Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

BIG THINKER

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2018
Posts
680
Reaction score
1,436
Haya sasa,

Kwa upande wangu mm nimebahatika kuzaliwa na kukulia kwenye familia ya KISHUA haswaa, nyumba,magari na chakula Cha Kila aina tena Kila siku.

Changamoto ya kuishi kwnye familia ya KISHUA ni kukosa muda Wa kuwa marafiki, pia ukitoka nje ya geti Kila mtu anakushangaa, marafiki wengi wa Kila aina wengine wezi wanakuibia vitu kama mipira nk, wazazi kukuona mtoto hata kama umekuwa, nimeogeshwa na Mama na wadada wa kazi Hadi namalizia la Saba.

IMG-20230201-WA0013.jpg
 
Niliwah kutoroka nikaenda kwa rafiki yangu kwao maisha ya kawaida wakanipa chakula niliharisha sitasahau Hadi nikapelekwa hospital usiku wazaz wa rafiki yangu wakakamatwa na urafiki wetu ukaishia hapo, nisamehe bwana Simon popote ulipo.
 
Ngoja nikae kimya coz JF ukitaka uonekane kua ni mkweli basi jitangaze kua unapitia magumu na upo kwenye dhiki,kila mtu atakuonea huruma na kukuombea dua kisha kukutia moyo, sijui pambana utatoka tu,

Ukisema kua una good life, utasikia acha uongo,mtu mwenyewe upo kwa Shemeji yako unagombania remote na watoto wa Dada yako.

😀 😀
 
Niliwah kutoroka nikaenda kwa rafiki yangu kwao maisha ya kawaida wakanipa chakula niliharisha sitasahau Hadi nikapelekwa hospital usiku wazaz wa rafiki yangu wakakamatwa na urafiki wetu ukaishia hapo, nisamehe bwana Simon popote ulipo.

[emoji23][emoji23][emoji23] dah chakula kilikuwa kina nini? Acha ushamba au umeamua kutukejeli sisi masikini
 
Back
Top Bottom