Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Ha ha ha ha
siku hiyo nilikuwepo mkuu.

Ila japo jamaa alikuwa anaiba kweli ila tulimdhalilisha sana yule mzee.
Haiwezekani kwa kujituma kote kule tumdhalilishe vile, sema basi tena mambo ya mob psychology.

Siku hizi kastaafu tayari.

Unamkumbuka yule mpishi form one??
Unamkumbuka Bandhiho??
Unamkumbuka mnyama Nyemenohi, mzee wa kitambi kikubwa mpaka kinataka kugusa chini??
Unamkumbuka ticha scorpion??
Sio Nyemenehi ni Nyamanohi hahahahaa
 
Mwalimu nani pale Musoma Tech? Maana kuna mwalimu Muganyizi baadae akarudi Boys na kustaafia pale.

Amejenga jirani na shule kuke kijijini!

Pia Chigugu mnamkumbuka? Hahahaaa Bwiru Boys hatari sana!

Nilienda pale miaka ya 2000 katikati nikamkuta mkuu mpya anaitwa Kisuu, Mnyaturu flani, tukabadilishana namba jioni tukakutana SPAROW maeneo ya Ghana kula kilaji!

Aisee anazimeza sana. Ni mtu poa sana!

Dah nimepamisi Mwanza for real!
Mwalimu Begenyezaa likuwa na macho mekundu fulani hivi anafundisha kozi za Civil Engineering hasa hasa Brickwork.

Mwalimu Muganyizi gani unayemzungumzia, maana yule aliyekuwa anafundisha Engineering Science baadaye alikuwa Second Master, tulikuwa tunamuita Bega, Pia alikuwepo Muganyizi mwingine maarufu kama mjomba, huyo alishafariki kitambo.

Chigugu Dokta namkumbuka sana na Kigugumizi chake, keshastaafu na yeye, alikuwa anaishi kwenye nyumba za mawe njia ya kama unakwenda Brweries kwa nyuma nyuma kule.

Kissuu alikuwa mtu poa sana, ila alikuwa mmoja wa waalimu makatili sana na walioiharibu ile shule.
Keshastaafu sasa hivi anakula tu pensheni yake.
 
Sio Nyemenehi ni Nyamanohi hahahahaa
Nyamanohi??

Tulikuwa tunamuita kifupi tu , Nyeme.

Jamaa aliwahi kuuza samani zote za ndani kwenda kuangalia kombe la Dunia Brazili nafikiri.
Ile TV tuiyokuwa tunatumia school enzi hizo ilikuwa ya kwake.

Jamaa alikuwa anakula fegi hatari.
 
Nyemenohi alikua na tabia mbaya sana, akikuta mmekaa mnapiga stori anapita nyumna kimyakimya. Akishawavuka tu anawauliza kwanini hamjamsalimia hapo mtachezea stick za kutosha.
Akikudaka lazima ukachimbe uwanja kuupanua kule walikokuwa wanakaa washangiliaji...
 
Yap
Alipiga hela ndefu sana pale.

Kuna yule mjepu alikuwa anafundisha plumbing, alitoa Milioni 50 za kujenga mabweni.
Kisuu akazinywa, akatumia kama milioni 8 hivi akamiksi na matofali yetu ya adhabu akasimamisha library na mabweni.

Unaikumbuka katara??
Unamkumbuka Chigugu??
Mzee chigugu hahahaha...kisuu alipiga pesa akahamishiwa kashule ka kata kanaitwa Buigiri kapo chamwino dodoma, akaenda akahonga zile pesa akapelekwa nadhani Tosamaganga kule iringa, akastaafu saa hii anakula.pensheni yake kajenga na anaishi Moshi. Mtoto wake mkubwa Sarah alikuwa rafimi yangu mzuri tu
 
Mzee chigugu hahahaha...kisuu alipiga pesa akahamishiwa kashule ka kata kanaitwa Buigiri kapo chamwino dodoma, akaenda akahonga zile pesa akapelekwa nadhani Tosamaganga kule iringa, akastaafu saa hii anakula.pensheni yake kajenga na anaishi Moshi. Mtoto wake mkubwa Sarah alikuwa rafimi yangu mzuri tu
Kisuu nilikutana naye mwaka 2013 Iringa, tulikutana hotelini. Lakini nilimuona kama kawa kilema kidogo
 
Back
Top Bottom