Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Mzee chigugu hahahaha...kisuu alipiga pesa akahamishiwa kashule ka kata kanaitwa Buigiri kapo chamwino dodoma, akaenda akahonga zile pesa akapelekwa nadhani Tosamaganga kule iringa, akastaafu saa hii anakula.pensheni yake kajenga na anaishi Moshi. Mtoto wake mkubwa Sarah alikuwa rafimi yangu mzuri tu
He he he he
Kumbe unamfahamu mpaka binti yake??

Pamoja na utukutu wote wa Kissuu ila kwa sasa kawa mtu poa sana.
Kuna grupu moja ya Wassap tulikuwa naye, vijana kwa hasira wakamleftisha fasta.
teh teh teh

Chigugu mzee wa watu alikuwa hana maneno na kaofisi kake kalikuwa pembeni ya duka la shule pale.
Kweli maisha tunatoka mbali sana.
 
Hakuna kitu kama hicho..
Halafu siku hizi umetukimbia kule kwenye uzi wetu pendwa.
Kule huwa nakuja, japo si mara kwa mara.

Tatizo nimekuwa nikichangia nyuzi nyingi sna humu jukwaani, sasa inabidi utumie muda mwingi kujibu quotes za watu.
Ila nitarudi weekend hii
 
Kawa Kilema alikuwa anachechemea???
Yap. Sasa sijui kama alikua na jeraha mguuni au ndo alivyo. Personally sikuwahi kumpenda. Kuna siku tulikutana kwenye gari natoka mjini sijavaa uniform. Tulivyoshuka akanidaka alinipiga makofi mawili palepale kituoni
 
Nakumbuka maisha ya Bwiru Boys miaka hiyo ilikuwa full mikasa.

Kulikuwa na eneo linaloitwa Mombasa, mahali ambapo vijana wa Boys walikuwa wanazama kuwapiga chabo mabinti wa girls pindi wanaoga.
Sehemu hii ilikuwa maarufu sana maana upande wa Ziwa waiokuwa wanautumia wasichana wa Girls maarufu kama "mende" ulikuwa unatenganishwa na upande wa boys kwa kilima fulani hivi kina mawe ya hatari, lakini vijana walikuwa wana risk life kwenda kula chabo.

Nakumbuka ishu ya headmaster wetu kupindi hicho kulikuwa na tetesi kuwa anapita na mistress wa Nganza, sasa kimbembe kilikuwa ole wenu siku ya debate au bugi(disko) mtoe pendekezo la kuwaleta Bwiru Girls, headmaster ataahirisha hata hilo disko, ila mkimletea mabinti wake wa Nganza, hata usafiri atawapa free.

Nakumbuka misemo maarufu kama kuguga likimaanisha kupiga msuli au kusoma, msemo kama kugenya likimaanisha kufariki, msemo kama fororo ukimaanisha uji usio na sukari, msemo kama mnyambo ukimaanisha mtu mwenye tabia za ubaguzi na kujisikia sikia , msemo kama kudabo ukimaanisha kudrudia msosi mara mbili, form one wakiitwa nguruwe na mingineyo mingi.

Nakumbuka pia visa vya mwanafunzi mmoja alikuwa shombe shombe alikuwa bingwa wa kupita na wake za maticha, mpaka akazaa na mke wa ticha mmoja hivi(Jina tunalihifadhi), akazaa kijana shombe shombe na kuleta mtikisiko mkubwa sana kwenye ndoa ya ticha wetu.

Walimu kama Mazebele, Rung'wecha, Begenyeza, Kissuu, Mchizi Mox, Massaba(R.I.P), Ruhiye(R.I.P) na wengineo wengi.

Nasikia pia kuwa hata Founder wa Forum hii muheshimiwa sana Maxence Mello ni product ya Luthuli Domitory pale njia ya kuelekea ukarani na alikuwa ngugi kweli kweli(just kidding).

Tukumbushane life ya Bwiru aisee.

12651326_10201448336607019_3786303634314722495_n.jpg
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
 
Yap. Sasa sijui kama alikua na jeraha mguuni au ndo alivyo. Personally sikuwahi kumpenda. Kuna siku tulikutana kwenye gari natoka mjini sijavaa uniform. Tulivyoshuka akanidaka alinipiga makofi mawili palepale kituoni
Ha ha ha ha
Jamaa alikuwa na kiburi fulani hivi mpaka kinakera.

Ila kawa mtu mstaarabu sna sasa hivi, Nafikiri kuna kitu alijifunza kwenye maisha yake baada ya kutoka Bwiru
 
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
Mkuu ulikua mwana casfeta nini, maana hao ndo walikua sio wadau wa mombasa
 
He he he he
Kumbe unamfahamu mpaka binti yake??

Pamoja na utukutu wote wa Kissuu ila kwa sasa kawa mtu poa sana.
Kuna grupu moja ya Wassap tulikuwa naye, vijana kwa hasira wakamleftisha fasta.
teh teh teh

Chigugu mzee wa watu alikuwa hana maneno na kaofisi kake kalikuwa pembeni ya duka la shule pale.
Kweli maisha tunatoka mbali sana.

Mzee Chigugu na kigugumizi chake hahaha!

Yupo bado mwanza naeneo ya Mnalani kajenga katulia!

Kisuu kapooza sana!....baada ya kustaafu mambo hajamwendea sawa!

But yupo njema sana. Nashukuru Mungu kwa Afya yake
 
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
Teh teh teh
Hukuwahi kuhudhuria mombasa??
Vipi Ukarani??

Hukuwahi kwenda kuiba mahindi ya shule na kuyaloweka usiku kucha kwenye maji asubuhi yalainike ili uyachome??
 
Back
Top Bottom