida na kutolewa mahari, hawapingi lolote. Ni asili kununuliwa, huwezi kwenda kinyume na asili.

Wao wenyewe hujiweka sokoni ili wanunuliwe na vigezo vingine hujitengenezea mfano kubadili shape.

Kalipe mahali.
 
Ukisema "huwezi kwenda kinyume na asili" hiyo ni logical fallacy, argument from nature. Pia ni logical fallacy ya argument from tradition.

Na tungefuata kanuni hiyo, JF isingekuwapo leo.

Tungesema asiki yetu ni kutumiana jumbe kwa sauti za ngoma na alama za moshi, hatuhitaji hata barua.

Tungesema hata tukiumwa magonjwa tusitumie dawa, maana magonjwa nayo ni asili.

Tungesema tusijenge nyumba za simenti, maana si asili yetu.

Hata haya maandishi tusingeyatumia, si ya asili yetu.

Hata lugha ya Kiswahiki isingekuwapo, kwa sababu imetohia maneno mengi ambayo si ya asili yetu.

It's a ridiculous idea.
 
Unatumia mifano dhaifu ku justify hoja yako

Hoja ya kutumiana jumbe kwa sauti ya ngoma na moshi msingi ni mawasiliano

Hoja ya kujitibu kwa namna yoyote msingi ni kujifutia tiba.

Hoja ya kujenga nyumba ya saruji na tofali msingi ni kujitafutia malazi.

Mawasiliano, kujitatafutia tiba na kutafuta mahali pa kijihifadhi ndio asili ya binadamu, mahitaji haya hubadilika kulingana na teknolojia. Ndio maana tulitoka zama za make, chuma na leo tuko zama za viwanda ambapo msingi ni kurahisusha mahitaji yetu.

Point ya msingi kwenye hoja ya mahari inabaki kuwa pale pale kuwa kwa asili ya kitabia na kimaumbile kuwa mwanamke atazaa, atanyonyesha lakini kwa utashi wa akili yake atapenda kununuliwa na ndipo furaha yake ilipo.

Tofauti na sisi wanaume ambao kuwazalisha hao majike na kutawala ndio asli yetu na furaha yetu ilipo.

Fatilia vyema,.mara kadhaa wanawake wengine walijitokeza kuweka wazi bei zao, namainisha mahari, mwingine hapa juzi niliona akijutangaza kuwa mahali yake ni milioni 500.

Usiponunua chochote kwa mwanamke hata tendo la ngono atakupa kwa kukupimia akiona hujiongezi atakuacha kabisa.

Tunawanunua wanawake katika nyanja nyingi ila hatuwezi kuongea kwa sauti ila tunatumia jina la kuwahudumia.
 
Kuishi na mtoto wa watu bila kutoa mahari sio ujanja. Kuna jamaa alikuwa anaishi na mwanamke ile sogea tukae bahati mbaya mwanamke akafariki. Jamaa kuzika maiti ilibidi atoe mahari kwanza coz walimkazia mazima. Kifupi alipata aibu sana.
 
Unatumia mifano dhaifu ku justify hoja yako

Hoja ya kutumiana jumbe kwa sauti ya ngoma na moshi msingi ni mawasiliano

Hoja ya kujitibu kwa namna yoyote msingi ni kujifutia tiba.

Hoja ya kujenga nyumba ya saruji na tofali msingi ni kujitafutia malazi.

Mawasiliano, kujitatafutia tiba na kutafuta mahali pa kijihifadhi ndio asili ya binadamu, mahitaji haya hubadilika kulingana na teknolojia. Ndio maana tulitoka zama za make, chuma na leo tuko zama za viwanda ambapo msingi ni kurahisusha mahitaji yetu.

Point ya msingi kwenye hoja ya mahari inabaki kuwa pale pale kuwa kwa asili ya kitabia na kimaumbile kuwa mwanamke atazaa, atanyonyesha lakini kwa utashi wa akili yake atapenda kununuliwa na ndipo furaha yake ilipo.

Tofauti na sisi wanaume ambao kuwazalisha hao majike na kutawala ndio asli yetu na furaha yetu ilipo.

Fatilia vyema,.mara kadhaa wanawake wengine walijitokeza kuweka wazi bei zao, namainisha mahari, mwingine hapa juzi niliona akijutangaza kuwa mahali yake ni milioni 500.

Usiponunua chochote kwa mwanamke hata tendo la ngono atakupa kwa kukupimia akiona hujiongezi atakuacha kabisa.

Tunawanunua wanawake katika nyanja nyingi ila hatuwezi kuongea kwa sauti ila tunatumia jina la kuwahudumia.
Argument from nature is a logical fallacy.

Argument from traditionnis a logical fallacy.

Do you even know what a logical fallacy is?
 
Kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye.

Basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote, na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari.
Kuishi naye tu na kumhudumia tayari ni msaada mkubwa sana kwa familia yake
 
Back
Top Bottom