Wale mliowahi kuagiza magari online

Unataka kusema bei ya Vitz (2005) mfano ya $100, hadi kufikisha TZ, gharama yake itakuwa ni kubwa kuliko ukinunua showroom? Huyo wa showroom faida anapataje? Kama hujawahi kuagiza gari, soma na ujifunze kwa wengine. walioagiza.
Za shoo room zinaagizwa nyingi so inakua bei rahisi kuanzia kununua na garama nyingine. Ujasoma biashara ndo maana unalopoka unazani hii biashara ya kuuza kuku. Tafuta watu wa bandalini kwa ushauri zaidi
 
Hujui kitu wewe acha maneno mengi. Nitakupa mfano mmoja, kwa leo Beforward, Toyota Rush (2007) ya bei nafuu ni $4272 (karibu na sh 9.6mil), ushuru wake ni sh 7.1mil, jumla 16.7mil. Wa showroom hajaweka faida yake ambayo ni 2-3 mil. Hebu niambie, ni showroom gani DSM ambayo utapata hiyo gari, inauzwa chini ya milioni 16, kwakuwa ukiagiza magari mengi bei hupungua, labda gari la kufugia kuku ndiyo utapata chini ya hapo. Ushauri wa kwanza, acha kuongea mambo usiyoyajua ili uonekane unajua. Pili, rudi shule kajifunze kuandika maneno ya Kiswahili.
 
unazani ni biashara za nyanya agiza gari ujionee mwenyewe. Siwezi bishana na viraza
 
unazani ni biashara za nyanya agiza gari ujionee mwenyewe. Siwezi bishana na viraza
Nilishaagiza huu mwaka wa 3, na nishasaidia watu zaidi ya watatu, nakushangaa wewe uongeaye usivyovijua. Mimi nimekupa mifano hai, wewe unatoa kejeli, inadhihirisha hakuna ujualo. Zunguka showrooms za DSM kisha urudi na ushahidi wa wazi kutetea hoja yako. Achana na habari za kwenye vijiwe vya kahawa.
 
habari zako ndo za vijiwe vya kahawa kuonyesha mimi natoa habari za vijiwe vya kahawa weka hizo documents au nakala kwenye huu huzi(thread) kusibitisha kama ni kweli
 
Nimeshangaa kwa kweli....huyo supplier ni Bomu

That's y inashauriwa makampuni ya maana kwa kuagizia Gari only SBT na BeFoward wako makini!
 
Mkuu we kiboko!

Utofauti wa Gari likiwa Japan na live ni upi?

Tena mi naona likija live ndo linakuwa jipya kuliko hata picha
 
Ukifata Gari showroom ni lazima wanataka mafaida tena kuanzia 4- 5m

Hakuna biashara isiyo na faida dunia hii
 
habari zako ndo za vijiwe vya kahawa kuonyesha mimi natoa habari za vijiwe vya kahawa weka hizo documents au nakala kwenye huu huzi(thread) kusibitisha kama ni kweli
Zipo nyingi siwezi weka zote hapa, sema unataka ipi kati ya hizi:
1. Export certificate
2. Shipping liner ilyoleta gari
3. Certificate of export inspection
4. Certificate of Appraisal toka EAA
5. Invoice ya gari toka (Beforward)
6. Payment note (TRA) kuwa gari imelipwa ushuru
7. Assessment document (TRA)
8. Tax payment slip
9. Motor vehicle license
 
Hizo document 9 ndo unasema nyingi ziweke hacha mbwembwe na maneno ya kiswahili. Weka document kuanzia unaagiza mpaka linaingia barabarani acha polojo
 
Ukifata Gari showroom ni lazima wanataka mafaida tena kuanzia 4- 5m

Hakuna biashara isiyo na faida dunia hii
Witnenessj, mwambie huyo sababu yeye anasema, gari la kuagiza, mfano Vitz ya dola 1500 ya mwaka 2000, ukiagiza, litakuwa na bei juu kuliko la showroom la bei hiyohiyo. Na hoja yake ni kwamba, wale wa showroom hupata hayo magari kwa bei nafuu sababu hununua mengi kwa wakati mmoja. Hii kitu hakuna.
 
Hakuna kitu kama hicho asee...

Watu tunaagiza Magari nje ili kupunguza gharama za showroom so simple!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…