Kwa nynda za juu kusini na Kusini;
Njombe unaweza kwenda kitulo ni mbuga ya Maua na ndege,sehemu moja nzuri kwa picha na hali ya hewa,hii ni makete.
Nyumbanitu na mashamba ya parachichi unaweza kuenjoy Njombe mjini.Njombe inafikika kwa gari kutokea Dar es salaam au Ndege ushukie Songwe,route zipo ila sio nyingi kwa uwanja wa Njombe.
Kuna route unaweza kutokea Kyela kwa boat ukaenda Ludewa ukarudi Njombe,hii ni zaidi ya utalii na unaweza kuunga Ludewa mpaka mbamba bay ukarudi Songea.
Mbeya kuna Tukuyu kuna lile ziwa la Mungu, pale Tukuyu kwa wale watu wa Misosi ni sehemu nzuri na katika kubadilisha hali ya hewa. Uzuri unaweza kutokea hapa ukaenda kitulo au ukatoka kitulo ukafika hapa.
Kyela kuna Beach nzuri Sana Sana na ziko Affordable sana ni wewe uchague kuanzia Ngonga au huku mwanzo kwenye landmark hotel. Mbeya na Songwe unaweza tumia gari au ndege kwa kutumia uwanja wa Songwe.
Songwe unaweza kutembelea Kimondo na wale wa hotel Utengule Hotel huku unakunywa kahawa Murua kabisa.
Iringa sio kuzungumza kwa hotel sio haba na ziko Affordable,kuanzia Ruaha ukamalizie Isimila na Agritourism ukiienjoy vizuri. Unaweza tumia gari au Ndege kutokea Dar au Dodoma.
Ruvuma ukiwa na usafiri private utaenjoy,hotel Songea mjini zipo,unaweza kutembelea mji mdogo wa historia Peramiho utaona mengi,kuna Milima Matogoro nao Una view nzuri lakini makumbusho ya majimaji na maeneo mengi yenye historia ya nchi hii na hayajulikani kabisaa
Mbinga kuna Liparamba na mwisho ziwani,bado kuna mengi ya kuyaona hapo katikati iwe katika kilimo au mazingira ya kuvutia mengi sana.Unaweza tumia gari bus au private kutokea Dar, unaweza kupitia iringa au Lindi.
Mtwara unaweza kupumzika Masasi mjini au Mtwara kutegemea na unakotaka kwenda.
Ukiwa Masasi unaweza kupanda Ile Milima na ukapata mtulizo wa kimawazo huku unaangalia mji,unaweza kutembelea Kanisa kongwe la Anglican,unaweza kwenda Mji mdogo wa Ndanda lakini pia ukamove mpaka Newala ambako ni juu ukajionea hali ya hewa ya tofauti na mazingira pia, hii route unaweza kutembelea maeneo ya hifadhi ya Mpombe na hata mto Ruvuma pia.
Mtwara mjini unaweza kuanzia mikindani pale kuna Old boma,ukaenda mjini kuna msangaa mkuu na mwisho Msimbati,kwa sasa Msimbati kuna beach lodge ya upekee hakika utaenjoy.
Ukiwa Mtwara unaweza kufanya evening walking beach au feri na kuenjoy samaki wa aina mbali mbali. Malazi sio ghari.Mtwara unaweza kutumia bus kutokea Dar au Ndege.
Lindi kwa ukweli kuna Option moja sababu option ya Lindi mjini unaweza kutokea Mtwara mjini ukaenda Lindi,kuna beach nzuri pale na kuna Rondo natural Reserve kule Rondo plateau,ni experience nzuri sana kisha unarudi Lindi, wale wa kilimo unaweza kuenjoy mashamba ya Nazi kule Ng'apa na mashamba ya chumvi kwa wingi,unaweza kumalizia beach ya mchinga (full white sand)
Kilwa. Hakuna asiyepajua kuna mengi na wengi ukweli hawaijui vizuri, unaweza kutokea moja kwa moja kwa gari tokea Dar es salaam.