Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Eeeh namsoma Muddy mzawa wa kawe jina lingine alikuwa anaitwa BABU WA CHIGA mweusiiiii na kigugumizi chake...

Pia kulikuwa na baharia mwingine ana buti kubwa akitembea inaanza buti mwili unafuatia alikuwa anajiita PEACEMAKER hhaaaa hhhaaaaa

True Boy. Long tym aisee.
 
Yule demu alikuwa anatoa tigo yupo humu?
 
Makongo High School wanafunzi ni mwendo wa kunyoa si mademu si wanaume hakuna kubana sijui kuset lakini masista duu walikimbiza hadi watoto wa St Mary's waliokuwa wanabana nywele na kusuka
 
Aiseee inatia faraja sana kusikia hizi stories.. Mm nimekaa miaka minne hapo.. Nimetoka 2009.
Tumekaa na Afande miraji Mpka mauti ilipomkuta na wananchi walilia vile vile walivyokua wanatoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lake.
Babu chacha mpenda mizigo.
Bila kumsahaua Afande sele sijui yule mwenye kitambi mpenda kula.
Namkumbuka major tarimo katupigisha sana pindi la computer kwenye zile lab mbili.
Master mayebe ambae walikua wanasema yuko kwenye intelligence ya jeshi.
Kanali kipingu alipokua akija assembly na sare Zake katui inspire sana.
Major mwaseba.
Kombaha alikua ana mikwara kisa alikua ananimilik kombi ya KLF.
Na wengine wengi..

Bila kusahau ukienda toilet Unakuta chata kubwa la POP2.
tuache utani nyambizi wakati wa Pepa kunaboa...

Makongo imetufundisha sana ujanja na kuchakata akili kuto ku give up maana stiki zilikua zinaanzia getini. Wanawake shika mguu mmoja Wanaume kunja ngumi.

Kuna MP Mmoja nilikua simpend juzi nikamuona kwa aziz ally kashastaafu Nusura nimpige Jiwe.

Kisonga ni Habari nyingine.. Wengine wanasema alikua mjeshi asiyevaa sare wengine wanasema raia tu.. Japo alikua anatafuna sana Dada zetu wa form 5 na 6...hasa wakiwa na. Maumbo nadhifu kwenye zile sketi zenye V
 
Daaaaah sio mchezo Makongo na vituko vyake akina Afande Kisarika, Kombaha...ilikuwa shule ya jeshi lakini wanafunzi wake walikuwa manunda kweli kweli
Kisarika alikua peace mbona au sababu alikua afisa?? Kombaha Sasa ni shidaa... Mungu amrehemu alipo
 
Kuna mwalimu anaitwa kenyaman anabonge la saut apa na mbagara
Alafu walikuja wajeda flani ivi wakuda kinoma tukawaita manyota
Je mnalikumbuka joro
Joro ukoko Ule wa pilau au Wali.. Karibu na Kale ka kibanda ka juisi ya miwa kwa yule mzenji
 
Naaam...maabara ya kemia..
Mkaanga sumu alimwambia mshkaji wangu alivyokua anamuomba pipette ya ziada baada ya ile ya awali kuwa ina leak na haitoi vipimo sahihi. Ilikua kwenye chemistry practical pale lab.. Mshkaji akasema Mkaanga sumu naomba pipette mpya, jamaa akamjibu "pipettia na mboo yako" mbele ya darasa la form 3S3
 
Baada ya Kanali Kipingu kustaafu nafikiri Meja Mwaseba ndiye aliteuliwa kuwa mkuu wa shule

Kama sijakosea alikuwa anafuga mustachi halafu ana wowowo
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Baada ya Kabali Kipingu kustaafu nafikiri Meja Mwaseba ndiye aliteuliwa kuwa mkuu wa chuo

Kama sijakosea alikuwa abafuga mustachi halafu ana wowowo
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Ha ha.. Wowowo Hilo sio la kuuliza..... Yes alikua mkuu wa shule baada ya kanali
 
Daah,, nimekumbuka mbali sana, enzi za Makongo.
Makongo iliyosheheni vipaji kuanzia vya waimbaji, waigizaji, presenters mpaka wachezaji mpira kama kina Henry Joseph Shindika, Juma Abdul wa Yanga almaarufu Juma Kishingo (kisa ana shingo fupi kama kisigino cha mtoto,, teh teh), Juma Kaseja, Nsa Job,,,, bila kumsahau mtoto wa kike msakata kabumbu na shabiki maarufu wa Simba my classmate Shose Masao RIP!!!!
Presenters kama kina Salama Jabir, Sekioni David (Muasisi wa Orijino Komedi ya Kina Mpoki na Joti), Amina Chifupa RIP,,,, list n ndefu sana.

Enzi hizo tuliokaa bwenini,, kama unaingia shift ya mchana basi tunaamshwa kwa kengele saa 12. 30 asbh, unawahi Roll call/ rokoo unakabidhiwa panga au fyekeo kisha unakabidhiwa kajiplot kako chenye majani na vigingi ukaangushe chini.

Thnx kwa mleta mada, umenikumbusha mbali sanaaaaa,,,
 
Asubuhi kwa wale wa bweni kulikuwa kuna kitu kinaitwa WARM UP asubuhi na mapemaa
 
Makongo ilikuwa kwere enzi hizoooo
 
Dah timu ya soka pale wamepita wengi sana akina Amri Kiemba, Pawasa, Wilfred Kidau, Kaseja, Haruna Moshi, John Sebles, Aaron Nyanda, Jerry Tegete, Kaseja, Abuu Mkangwa yaani ilikuwa ni kwereeee
 
Akina Josee Mara wa Clouds Leo Tena, Timothy Chelula wa Azam TV, Mwanahamisi Mish Bomba Magic Fm, Mwani Nyangasa mwandishi wa michezo Dimba.......
 
Nani anaukumbuka ufisadi wa Afande Miraji kwenye vitambulisho ?

Alikuwa anatukalisha kwenye benchi watu wanne kwa mpigo na kutupiga picha kicha anakata tu vichwa na kufanya Passport Size
 
Nani anaukumbuka ufisadi wa Afande Miraji kwenye vitambulisho ?

Alikuwa anatukalisha kwenye benchi watu wanne kwa mpigo na kutupiga picha kicha anakata tu vichwa na kufanya Passport
Size
dah alikuwa mzee wa kujiongeza hatareee kwenye kitengo chake kile ofisi imejaa mafyekeo, majembe, bakora ofisi ya mabati full suti
 
Enzi za Turunya Bar na 4 ways Mwengeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…