Wale mnaoulizaga inakulaje wese, sasa mchina kashamaliza kazi kwa gari zisizoenda sheli!

Wale mnaoulizaga inakulaje wese, sasa mchina kashamaliza kazi kwa gari zisizoenda sheli!

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Ev 1.PNG



ev2.PNG


Wazee hizo gari zinaitwa EV Cars yani Electronic Vehicles, ziko compact size ya kubeba watu wanne size ile ile ya "BEBIWOKA" tulizozoea kupishana nazo mtaani! Habari njema ni kwamba hizi gari zinatumia charger ya mithili ya simu kwahivyo utaweza kuzichaji kila ulalapo usiku! Single charge inaweza kutembea kati ya 100-150km bila usumbufu na ikiwa idle inakuwaga na solar panel inayolichaji betri lake! ikumbukwe hii gari inatumia umeme pekee so hamna trip za kwenda sheli we ni plug tu na umeme! betri huchaji hadi kujaa ni masaa 8-10! Bei ni kitonga kama mnavyoona na unakuwa umenunua gar brand new 0kms kwa around million 9 hapo, ikumbukwe tu kuwa humo ndani ni full mufindi!!!!

wadau mnaonaje je hizi gari ziko makini
 
Nishaagiza moja nimeambiwa mpaka januari naweza kuwa nshalipata, nitawaita mje mushangae
itakuwa safi mkuu, wabongo si unajua wana akili za kondoo ama nyumbu, mpaka waone mtu kaagiza ndio watafuata nyuma hapo! So tegemea chain ya wafuasi
 
Mambo iko TESLA
Hiyo kiboko na ni ghali haswa

James Dyson ambae ni maarufu kwa vacuum cleaner anafungua kiwanda Singapore kutengeneza electric cars

Tuone mchuano wake na tesla
 
Pongezi kwao but I would rather go for Nissan leaf which is Japanese based technology than Chinese technology .

Nissani leaf iko poa,Tesla iko poa sana tatizo iko expensive sana hata hio cheap version wanazotoa(model 3) ni $35,000 hio MRP bado jamaa wa TRA ni shiida aisee.
 
Kwa sasa china wana massive production ya hizo EV mpk Tesla wameanza kupata wasiwasi kuhusu Market.
Yani acha tu, jamaa soko lao kubwa wame target USA ni kweli usemalo maana viwanda vikubwa vimepata kigugumizi sana sidhani kama wataruhusu hali hio iendelee huenda wakapiga ban shipping ya hivi vigari!
 
Shida ya bei za kariakoo ubora unakuwa wa wasiwasi
Ziko za Dollar kati ya 13000-20000 hapo ambazo ni nzuri na bora zaidi na hizo bei hazifikii gharama za Tesla,VW,Ford focus wala Chevrolet Bolt ila utapata premium quality!
 
Ziko za Dollar kati ya 13000-20000 hapo ambazo ni nzuri na bora zaidi na hizo bei hazifikii gharama za Tesla,VW,Ford focus wala Chevrolet Bolt ila utapata premium quality!
Hapo sawa na vipi kuhusu servicability ikizingua unapeleka gereji au kwa mafundi umeme?.
 
Back
Top Bottom