Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

He he he he
Kumbe unamfahamu mpaka binti yake??

Pamoja na utukutu wote wa Kissuu ila kwa sasa kawa mtu poa sana.
Kuna grupu moja ya Wassap tulikuwa naye, vijana kwa hasira wakamleftisha fasta.
teh teh teh

Chigugu mzee wa watu alikuwa hana maneno na kaofisi kake kalikuwa pembeni ya duka la shule pale.
Kweli maisha tunatoka mbali sana.
 
Hakuna kitu kama hicho..
Halafu siku hizi umetukimbia kule kwenye uzi wetu pendwa.
Kule huwa nakuja, japo si mara kwa mara.

Tatizo nimekuwa nikichangia nyuzi nyingi sna humu jukwaani, sasa inabidi utumie muda mwingi kujibu quotes za watu.
Ila nitarudi weekend hii
 
Kawa Kilema alikuwa anachechemea???
Yap. Sasa sijui kama alikua na jeraha mguuni au ndo alivyo. Personally sikuwahi kumpenda. Kuna siku tulikutana kwenye gari natoka mjini sijavaa uniform. Tulivyoshuka akanidaka alinipiga makofi mawili palepale kituoni
 
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
 
Ha ha ha ha
Jamaa alikuwa na kiburi fulani hivi mpaka kinakera.

Ila kawa mtu mstaarabu sna sasa hivi, Nafikiri kuna kitu alijifunza kwenye maisha yake baada ya kutoka Bwiru
 
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
Mkuu ulikua mwana casfeta nini, maana hao ndo walikua sio wadau wa mombasa
 
Mzee Chigugu na kigugumizi chake hahaha!

Yupo bado mwanza naeneo ya Mnalani kajenga katulia!

Kisuu kapooza sana!....baada ya kustaafu mambo hajamwendea sawa!

But yupo njema sana. Nashukuru Mungu kwa Afya yake
 
Daaaadek, we jembe umenirudisha home kabisa!!! Bravo Bwiru boys, live long *mangugi* Wote!! Ni bahati mbaya tu sikuwahi kukanyaga Mombasa, Sina cha kusimulia huko.
Teh teh teh
Hukuwahi kuhudhuria mombasa??
Vipi Ukarani??

Hukuwahi kwenda kuiba mahindi ya shule na kuyaloweka usiku kucha kwenye maji asubuhi yalainike ili uyachome??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…