Wale tuliotoka familia masikini na tukatusua kimaisha tukutane hapa

Ingekua kweli Kama ulivyojielezea kwenye uzi wako usingekua na thread zaidi ya 40 kwa kipndi Cha miez miwili tangu ujiunge na jf.
Nambie huo muda wa kung'ang'ana na jf unaupata wapi ikiwa wew ni mtumishi wa ofisi mbili tofauti
Screenshot_20211001-163720.jpg
 
Ingekua kweli Kama ulivyojielezea kwenye uzi wako usingekua na thread zaidi ya 40 kwa kipndi Cha miez miwili tangu ujiunge na jf.
Nambie huo muda wa kung'ang'ana na jf unaupata wapi ikiwa wew ni mtumishi wa ofisi mbili tofautiView attachment 1959370
Upo sahihi, kikubwa ni kupangilia tu muda wako. Mfano, unaweza weka thread hata nne kwa mkupuo. Sasa utashindwaje kuwa na thread 40 kwa miezi hiyo? Kikubwa ni ratiba tu ndugu. Naomba niishie hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitumie nguvu kubwa kutetea hili dogo, uhalisia unakataa hata kama utakesha mpaka asubuhi. Sekta ya umma haiko hivi unavyotaka kueleza.
Halafu mimi sio dogo kaka 31 yrs now! Kwa hiyo nimeongopa sio? Duuh! Hivi umeelewa post yangu kweli? Nina mashaka katika hili!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masikini akipata..hulia mbwata.

Acha vitendo vijidhihirishe na siyo maneno mengi.

Cheo ni dhamana,umetusua kiuchumi,je kijamii?

Kutusua kuna maana pana sana.
Si dhambi mimi kusema hivyo. Sijamkashifu yeyote wala kumdharau. Najaribu kuwapa moyo wote wanaopitia magumu, kupitia hii thread yangu ya historia yangu. Nafikiri umeelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshahara wa m8 kwa mwezi maana yake na majukumu yanqongezeka... huwezi pata mida wa kupost ishu hizi hapa. Kama ni kweli basi una bahati
 
Wanajamvi nawasalimu!

Nilipokuwa chuo niliishi maisha magumu mno, mlo nilikuwa nakula mmoja tu napo ni jioni. Home hakukuwa na hela na hawakuweza kunilipia ada. Hela yote ya boom nilikuwa naigawa kulipa madeni, ada na pango, na kubakiwa na kiasi kidogo mno ambacho hunisogeza kwa siku chache tu.

Wasichana wazuri nilikaa nao mbali kwani sikuwa na cha kuwapa. Wanasema ni bora kujifanya unazo ili uwanase, ila kwangu uongo ulikuwa ni mwiko kwani aibu ya kuumbuka ni kubwa mno. Nimeshakosa tests kadhaa chuo kwa kukosa hela ya ada ila kwa uwezo tu wa Mungu nilifanikiwa.

Home hakuna hata mmoja aliyefika advance, ni mimi tu. Dada zangu karibia wote wanne walipata mimba na hawakuweza kusoma. Mmoja ameishia form four na akafeli.

Kaka zangi wawili wameishia la saba na kufeli kuingia form one.
Pata picha hapo maisha yalivyokuwa magumu. Ilifika wakati mtaani tulikuwa tunachekwa kwani tulijazana watu wengi ndani ya nyumba moja ndogo ya vyumba vitatu, na vyote uliishi humo kuanzia baba, mama, ndugu na watoto wote.

Narudi maisha ya chuo...Chuo sikuwahi kutembelea kumbi za starehe kwani sikuwa na pesa za kutosha, na ukizingatia DSM kila weekend wanachuo hufurika kumbi zote za starehe kula bata.

Nilivaa mavazi ya kimasikini japo si sana. Nilijitahidi kusoma kwa bidii na kwa uchungu mkubwa. Hakuna 'demu' yeyote aliyenipenda katika kipindi hiki, wote walinikwepa kama kinyesi. Ila sikuwa na kawaida ya kukopa kopa hela kwa watu au kulia lia shida hovyo. Kifupi nilikuwa ni masikini jeuri.

Sijui kilitokea nini ila kwa sasa ni manager katika shirika X la serikali hapa DSM, pia ni mkurugenzi wa body X ya shirika la serikali hapa DSM. Mishahara yangu yote miwili ni 8M plus marupu rupu, kwa mwezi.

Namshukuru Mungu kwa kunifuta machozi ya muda mrefu, na hayo ndiyo maisha niliyopitia chuo.

'Mungu na awaone wengj wanaopitia kipindi kigumu kwa muda huu'

Nawasilisha, karibuni tufarijiane na tukumbushane maisha haya ya uchungu.

Kwa sasa nashukuru Mungu wanangu wanaitwa WA KISHUA. Thanks
kwa maelezo yako bado hujatusua, ungesema una kampuni yako inayokuingizia kadhaa hapo ningekuelewa
 
Kwa sasa nashukuru Mungu wanangu wanaitwa WA KISHUA. Thanks lord![emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Ndugu zako unawakumbuka lakini
 
Back
Top Bottom