Wale Graduate mlioweza kujiajiri mlitumia mbinu (njia) kuweza kujiajiri?

Wale Graduate mlioweza kujiajiri mlitumia mbinu (njia) kuweza kujiajiri?

Hebu weka wazi mkuu, unafanya inshu gani?
Financial markets mkuu. Hii ni saiv tu mda huu...
Screenshot_20200711-102254_MetaTrader%205.jpg
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Akhsante kwa kunitia moyo.
Mimi nilikuwa siamini katika kufanya hizo biashara.
Nitajaribu,skills kwa kiasi ninazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
My dear You should never quit...try it, try it, try it ...utakuja enjoy sana apo badae...

Good things take time...

Usikubali kuyumbishwa na mtu...
 
Kutokana hili tatizo la ajira kuzidi kuongezeka hapa nchini na kuacha baadhi ya Graduate wakizagaa tu mtaani, kuzurula mtaani, kukaa nyumbani tu naomba mtu anisaidie kutupa njia au mbinu mlizotumia kuweza kujiajiri.

Graduate wengi sana wapo mtaani kwa sasa hawajaweza kujiajiri, wengine bado wanasumbuliwa na mawazo (stress) zaidi ya mwaka wa tatu sasa hivi. Je, nyie mlioweza kujiajiri mlianzaje hadi mkafanikiwa kujiajiri ?

Ni njia (mbinu) gani mlitumia hadi mkaweza kujiajiri?

++Kama vile kupata mtaji(mlianza na mtaji wa shingapi?)

++Biashara mlizo anza nazo

+++Changamoto

+++ Kukwepa aibu na mengineyoo

Naomba mtuambie jinsi mlivyo fanya hili litasaidia sana graduate waweze kupata fikra mpya na waweze kujiajiri huku wanatafuta ajira wengine wajiajiri kabisa kuliko kukaa tu nyumbani, kuzurula mtaani, kushinda kwenye mitandao.
Rafk angu mmoja hivi waliunga kikundi wa4
Walifungua kampuni wakiwa chuo
Wakaanza kutafuta tenda ya kazi walizosomea...
Wakaanza kupata kidogo kidogo...wakajishkiza ofisi za wazazi na muda mwingine majumbani

Wamesota sana sana na bado wanapambana lakini their future is too bright tayari matunda wanayaona..wanaishi comfortably saivi ...wana ofisi yao saivi nzuri mnooo ila imepita miaka 8!the hustle is real!

So mnaweza jaribu
Ni idea mojawapo
 
Huu ujinga ndiyo sitaki kuusikia. Na kama kweli wewe ndiye msomi basi taifa limekufa hili. Unaanza kuuliza utalimia nn? Unauliza utang'oa vipi visiki shambani?

Huyo bibi na babu yako mpk leo wamekuwa wazee nani amekuwa akiwafanyia hizo kazi? Sasa wewe una kitu cha ziada "elimu" dhidi ya hao bibi na babu zako. Unashindwa vipi kuishi kwa kilimo?

Kwahiyo unataka upewe ajira ya mshahara wa laki 2 katikati ya jiji ama mji? Ambapo utaishia kuishi kwa kukopa kopa unga kwenye maduka ya Mangi. Acha ujinga kilimo kinalipa, ndiyo maana 80% ya watanzania wanakitegemea. Wewe msomi gani unakiogopa kilimo?

Umenichefua wewe!!
Acha kashfa mwenzio anapotoa hoja,swali alilouliza linaonyesh wazi kijana ni msomi kwa kuwa ameweza kuwaza extra miles,haya tukisema tufanye kilimo Cha mababu zetu tutafika wapi?tunahitaji mapinduzi ya kilimo hicho kilimo Cha mkono atang'oa visiki vingapi?
 
Mkuu Mimi ni mhitimu wa 2018, mpka hapa nilipo leo nilisota sana nilianza na biashara ya mchele lakini baadae nikabadili gia.

Kwasasa ninajishugulisha na biashara ya samaki kutoka mwanza( Sangara na sato), kiukweli ni biashara nzuri sana!!

Unafanyaje? Natumiwa samaki Mwanza - Moshi wakifka nna ofisi nauza wabichi jumla na rejareja, lakini kuna department nyingne nimeweka mdada huwa anakaanga Sangara vipande kuanzia 1500, 2000,na 2500.

Kwa siku nakaanga kilo 10- 15, wakati wabichi inategemea na siku hiyo wateja wangapi wana hamu ya kula samaki lakini sio chini ya kilo 10.

Na oda za supermarket pia huwa nawauzia, na watu wahotelini pia.

Nilianza na kilo 50 za sangara na sato 50kg, now nna uwezo wa kuagiza 200kg. Karbu kwa maswali View attachment 1503055
Hongera sana mkuu kwa kuthubutu.
 
Acha kashfa mwenzio anapotoa hoja,swali alilouliza linaonyesh wazi kijana ni msomi kwa kuwa ameweza kuwaza extra miles,haya tukisema tufanye kilimo Cha mababu zetu tutafika wapi?tunahitaji mapinduzi ya kilimo hicho kilimo Cha mkono atang'oa visiki vingapi?
Ukinisoma katikati ya mistari sikupigia debe kilimo cha mkono. Ninachopinga viakali hapa ni graduates kukaa wakililia ajira wakikataa kufanya shughuli za kilimo.

Wako tayari kufanya kazi za kuajiriwa zisizo na staha na ujira kidogo. Lkn ukiwagusia suala la kilimo wanapiga kelele za kukosa mitaji . Ndiyo maana nimetoa ushauri kwamba ni vema graduates wabadili fikra. Wakubali kuanza kilimo kwa mtaji wa nguvu na elimu zao ili waanze kuokoteza fedha zitakazo wapelekea kuwa na uwezo wa kifedha. Baada ya hapo sasa ndiyo wanaweza kufanya kilimo biashara.

Kwa ufupi graduates waanze na kilimo malengo ndipo wafanye kilimo biashara. Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Wasitake kuanza na makubwa wakati madogo hawana.
 
Faida ipo ndo maana naendelea kufanya.
Kuhusu changamoto zipo, kutumiwa size kubwa( samaki wa kilo 9) wakati soko langu linahtaji samaki size ya Kati ( 1.5kg - 2.5kg). Samaki akiwa mkubwa Sana ni hasara, sababu baada ya kukata kichwa chache kitakuwa na uzito mkubwa ( labda upate mteja wa kununua mzima)

Pili kuna baadhi ya siku unaweza kupokea samaki wawili au watatu wameharibika lakini hapa hutegemea sana na mtu anayekutumia mzigo, kwangu mm hutokea mara chache sana kwa mwezi ata Mara 1, au isitokee kabsa!! Kijana wangu mi mwaminifu mno.

Kubadilika badilika kwa bei, kila week samaki hubadilika bei, inaweza Kupanda au kushuka, ila ikishuka utaenjoy Sana, mfano ikashuka mpka 3400 wakati ww huku unauza 6000 au 6500 na wateja hawajui kama imeshuka!!.

Tatu, hakuna kipimo cha usahihi kwamba hapa ni kilo 1 au nusu Bali nnakata kwa uzoefu tu, uzoefu ndo umenifundisha kuwa nikikata hapa ni kilo 1 au hapa ni nusu kilo, ila ukikosea kukata ni changamoto kumshawishi mteja aongeze pesa kisa eti umekosea kukata.

Ila mpka saiv nna uwezo mzuri kabsa wa kukadilia kuwa hapa ni nusu au hapa ni kilo, mpka wateja huwa wanashangaa sana!!

Umeme, ila kwangu sijawahi kupata hili tatzo mpka nikakosa raha eti umeme umekatika, ukikatika baada ya mda unarudi, Ila kama upo vzr unaweza kununua generator.

Ntakuja kuendelea
Nimependa uzoefu wako hongera sana👏🏽
 
Mkuu Mimi ni mhitimu wa 2018, mpka hapa nilipo leo nilisota sana nilianza na biashara ya mchele lakini baadae nikabadili gia.

Kwasasa ninajishugulisha na biashara ya samaki kutoka mwanza( Sangara na sato), kiukweli ni biashara nzuri sana!!

Unafanyaje? Natumiwa samaki Mwanza - Moshi wakifka nna ofisi nauza wabichi jumla na rejareja, lakini kuna department nyingne nimeweka mdada huwa anakaanga Sangara vipande kuanzia 1500, 2000,na 2500.

Kwa siku nakaanga kilo 10- 15, wakati wabichi inategemea na siku hiyo wateja wangapi wana hamu ya kula samaki lakini sio chini ya kilo 10.

Na oda za supermarket pia huwa nawauzia, na watu wahotelini pia.

Nilianza na kilo 50 za sangara na sato 50kg, now nna uwezo wa kuagiza 200kg. Karbu kwa maswali View attachment 1503055
Mchele ulikuwa unauzaje jumla au rejareja? Na ilikuwaje ikafa namaanisha changamoto ulizokutana nazo
 
Rafk angu mmoja hivi waliunga kikundi wa4
Walifungua kampuni wakiwa chuo
Wakaanza kutafuta tenda ya kazi walizosomea...
Wakaanza kupata kidogo kidogo...wakajishkiza ofisi za wazazi na muda mwingine majumbani

Wamesota sana sana na bado wanapambana lakini their future is too bright tayari matunda wanayaona..wanaishi comfortably saivi ...wana ofisi yao saivi nzuri mnooo ila imepita miaka 8!the hustle is real!

So mnaweza jaribu
Ni idea mojawapo

Walikua na maono sawa, hongera kwao.
 
Nilikodi shamba hekari 5
Nikalima cabbage, nikahudumia vizuri ilikuwa kilimo cha umwagiliaji

Nilimwagia
Kupiga dawa
Kuweka mbolea za viwandani
Kupalilia nk

Nilitumia/nilipoteza almost 9.7m

Zilipokomaa, soko likawa kizungumkuti, serikali inazuia wakenya kuja kununua mazao na vikwazo lukuki vya kijinga sana
Wateja niliokuwa nawategemea sana ni wakenya kwani wananunua kwa wingi na kwa bei nzuri.

hadi mvua iliponyesha zikaozea shambani zote
Sikupata hata Tsh 100

Mtu asiyelima ni kawaida kuongelea kilimo kiraisi sana lakini uhalisia hauko hivyo

Serikali inatia wananchi umasikini kwa kiwango kikubwa mno kwa matamko na makatazo ya kijinga na yasio ya kiungwana

Juzi nilimsikia Bashe akilizungumzia hili watu wanalima halafu serikali inawakataza kuuza mazao yanaharibika kama ilivyotokea pia kwenye mahindi mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Sumbawanga (Rukwa)
They don't care!!
pole sana ,japo naamini ushapoa
 
Back
Top Bottom