Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Inawezekana Afrika tuna wanafalsafa wengi sana, lakini hatuandiki tu mambo.

Yani tuna mifumo mingi sana batili, na watu wengi sana wanaona ubatili huo, lakini, watu wengi hao, kwa kipindi kirefu, wamekuwa wagumu kufunguka na kuiondoa hii mifumo batili. Kwa sababu nyingi tu, mojawapo ikiwa ni social penalty ya kuondoa mifumo hii batili.

Ikiwa mwanamke anaangaliwa kama mali na familia zinanufaika kwa kumuuza kwenye ndoa, kuondoa mfumo huo ni kuondoa mfumo unaoizalishia familia kipato, wengi hawatapenda hilo.

Ila, wenzetu wamejikubalia kwamba, kuwe na uwazi, watu waandike sana mapungufu, halafu mabadiliko yakubalike.

Ndiyo maana unaweza kukuta mpaka leo tunamnukuu John Stuart Mill kwenye mambo ya uhuru, wakati kwetu tunao kina Nyani Ngabu kibao waliofikiria hivyo hivyo kwa miaka mingi sana.
 
Mkuu Kiranga ,vipi kitabu chako kiliishakamilika?
 
Kwani wewe haujalelewa na kuhudumiwa? Kwanini naye asitoe zawadi kwenu?
 
Kwani mwanaume naye huwa hatunzwi na wazazi wake hadi mnasema mtoto umemkuta katunzwa??? Biashara ni biashara tu... Sijawahi ona zawadi inapangwa na comand juu labda biashara tena sio barter trade ya akina vasco da gama bali za karl peters. Kama mahari ni zawadi subiri watakuletea sio uwapangie ng'ombe watatu ilihali hata hujawah fuga kuku shefuuu
 
Hakuna kitu cha kijinga kama kile ni aheri awe hawala tu na siyo kumchukua na kuanza kuishi naye bila kwenda kutambulika hata kutoa kidogo

Imagine siku ya siku ki kaukita unafikiri nani atakuelewa eeeeeeh

Mavi debe
 
Wazazi hawana haki ya kutaja mahali. Ongea na binti akutajie kiasi cha mahali unachoweza kulipa..

Haifai kukaa na mwanamke ukiwa bado hujamuoa wala kumtolea mahari. Hio sio ndoa bali ni uzinzi.
 
Kila la kher
 
Mimi nina mawazo haya kulingana na mtazamo wa mahari

Mwanamke ni kiumbe ambacho wanaume tunanunua either direct au indirect katika maisha ya kila siku

Suala la mahari ni biashara ambayo hata wanawake wenyewe hawana shida nayo;
Ukitaka kujua ni biashara kuna kigezo cha quality na price yake
Kuna jamii za kiafrica walipokutana kujadili mahari ya binti mweusi ilikuwa tofauti na ya binti mweupe
Lakini pia kuna specification mfano
Ubikra
Kutokuwa na mtoto
Elimu aliyonayo

Yote haya huathiri bei ya binti.

Wanawake wanajua hii ni biashara na hawana shida na hilo kiasili,

Wengine ukiwafatilia kauli zao zikitoka midomoni mwao wakisema

Nina shepu.
Nina rangi
Nina kimo
Nina elimu

Yote haya huyatumia kuamua bei zao

Wengine hujikuta wakienda nchi za mbali kubadilisha maumbile ili kukutana na sifa za wanaume sokoni.

Kimsingi nifupishe kuwa kiasili mwanamke uwe umemuoa yuko ndani ama hujamuoa utafanya biashara.

Mwanamme legelelege kwenye utafutaji atanyinwa haki yake ya ndoa tena kwa mwanamke aliyemtolea mahari.

Waafrika tumeamua kuwa wakweli tu,tumeamua kufanya biashara ili kieleweke.

Wenzetu wazungu wana namna wasiyoiita mahari lakini wanafanya biashara tu.

Hata hawa wahindi mnaosema wanawake ndo hulipa mahari, hiyo mahali haiendi kwa mwanaume hohehahe.

Tuendelee kulipa mahali, kufanya biashara.
 
Wanawake hawana shida na kutolewa mahari, hawapingi lolote. Ni asili kununuliwa, huwezi kwenda kinyume na asili.

Wao wenyewe hujiweka sokoni ili wanunuliwe na vigezo vingine hujitengenezea mfano kubadili shape.

Kalipe mahali.
 
Wanawake hawana shida na kutolewa mahari, hawapingi lolote. Ni asili kununuliwa, huwezi kwenda kinyume na asili.

Wao wenyewe hujiweka sokoni ili wanunuliwe na vigezo vingine hujitengenezea mfano kubadili shape.

Kalipe mahali.
Ukisema "huwezi kwenda kinyume na asili" hiyo ni logical fallacy, argument from nature. Pia ni logical fallacy ya argument from tradition.

Na tungefuata kanuni hiyo, JF isingekuwapo leo.

Tungesema asiki yetu ni kutumiana jumbe kwa sauti za ngoma na alama za moshi, hatuhitaji hata barua.

Tungesema hata tukiumwa magonjwa tusitumie dawa, maana magonjwa nayo ni asili.

Tungesema tusijenge nyumba za simenti, maana si asili yetu.

Hata haya maandishi tusingeyatumia, si ya asili yetu.

Hata lugha ya Kiswahiki isingekuwapo, kwa sababu imetohia maneno mengi ambayo si ya asili yetu.

It's a ridiculous idea.
 
Unatumia mifano dhaifu ku justify hoja yako

Hoja ya kutumiana jumbe kwa sauti ya ngoma na moshi msingi ni mawasiliano

Hoja ya kujitibu kwa namna yoyote msingi ni kujifutia tiba.

Hoja ya kujenga nyumba ya saruji na tofali msingi ni kujitafutia malazi.

Mawasiliano, kujitatafutia tiba na kutafuta mahali pa kijihifadhi ndio asili ya binadamu, mahitaji haya hubadilika kulingana na teknolojia. Ndio maana tulitoka zama za make, chuma na leo tuko zama za viwanda ambapo msingi ni kurahisusha mahitaji yetu.

Point ya msingi kwenye hoja ya mahari inabaki kuwa pale pale kuwa kwa asili ya kitabia na kimaumbile kuwa mwanamke atazaa, atanyonyesha lakini kwa utashi wa akili yake atapenda kununuliwa na ndipo furaha yake ilipo.

Tofauti na sisi wanaume ambao kuwazalisha hao majike na kutawala ndio asli yetu na furaha yetu ilipo.

Fatilia vyema,.mara kadhaa wanawake wengine walijitokeza kuweka wazi bei zao, namainisha mahari, mwingine hapa juzi niliona akijutangaza kuwa mahali yake ni milioni 500.

Usiponunua chochote kwa mwanamke hata tendo la ngono atakupa kwa kukupimia akiona hujiongezi atakuacha kabisa.

Tunawanunua wanawake katika nyanja nyingi ila hatuwezi kuongea kwa sauti ila tunatumia jina la kuwahudumia.
 
Kuishi na mtoto wa watu bila kutoa mahari sio ujanja. Kuna jamaa alikuwa anaishi na mwanamke ile sogea tukae bahati mbaya mwanamke akafariki. Jamaa kuzika maiti ilibidi atoe mahari kwanza coz walimkazia mazima. Kifupi alipata aibu sana.
 
Argument from nature is a logical fallacy.

Argument from traditionnis a logical fallacy.

Do you even know what a logical fallacy is?
 
Kuishi naye tu na kumhudumia tayari ni msaada mkubwa sana kwa familia yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…