Wale wa home made products, njooni hapa

Wale wa home made products, njooni hapa

JINSI YA KUTENGENEZA KIWI (DAWA)YA VIATU

MAHITAJI

√bee wax (nta ya nyuki) ¼kilo
√mafuta ya zeituni vijiko 5 vya chakula
√brown oxide au black oxide-inapatikana SIDO au Allied chemicals

Nitatoa namba mwishoni ya Allied chemicals kwa atakayehitaji ataagiza.

MCHAKATO

Chukua sufuria liweke kwenye moto wa kadri, kisha weka maji kwa sufuria kidogo tu kama nusu lita hivi kisha weka bakuri la plastic lielee juu ya maji alafu chukua nta yako igawanyishe mara mbili (nusu ya robo) alafu nusu ya kwanza itunze tu kwa matumizi ya wakati mwingine, alafu nusu ya pili ikate kate vipande vidogovidogo kisha viweke kwenye bakuli linaloelea kwa maji yanayoendelea kupata moto

Weka mafuta ya zeituni vijiko 5 pamoja na nta na anza kukoroga taratibu mpaka mchanganyo uyeyuke kabisa na baada ya hapo weka kijiko kimoja na nusu cha black au brown oxide(usiweke zote) Kisha endelea kukoroga mpaka mchanyato wako uungane kabisa, kisha mwaga huo mchanganyo kwa kopo lako safi na liache kwa nusu saa hivi lipoe kabisa na tayari mambo yatakuwa murua kabisa

Tumia dawa yako ya viatu kadri upendavyo
 
kuna dhana tatu hapo 1.ndoo ya plastic 2.maji ya mchele lita 2 3.koustic soda.

Maelezo.

Ni marufuku, kutumia chombo chenye asili ya chuma kuyeyusha koustic kwa sababu kitayeyuka chenyewe, tumia ndoo au chombo cha aluminium au plastic hasa plastic.

Kuyeyusha koustic nusu kilo unahitaji maji lita nne, hivyo baada ya kupata mchanganyo kwa hizo siku 2 au 3 na kutoa kiasi unachohitaji utatunza inayobaki kwa ajili ya matumizi ya wakati mwingine au la utaimwaga tu.
Asante mkuu, swali jingine ujafafanua mafuta yawe kiasi gani
 
MALIGHAFI

✓Maji ya mchele
✓kaustiki soda
✓mafuta ya mise au Nazi

Hatua ya kuandaa

Andaa ndoo Lita 20 weka maji yalio oshewa mchele kwenye ndoo Lita 4

Kisha weka kaustiki soda nusu kilo kisha koroga kwa muda Wa dakika 5 kisha hifadhi sehemu salama kwa muda Wa siku 2 hadi 3

Baada ya siku 3

Anza kuchemsha mafuta ulionayo kama ya Nazi au mise au ya mawese hakiksha yanapata moto na kua na vuguvugu (yasichemke sana)

Baada ya hapo kata kidumu cha Lita 5 kwa juu kisha weka maji Yale ya mchele ulio changanya na kausti weka nusu Lita kisha weka mafuta yako Lita moja kisha koroga kwa haraka na muda mfupi utaona mchanganyiko Wako umekua mzito kama uji

Mimina na utie katika umbo na acha ikauke

Itakauka kwa muda wa masaa 6 hadi 8

Baada ya kukauka utapata sabuni ambayo inaondoa vipere usoni na kuacha uwe nyororo kabisa
Usinichoke, na hapo kwenye kukata kidumu Cha lita tano inabidi , kwenye dumu umesema niwekee kiasi gani Cha mchanganyiko, na mchanganyiko ule unaobakia kwenye ndoo wa kumwaga au inakuwaje?
 
Usinichoke, na hapo kwenye kukata kidumu Cha lita tano inabidi , kwenye dumu umesema niwekee kiasi gani Cha mchanganyiko, na mchanganyiko ule unaobakia kwenye ndoo wa kumwaga au inakuwaje?
Maji ya mchele yaliyochanganyika na kaustic ni ½ lita tu na hizo lita 3 za mafuta
 
Halo halo haloo...? Ndio IGP, yes napiga simu toka JF mkuu... Eeh, ndio ndio mkuu tulikua tunahitaji ulinzi mkuu kuna thread ina madini sana mkuu, eeh ndio.. Ahaa.. Sawa sawa shukrani mkuu!.
 
MALIGHAFI

✓Maji ya mchele
✓kaustiki soda
✓mafuta ya mise au Nazi

Hatua ya kuandaa

Andaa ndoo Lita 20 weka maji yalio oshewa mchele kwenye ndoo Lita 4

Kisha weka kaustiki soda nusu kilo kisha koroga kwa muda Wa dakika 5 kisha hifadhi sehemu salama kwa muda Wa siku 2 hadi 3

Baada ya siku 3

Anza kuchemsha mafuta ulionayo kama ya Nazi au mise au ya mawese hakiksha yanapata moto na kua na vuguvugu (yasichemke sana)

Baada ya hapo kata kidumu cha Lita 5 kwa juu kisha weka maji Yale ya mchele ulio changanya na kausti weka nusu Lita kisha weka mafuta yako Lita moja kisha koroga kwa haraka na muda mfupi utaona mchanganyiko Wako umekua mzito kama uji

Mimina na utie katika umbo na acha ikauke

Itakauka kwa muda wa masaa 6 hadi 8

Baada ya kukauka utapata sabuni ambayo inaondoa vipere usoni na kuacha uwe nyororo kabisa
Kupata maji ya mchele 4ltrs natakiwa kuosha mchele kiasi gani?
Je naweza nikasaga mchele nipate unga halafu nikakoroga kwenye maji ya kawaida halafu nichanganye na kaustic? Nitapata matokeo niyatakayo
 
Halo halo haloo...? Ndio IGP, yes napiga simu toka JF mkuu... Eeh, ndio ndio mkuu tulikua tunahitaji ulinzi mkuu kuna thread ina madini sana mkuu, eeh ndio.. Ahaa.. Sawa sawa shukrani mkuu!.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimetuma ulinzi tayari
 
Samahani hizi hizi vitamin C za vidonge unazisaga ama zipo special kwa matumizi kama hayo?
Kuna unga special mkuu, ukipenda utatumia pills
Screenshot_20210225-185813~2.jpg
 
TENGENEZA DAWA YA MENO(TOOTH PASTE) UKIWA NYUMBANI

NJIA YA KWANZA

1.Chukua baking powder (chapa maandashi) - kijiko 1 cha chakula

2.Chukua essential oil - weka matone 3

3.weka maji matone 5

Changanya vizuri mchanganyo huo, na utakuwa tayari kwa matumizi

NJIA YA PILI

1.Chukua baking powder - kijiko 1 cha chakula

2.chukua chumvi kijiko 1 pia

3.ongeza matone matatu ya essential oil

4.weka maji matone machache

Changanya vyema mchanganyo huo na tayari kwa matumizi

Pitia link hapo kuangalia uhalali wa ingredients hizo (zimethibitishwa na zinafaa tu kwa matumizi ya binadamu)
 
Kwa wale wa Mwanza wanaohitaji essential oils angalia hapa chini, na kwingineko jaribuni cosmetics shop au supermarkets.
Screenshot_20210225-193826~2.jpg
 
NJIA YA TATU

1. Chukua vijiko 2 vya baking powder

2.Weka vijiko 2 vya coconut oil

3.Weka matone 10 ya essential oil

kisha changanya vyote kwa pamoja mpaka mchanganyo uwe mwepesi (sio mwepesi Sana) utakuwa tayari kwa matumizi.
 
Back
Top Bottom