Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Kumbe nawe ni mmoja wa Bwiru Wasichana!! [emoji23]
Tukiwaita Mende enzi hizo! Mdada wa Bwiru niliyeruka naye debe la welcome form one hatimaye sasa ni mama wa wanangu! Mlikuwa mnatuzingua na Nsumba lakini nilikuwa nawaelewa sana kuliko Nganza!
Eeh na sisi tulikuwa tunawaita wadudu wa kwenye maharage lol
Jamani sikuwahi kwenda bugi, hongereni sana
 
Kumbe nawe ni mmoja wa Bwiru Wasichana!! [emoji23]
Tukiwaita Mende enzi hizo! Mdada wa Bwiru niliyeruka naye debe la welcome form one hatimaye sasa ni mama wa wanangu! Mlikuwa mnatuzingua na Nsumba lakini nilikuwa nawaelewa sana kuliko Nganza!
Waooo!!hongera mazee
 
Ukiwakuta sasa walivyoshamiri kwenye maharage, na ole wako kaka masanja akufume unadabodisha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], alikuwa na uchungu na kile chakula kama anakinunua yeye.....Bila kumsahau baba Lucy...Mama Anord msukuma wa watu hakuwa na neno kabisa...Maisha haya dah!

Nakumbuka siku ya kwanza naripoti ilipofika jioni baada ya kukiona kile chakula (ilikuwa ugali + beans) wadudu weupe wanaelea...Nilidondosha chozi walahi.....
 
ha ha umenikumbusha mbali sana aisee. Me term ya kwanza yote sikugusa ugali, muda wa ugali nilikuwa naassume tu nimeshiba. , na hivi ijumaa ilikuwa siku ya suti mmh. Ila baadaye nilizoea vizuri tu.

unamkumbuka yule mpiga picha alikuwa anaitwa kaka phonce, kama sijasahau na dada vero wa canteen?
Ndio nawakumbuka vizuri....mdomo wake kuufumba ilikuwa kazi[emoji38][emoji38]

Hivi ulipata taarifa mafyekeo alishaiaga dunia??
 
Sikumkuta mkuu.

Nilifundishwa na Rung'wecha, alikuwa bingwa wa Maths sana miaka hiyo.
Ila ajabu nilienda mpaka chuo nikaja kubanana naye chuoni tukawa tunagombani ama shuttle.

Yani mwalimu wako amekufundisha shule na ulikuwa unamkubali balaa halafu unakutana naye chuoni, hapo ndipo unakuja kugundua kumbe alikuwa wa kawaida tu.

Maisha haya hayako fair kabisa.
Alikuwaga amesoma FTC, sisi tulipoenda pale kuanzisha A level akawa anavunja namba, aliacha rasmi kufundisha o level. Baada ya semester moja akala shavu LA engineer wa wilaya ya misungwi. Ndo akaona umuhimu wa kurudi shule kutafuta degree.
 
Aisee hongera sana.. Hivi hii mende ilitokana na nini?
Asante sana, tuligandana tukaenda Tabora A-level, yeye Girls mimi Boys, baada ya Chuo tukawa mwili mmoja!
Aisee jina la Mende tulilikuta origin yake hakuna aliyekuwa na uhakika ila niliwahi kumwuliza anko alimaliza Boys 1988 alisema those days halikuwepo it seems lilianza in early 90's
 
Masaba pia keshafariki.

Unamkumbuka??
Alikuwa ana kilema cha mguu anafundisha Electrical.

Pia nasikia Baunsa yue mashoto yuko jela, amefungwa kwa kosa la kmpiga mkewe mpaka akaua.
Baunsa alitoka miezi sita badae, nimemaliza 2010 na alitoka akarudi pale pale na mwaka 2013 nilienda nkakuta ndo kafanywa mwalimu wa nidhamu
 
Asante sana, tuligandana tukaenda Tabora A-level, yeye Girls mimi Boys, baada ya Chuo tukawa mwili mmoja!
Aisee jina la Mende tulilikuta origin yake hakuna aliyekuwa na uhakika ila niliwahi kumwuliza anko alimaliza Boys 1988 alisema those days halikuwepo it seems lilianza in early 90's
Hongereni kwakweli na muendelee kudumu.[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]..
 
Back
Top Bottom