Wale mliooa wake zenu wakiwa na zaidi ya miaka 30 na wadada mlioolewa mkiwa na zaidi ya miaka 30 pia, karibuni kwa maoni na uzoefu wenu

Wale mliooa wake zenu wakiwa na zaidi ya miaka 30 na wadada mlioolewa mkiwa na zaidi ya miaka 30 pia, karibuni kwa maoni na uzoefu wenu

Bado sana,mamdogo wangu kavaa shela mwakajana akiwa na 44 sema shida mtoto kusumbuka kumpata
Sasa mwaka jana tu na unasema amesumbuka kupata mtoto...

Au alisumbuka kabla ya kuvaa shela?
 
Tatizo % kubwa ya wadada wenye 27+ years na hawana mtu wa maana almost wanakuwa na ma shida mengi.
Unawakuta kwenye dating apps wamejipa masifa kedekede I can cook I can do this n that... Mara God fearing girl.....
But na sisi wanaume tu najiuliza 1 question... Kwamba with all em qualities why you still single??? Na hapo ndo huwa tu naogopa majibu na tunakimbia.
Maana tunajua kuwa kama the last Guy amekimbia shida zako kwa sifa zote hizo ulizotaja unazo then wewe kweli ni PASUA KICHWA. ndo maana ukishafika hiyo age basi kupigika ni lazima na masela wanasepa.
 
Hello wakuu!,

Happy Sunday to everyone, karibuni kwa maoni yenu, je ni kweli ukiwa above 30yrs kuna possibility ya kutokuolewa kwa wadada? Sababu ni nini, kwani suala la ndoa linazingatia umri na si upendo baina yenu mnaotarajia kuwa wanandoa? Mliooa na kuolewa katika umri huo je kuna tofauti yoyote mnayoiona? Maisha yanaendaje? Ushauri wenu ni upi kwa wengine?.

Kumekuwa na maneno ya kutishana mitaani na hata baadhi ya threads humu kwamba mdada ukiwa na 30s ndiyo basi tenaa, sometimes hupelekea wadada kuolewa tu na mtu yeyote hata wasiyempenda sababu tu ya kigezo hicho kwamba she's in her 30s na anahofia atakosa ndoa.

Zamani mtaani kwetu nilikuwa nikisikia wakisema aunt fulani hajaolewa hadi leo, wanamshangaa, naona sasa kibao kimegeuka nimekuwa huyo aunt pia aah😂.

Karibuni na muwe na Jumapili njema...
Menopause inakaribua
Kama ni gari imetembea km laki moja,tangu uvunje ungo moaka 30 kitu kimeota sugu
 
Hii thread ina posts zinaweza kumfanya mdada akawa na siku mbaya sana kifikra. Watu wanajua kutema sumu sio poa!!
Ha ha ha labda awe mgeni na JF lakini kama mwenyeji hizi mambo zipo enzi na enzi humu.
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo.

Kwa nini tunaipa ndoa uzito mkubwa ambao haistahili. Kwani maisha bila ndoa hayawezekani?

Unamkuta dada wa watu mzuri tu na tabia yake safi lakini analiwa ovyo na wanaume wasioeleweka na wasiompenda kisa kutafuta ndoa. Tena wengine shida yao ni kuvaa shela tu awakoge kina Mwajuma Nchokonoe kwenye vijiwe vya umbea vya kisasa vya instagram na whatsapp.

Ladies you can make your life beautiful even in absence of marriage.

Naona umeamua kupoteza mda wako kuwashauri wanawake madhara ya chips yai kuku

Ndugu wakitoka hapo wanaenda kula hizo hizo japo hapo unawaona wanaku sapoti mada yako

By the way,huwezi kupingana na nature,kinachowasumbua sio ndoa ni nature na perceptions za jamii
 
Kuolewa na kuoa ni hiyari sio lazima,
Kuna maisha mengine nje ya ndoa, acha maisha yaendelee.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Halafu mambo yetu yaleee mtu unapata wap sasa kama huna mume wala muke?
 
Ndo narudi pale pale aliyeweka ndoa focus yake ya maisha,ni mtu ambaye anamtegemea binadamu mwenzake. Ushauri wangu upo pale pale wanawake wajiongezee thamani wataolewa. Unaweza ukafocus uolewe, ukabadili mienendo yako dada yangu lakini Kuna mahali utashindwa ku compromise. Maisha ni zawadi Mungu kakupa ishi utakavyo jipende jipe kipaumbele trust me utapata furaha ya kudumu.
Huo ni mtazamo wako hauwezi ukawa mtazamo wa watu wote.
We are interdependence to each other huwezi ku-declare humtegemei mtu
yeyote utakuwa unadanganya unless wewe uwe motivational speaker.
 
Mimi hapa mshangazi wa haja nipo na sina shaka. Niko na very early 30s. Familia naitamani na kuolewa natamani lakini siko tayari kuolewa kwa mtu sijampenda na pressure ya society pia. Sina hofu kabisa. Mbona wapo hawajaolewa na life linasonga? Do not marry mtu hujawa tayari kuishi nae ili kuimpress jamii. Mshangazi mwenyewe nna roho yangu ya kizungu... usiteseke shoo. Kwani Mzee Shirimaa amekutelekeza tena? Pale umepigwa shoo[emoji23]

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Hapana hizo ni hulka na mawazo ya kibinadamu,jambo la kuolewa halina mda wala ukomo wa umri.

Mimi binafsi nimeshuhudia ndoa nyingi sana ambazo wanawake wameolewa wakiwa above 35.

Mambo ya msingi za kuzingatia ili kutengeneza njia ya kuolewa

-Kujipenda kwa kuvaa vizuri na kuwa na muonekano mzuri sisemi ujichubue,oga vizuri kila sehemu ya mwili vizuri,paka mafuta au losheni ambayo itang'arisha mwili na siyo kukuharibu,tumia perfume yenye harufu nzuri na siyo ya kukera watu na kujitunza vizuri usigawe mwili kwa kila mtu siyo karanga hizo.Msubiri mumeo aje afungue vitu vipya kwenye box usije ukawa na kutu.[emoji177]

-kuwa na mwenendo na tabia njema uwapo kwenye jamii,kazini,kanisani au sehemu yoyote

-Kula chakula bora kwa kuzingatia afya yako

-kufanya mazoezi yatakayokuweka fit kiakili na kimwili.

-kuhudhuria kwenye ibada mbalimbali,seminar,Mikutano,sherehe na kwenye shughuli za kijamii kama misiba na shughuli za maendelea.

-Fanya kazi kwa bidii hakuna mwanaume anayempenda mwanamke mvivu,akimpenda basi anataka kumtumia
tu.

-Njia nyingne muhimu sana itakayokuhakikishia kumpata umpendae naye akupendaye ni kusali kwa imani kwa Mwenyezi Mungu bila kukata tamaa.Nakuhakikishia utapata unachositahiri kupata.[emoji120][emoji120]

Hizi ni njia anazoweza kutumia hata mwanaume kupata mke sahihi....

NAPENDA KUWATAKIA VALENTINE DAY,,[emoji312][emoji312][emoji3531]KWA WAPENZI,WANANDOA, FAMILIA,JAMAA NA MARAFIKI WOTE

UPENDO UDUMU KATIKA KATI YETU NA WATU WOTE[emoji123][emoji177][emoji322][emoji322]

Nifollow kupitia
petermarco65@gmail.com
 
Tatizo % kubwa ya wadada wenye 27+ years na hawana mtu wa maana almost wanakuwa na ma shida mengi.
Unawakuta kwenye dating apps wamejipa masifa kedekede I can cook I can do this n that... Mara God fearing girl.....
But na sisi wanaume tu najiuliza 1 question... Kwamba with all em qualities why you still single??? Na hapo ndo huwa tu naogopa majibu na tunakimbia.
Maana tunajua kuwa kama the last Guy amekimbia shida zako kwa sifa zote hizo ulizotaja unazo then wewe kweli ni PASUA KICHWA. ndo maana ukishafika hiyo age basi kupigika ni lazima na masela wanasepa.
Kwenye badoo huko wanajipa misifa, kuna mwanagu dereva wa halotel anawabutua, tena wengi wao ni 25-35.
 
Back
Top Bottom