Hujui kitu wewe acha maneno mengi. Nitakupa mfano mmoja, kwa leo Beforward, Toyota Rush (2007) ya bei nafuu ni $4272 (karibu na sh 9.6mil), ushuru wake ni sh 7.1mil, jumla 16.7mil. Wa showroom hajaweka faida yake ambayo ni 2-3 mil. Hebu niambie, ni showroom gani DSM ambayo utapata hiyo gari, inauzwa chini ya milioni 16, kwakuwa ukiagiza magari mengi bei hupungua, labda gari la kufugia kuku ndiyo utapata chini ya hapo. Ushauri wa kwanza, acha kuongea mambo usiyoyajua ili uonekane unajua. Pili, rudi shule kajifunze kuandika maneno ya Kiswahili.