Wale tuliopigwa fix mbalimbali zamani wakati bado tupo zama za giza bila internet tukumbushane fix mbalimbali

Wale tuliopigwa fix mbalimbali zamani wakati bado tupo zama za giza bila internet tukumbushane fix mbalimbali

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kitambo hiyo zama za mwamba Mwalimu Nyerere Rais wa kwanza wa Tanzania Filling station zilikuwa na majina maalum kutoka nchi za mabeberu, SHELLY, CALTEX, AGIP, BP, ESSO, TOTAL, peke yake sio sasa hivi hata mimi naweza kuanzisha filling station yangu na nikaipa jina la mwendawazimu yeyote kati ya hawa GENTAMYCINE au CAPO DELGADO . 😁😁😁

Sasa kuna Kamba tulikuwa tunapigwa kuhusu logo ya Agip Simba mwenye miguu sita na anatema moto ndio ndio mnyama radi mbinguni, yani ukisikia radi basi huyo mnyama wa Agip ndio anatema moto hapo.

Hebu na wewe tiririka fix ambazo uliamini ni ukweli?

FB_IMG_1694578655798.jpg
 
1.Ukiwa umekaa chini mtu akikuruka iwe ni miguuni au POPOTE utakua mfupi mpaka akurudie......

2.mtu akikupigia ufagio utakua haunenepi..

3.kuchomeka kijiti kichwani ukitenda kosa Ili usichapwe au kunyonyoa kope kadhaa na kuzitupia mlangoni Ili usichapwe....

4.mvua ikinyesha huku jua linawaka eti simba anazaa

5. Mkono ukiwasha usiukune maana ni dalili za kuokota au kupata PESA ☺️😊
 
Sasa nyiewazee wetu nimudamuafaka tukaechini tukubaliane mupigwe ban jf.

mshazeeka mitandao acheni mjikite kulea wajukuu na kusubiria kufa.
humu mitandaoni kumbe unaweza bishana na mwisho kutukana babuyako daa☹️☹️☹️

tuongee vizuri mumebakisha kipi kukiona Ili mtuachie mitandao Sisi kizazi new model?
 
Back
Top Bottom