Wale wa home made products, njooni hapa

Wale wa home made products, njooni hapa

Kwa Dar Es Salaam vifaa vya kutengenezea (chemicals) vinapatikana wapi.
 
mada nzuri sana. naomba kufahamu wapi nitapata mafuta ya manjano/turmeric kwa matumizi binafsi.
 
Hii chemical napata wapi wakuu.

Screenshot_20210806-174436_Chrome.jpg
 
NAMNA RAHISI YA KUTENGENEZA AIRFRESHER.

VITU MUHIMU
1.MAJI YALIYOTOKANA NA MVUKE
2.MARASHI UYAPENDAYO WEWE(FRUITY NI NZURI)
3.TAFUTA MKEBE SAFI WA KUWEKEA MARASHI YAKO

MBINU.

JIFUNZE NAMNA YA KUVUNA MAJI YA MVUKE (NI RAHISI ULIZA)

KISHA MIMINA MAJI YAKO KWENYE MKEBE SAFI, NA UMIMINE PERFUME KIDOGO AU NYINGI KULINGANA NA MAPENZI YAKO, THEN UR DONE, WEKA MKEBE WAKO SEBULEN AU KWENYE GARI AU MAHALI KOKOTE (ISIWE SEHEMU YA WAZI SAANA) FURAHIA HARUFU SWAFII KABISA MUDA WOTE.
 
Swali:
Essential oils ni nini na zipo za aina ngapi?

Majibu plz!
Essential oil ni mafuta ya asili ya mimea na mazao ya mimea, mafuta haya huwa hayawekewi vitu va ziada kuyaongezea thamani...hivyo sifa yake ni uasili wake, hata harufu sio boosted ni Ile ya asili kabisa, Hali kadharika rangi Huwa ni ya asili kabisa
 
Unaweza kujisomea kuhusu aina zake, lakini Kwa length ya wingi wa mimea na products zake ndiyo wingi halisi wa essential oils..
 
Essential oil ni mafuta ya asili ya mimea na mazao ya mimea, mafuta haya huwa hayawekewi vitu va ziada kuyaongezea thamani...hivyo sifa yake ni uasili wake, hata harufu sio boosted ni Ile ya asili kabisa, Hali kadharika rangi Huwa ni ya asili kabisa
Sawa mkuu. Kwa hiyo zote zinafaa kutengenezea dawa ya meno?
 
JINSI YA KUTENGENEZA LOTION KWA NJIA RAHISI KABISA.

Tanabahi: mahitaji yote yanapatikana maduka ya vipodozi, maduka ya dawa (baadhi) na mengine ni kwa mazingira yetu ya kila siku

MAHITAJI

✓Mafuta ya nazi (yanapatikana)
✓Aloe Vera gel (duka la vipodozi)
✓Rose water (jaribu supermarkets)
✓Glycerin(inapatikana)
✓Vitamin e Capsule/oil (duka la vipodozi)

UTARATIBU

Weka kwenye bakuli safi kijiko kimoja cha chakula cha aloe vera gel (ya dukani iwe 100% natural)

Ongeza kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya nazi pamoja na glycerin na rose water kisha ongezea na vitamin e kama ngozi yako ya mafuta tumia capsule kama kavu unaweza kutumia vitamin e oil

Changanya vizuri mpaka ichanganyike na uone imekua na rangi ya kupendeza na ipo laini kisha hifadhi kwenye kichupa safi tayari kwa matumizi

utadouble au kutripple malighafi kulingana na mahitaji yako

Note: chukua mahitaji kwa ujazo mkubwa na utakuwa na unatoa kidogo kidogo kila mara lotion ikiisha.

Mfundishe mtoto na mkeo wajikomboe kwa suala la manunuzi ya lotion, sio muda ntaweka formula nyingine ya lotion ntaunganushia na ya mafuta ya mgando.
Ooh
 
Back
Top Bottom