Mimi ni mmoja wapo wa tuliosoma advance kwenye hizi shule za
ufundi yaani Technical Secondary School wakati Olevel nimetokea
shule ambazo sio ya ufundi.
Shule zile ni zuri sana kwa Olevel kwa sababu wana jifunza ufundi
kwa vitendo, wana karakana na mitambo ambayo inawasaidia
kupata ujuzi.
Nakumbuka ilikuwa ikitokea shida/tatizo la umeme hao Olevel
wanao soma mkondo wa umeme (Electrical) wanakuja kutatua
wakati si tunao jiita form six tupo ila tuna theory tu ya Sayansi 🤣
Wanaume wazima tunakuja kubadilishiwa taa na wadada wa
form three au form four 🤣🤣🤣
HIvyo hivyo kwa issue ya maji plumber nao wanakuja kufix.
Nakumbuka mengi sana ila mengine mtayasema nyie
Mimi nilisoma Tanga School (Tanga Technical Secondary)
The first Government Secondary School in Tanzania.
SERVICE NOT SELF
Tanga shule ya Sifa.