Daah,, nimekumbuka mbali sana, enzi za Makongo.
Makongo iliyosheheni vipaji kuanzia vya waimbaji, waigizaji, presenters mpaka wachezaji mpira kama kina Henry Joseph Shindika, Juma Abdul wa Yanga almaarufu Juma Kishingo (kisa ana shingo fupi kama kisigino cha mtoto,, teh teh), Juma Kaseja, Nsa Job,,,, bila kumsahau mtoto wa kike msakata kabumbu na shabiki maarufu wa Simba my classmate Shose Masao RIP!!!!
Presenters kama kina Salama Jabir, Sekioni David (Muasisi wa Orijino Komedi ya Kina Mpoki na Joti), Amina Chifupa RIP,,,, list n ndefu sana.
Enzi hizo tuliokaa bwenini,, kama unaingia shift ya mchana basi tunaamshwa kwa kengele saa 12. 30 asbh, unawahi Roll call/ rokoo unakabidhiwa panga au fyekeo kisha unakabidhiwa kajiplot kako chenye majani na vigingi ukaangushe chini.
Thnx kwa mleta mada, umenikumbusha mbali sanaaaaa,,,